baharia 1
JF-Expert Member
- Sep 13, 2019
- 2,989
- 4,369
*Hivi Mlioaminishwa Kujenga ni Ushamba Mna Akili Ama MMEROGWA? *
Huku mtaani na mtandaoni kumezuka wimbi la vijana wa hovyo kabisa wanaoingia kwenye mkumbo wa kijinga.
Mtu anaibuka na kuanza kuhubiri upumbavu kwamba kujenga ni ushamba na fedha inatakiwa izunguke, bora ununue gari kali mjini na ukae nyumba ya kupanga kali.
Huu ni ufala wa kiwango cha lami unaotokana na ulimbukeni wa maisha na kutokujua kesho.
Wewe mpumbavu unayejiita mwanaume timamu, una mke na watoto, halafu huna hata kipande cha ardhi chenye bati lako mwenyewe, hivi una akili timamu kweli?
Wewe mshenzi wa tabia unajiona umeyapatia maisha kisa unaendesha chuma cha bei mbaya mjini huku mwenye nyumba wako akikukohoa kidogo tu unatetemeka
Eti money rotation, rotation gani wakati huna hata msingi ulioweka chini? Acha useng, jenga kwako mpuuzi wewe!
Ipo siku utajuta sana. Ugonjwa na dharura hazina hodi. Kesho ikitokea ukapata tatizo linalokulaza kitandani mwaka mzima bila kuingiza hata senti mia, huyo mwenye nyumba wako atakuvumilia miezi mingapi?
Kuendesha gari la milioni 30 au 40 huku unalala kwenye nyumba ya mtu mwingine ni sawa na kuvaa suti kali ya bei mbaya juu halafu ndani hujavaa Kitu, siku upepo ukivuma kidogo tu, aibu yako inakuwa wazi kwa kila mtu.
Kama unadhani hii ni michezo,
msikilize huyu mshenzi mwingine anaitwa Kelvin uone jinsi upumbavu na show-off zinavyoweza kuangamiza damu yako mwenyewe.
Kelvin alikuwa mtoto wa mjini wa kuitwa, mpenda mademu, na mtu wa starehe asiyetaka kabisa kusikia habari za kujenga. Mjini hapa kila mtu alijua Kelvin yuko juu, kila baada ya miezi miwili au mitatu alikuwa anabadilisha gari na kutembea na chuma mpya kabisa. Kumbe nyuma ya pazia alikuwa anafanya upumbavu wa kwenda kukopa fedha na kufanya top-up ili amwage gari la zamani achukue jipya kwa mkopo.
Kazi yake kubwa ilikuwa kutusimanga sisi tunaopandisha matofali polepole uswahilini kwamba tuna akili za kishamba. Yeye alikuwa anakaa kwenye jumba kali la kupanga na kuigiza maisha ya kitajiri huku madeni yakimfukuzia kwa nyuma.
Mambo yalipobadilika ghafla, Kelvin alipata maradhi yaliyomweka kitandani mwaka mzima. Biashara zilikufa, kipato kikakatika, na akaanza kushindwa kulipa marejesho ya mikopo ya yale magari pamoja na kodi ya nyumba.
Wenye magari na makampuni ya mikopo hawakuwa na msamaha, walituma mawakala na madalali wakaja kumpora kila gari lililokuwa nje. Siku iliyofuata, mwenye nyumba naye hakusubiri, alileta madalali wengine na mageti yakafungwa. Siku anatimuliwa, Kelvin alikuwa hawezi hata kusimama, akatolewa na kubebwa kwenye godoro chafu na kuwekwa pembezoni mwa barabara juu ya vumbi.
Siku hiyo ilikuwa msimu wa mvua kubwa. Mke wake alibaki anahangaika katikati ya mvua inayonyesha, akiwa amewakumbatia watoto wao wawili wadogo waliokuwa wanatetemeka kwa baridi na kulia kwa hofu na njaa, huku vitu vyao vyote vya ndani vikilowa maji mbele ya majirani waliokuwa wanawatazama kwa huruma na dharau.
Kelvin akiwa amelala kwenye lile godoro lililoloa maji, alishuhudia binti yake wa miaka mitano akimuuliza kwa sauti ya kilio, "Baba, kwa nini huyu mjomba anatufukuza na mvua inatunyesha? Nyumbani kwetu uko wapi?
Swali lile lilikuwa kama kisu chenye sumu moyoni mwake. Hakuna hata gari moja lililobaki la kumhifadhi yeye au familia yake, wenye nazo walishachukua chuma zao zote. Siku hiyo hiyo, mtoto wake mdogo alipatwa na pneumonia kali kutokana na ile baridi na kufariki dunia siku mbili baadaye hospitali ya serikali.
Baada ya msiba na uchungu ule wa kupoteza mtoto, mke wake hakutaka hata kumtazama tena usoni. Alimwambia waziwazi mbele ya ndugu: "Nilikuwa nakuheshimu ukijiita mwanaume kumbe ulikuwa unaniigizia maisha na kutoa dhabihu maisha ya watoto wangu kwa ajili ya magari ya mikopo na sifa za kijinga, Yule mwanamke alibeba nguo zake na binti yao aliyebaki, akamtema Kelvin akiwa bado amelala mgonjwa kwenye godoro na kuondoka mazima. Mke hakurudi tena, na wala hakutaka hata kujua kama Kelvin anakula au anakufa.
Mademu wote waliokuwa wanapanda naye yale magari ya top-up walitokomea zamani kabisa. Leo hii Kelvin ni mlemavu aliyechoka, hana mke, hana mtoto, hana gari wala nyumba. Yuko kijijini kwao peke yake akisukumwa kwenye kiti cha walemavu na ndugu zake waliomchoka, huku maisha yake yote yakiwa ni majuto na aibu tele.
Wewe mpumbavu unayewaza starehe na kuonyesha watu magari ya top-up na ya mikopo mjini huku huna hata chumba chako mwenyewe, jifunze hapa. Acha useng na ulimbukeni wa kitoto. Nunua kiwanja, pandisha matofali, weka bati juu, jenga kwako mpuuzi wewe ili uwe na ngome ya kuhifadhi familia yako kabla maisha hayajakukanyaga uso na mkeo akakukimbia na kukufanya uoshe macho kwa machozi ya damu.
MWISHO MWEMA