Kulipa kodi kubwa sio sifa

Kulipa kodi kubwa sio sifa

Kuna ndugu yangu alijitutumua na kupanga nyumba ya 1M bahari beach. Nadhani alitaka kumaintain standard kwa sababu nyumbani kwao ni hukohuko.
Asee Madeni yalitaka kumuuwa kuanzia kazini hadi Madeni ya mtaani alikuja fukuzwa kwenye nyumba na hapo anadaiwa kodi ya miezi sita sasa hivi yupo juu ya mawe karudisha mpira kwa kipa.
Mimi siwezi kabisa kujitutumua kwenye vitu ambavyo sina uwezo navyo kufurahisha watu, kodi yangu ya pango ni asilimia 5 tu ya taje home yangu.
Huyo alizingua sana,na wapo watu wengi sana wanaumia kwa kutaka show off za kijinga

Fanya jambo kwa uwezo wako,iwe kwa kila kitu sifa zitakupeleka pabaya sana
 
Huyo alizingua sana,na wapo watu wengi sana wanaumia kwa kutaka show off za kijinga

Fanya jambo kwa uwezo wako,iwe kwa kila kitu sifa zitakupeleka pabaya sana
Ndio kikubwa kila mmoja aishi kwa uwezo wake. Kipindi cha nyuma nilikurupuka kwenda kupanga nyumba ya gharama kidogo kulinganisha na kipato changu baada ya miezi sita ya kwanza kuisha pesa niliyonayo mkononi haitoshi nikaongea na mwenye nyumba nikaanza kulipa miezi mitatu asee ndani ya mwaka mzima sikufanya jambo lolote la maana kila nikigeuka kodi imefika nikawa kama nimekuja mjini kumfanyia mwenye nyumba kazi. Ikabidi nikimbie
 
Bahati nzuri uliona tatizo na kulitafutua ufumbuzi,ila kuna wengine wapo kwenye hiyo shida mapaka leo,na hawajajua bado kuwa wapo kwenye shida

Inasemwa Kodi yako isizidi asilimia 40 ya kipato chako
 
Hellow wa JF.

Utasikia vijana wakisema mimi siwezi kukaa/kupanga chumba/nyumba chini ya 300,000 au 500,000 au 800,000 kwa mwezi. Hapo hapo siku za mbeleni anakuja kuzalisha/zalishwa watoto kwenye nyumba za watu hana kiwanja wala nyumba.

Naomba niwakumbushe hakuna tuzo utakuja kupewa ya kulipa kodi kubwa.
ok 🤝
 
Back
Top Bottom