Sofia Mjema kushauri ndoa za utotoni

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,412
a.jpeg


Leo 22-10-2023 Serikali imetengua nafasi ya Katibu uenezi wa CCM -Sophia Mjema ambaye hajadumu hata kwa miezi 3 kutokana na kupwaya sana na baada ya nafasi ya kumuweka kukosekana imetengenezwa nafasi ya kuwa mshauri wa Raisi mambo ya wanawake na watoto;

Serikali imesaini mkataba waDP World na ili kuhamisha mjadala wakamteua Makonda ili watu wakose cha kujadili, wabaki na Makonda huku DP World imepita.
Serikali imeshindwa tena katika kesi ya ndoa za utotoni baada ya Mahakama ya Rufaa nchini humo kutupilia mbali pingamizi la serikali liliokuwa likitaka sheria ya ndoa chini ya miaka 18 iendelee.

Serikali ilikata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyotoa ushindi kwa watetezi wa haki za binadamu (Msichana Initiative) waliokuwa wakipinga baadhi ya vipengele vya sheria ya ndoa kwa madai vilikuwa vikimkandamiza mtoto wa kike.

Uamuzi wa mahakama hiyo ya rufaa unakamilisha safari ya miaka mingi ya watetezi wa haki za binadamu wakipigania ustawi wa mtoto wa kike ambao unadaiwa kukandamizwa na sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Katika shauri lao mbele ya mahakama kuu na baadaye mahakama ya rufaa, asasi za kiraia zilidai kitendo cha sheria ya ndoa kutamka kwamba mtoto wa kike anaweza kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 wakati yule wa kiume anaweza kuoa akiwa na umri wa miaka 15, inakandamiza ustawi wa watoto wote na pia inaleta mazingira ya kibaguzi kwa watoto hao jambo ambalo ni kinyume cha katiba ya nchi.

Mmoja wa mawakili wa upande wa walalamikaji, Alex Mngongolwa amesema, sheria hiyo ya ndoa, siyo tu kwamba ilikuwa inakiuka misingi ya katiba ya nchi, lakini pia ilikuwa haiowani na mikataba mingi ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Wachambuzi wa haki za binadamu wanasema kutenguliwa kwa sheria hiyo kunaweza kukawa ni habari njema kwa mamilioni ya watoto hasa wale walioko maeneo ya vijijini ambako wamekuwa waathirika wakubwa wa ndoa za utotoni.

Ripoti nyingi za tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa watoto wengi hushindwa kuendelea na masomo kutokana na ama kulazimishwa kuolewa au kupachikwa mimba kutoka kwa wale wanaojulikana kama ‘mabazazi’ yaani wanaume wenye kupenda kuwarubuni kingo’ono watoto wa kike.

SOPHIA Mjema ni muislamu na hawezi kushauri watoto waolewe wafikapo miaka 18, najua tu atashauri vitoto vikifika 14 years violewe.

Wewe baba , mama ambaye unajiita kada wa chama au chawa, kaa hapo sebuleni, mwangalie binti yako aliyeko Form One ambaye ahat nywele za ukeni hazijaota, mwangalie mwanao wa 14 years ambaye hata maziwa hayatokeza vizuri na hajui brazia/sidiria , fikiria binti yako ambaye hata kujitambua kuwa ni msichana hajajua, fikiria binti yako huyo hapo ameshika rimoti u, huyo unatoka naye kwenda mlimani City kutembea na anakula popcorn na kucheza na watoto wenzake WIKI IJAYO linakuja li- bazazi kutoa Mahari.
Yaani Serikali ilikata rufaa baada ya mahakama kusema watoto waolewe wakifika 18 years, ikataka iwe 14 years.
Serikali imeelekezwa kubadili hiyo sheria mbaya zaidi katika Tanganyika lakini imesususa!

Mjema, tunasubiri ushauri wako kwa Raisi.
 
Back
Top Bottom