Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,962
6,897
Habari,

Je, kuna mtu hufikia hatua akawa katika hali niliyonayo muda huu? I mean kwamba kuna wakati ukifika nikitafakari maisha yangu nahisi kama kukata tamaa, yaani kuhisi uchovu tu from no where.

Yaani sijui niiweke vipi ila kuna muda tu ukifikaga tafakuri ya maisha hunijia, najikuta nayaangalia maisha yanavyoenda na kuanza kujiuliza kwanini ninaishi na ndipo unagundua vitu vinavyonitoa kwenye mood ya hamasa ya kuishi.

Mungu ananibariki silali njaa, I pay my own bills on time, ila nikirudi katika kutafakari haya maisha tunayoyaishi wanadamu, nikitafakari kuhusu kifo, magonjwa, umasikini, ajali, fake people surronding us because of what we have waki-pretend kama wanatupenda ila tukiishiwa hatuwaoni, ukifanikiwa pia inabidi uwe makini maana maadui wanakuwinda pia nk, yaani ni kama mtu umekuja duniani kwa ajili ya kuteseka tu hadi ufe, basi nikiwaza hayo ndo najikuta napoteza kabisa mood ya kuishi.

I have tried kuiepuka hiyo kitu ila tafakuri hainiachi, nakuwa na furaha ya muda halafu baada ya hapo narudi kwenye tafakuri. Kuna muda tu nitajikuta mwenyewe mahali nikiwa na huzuni na mawazo on why sasa ninaishi si bora tu nisingekuwepo?

Wakati mwingine nikawaza labda kuwa na upweke wa u-single kunafanya niwe hivi na labda pengine nikiwa na mpenzi nitaachana na hii hali lakini sivyo, ni baada ya kuona hata huyo mpenzi anakuja kwangu ikiwa kama kuna kitu cha kumpa na kama sina basi sitomuona tena karibu yangu.

Sasa je, furaha na upendo ya kweli ya maisha ni nini? Basi nikiwaza hayo najikuta tena nikitokwa na mood ya kuishi kabisa.

Nani mwingine hupitia hali hii? Majibu yake ni nini kwako? Tupeane uzoefu ebu.
 
Hii Hali husababishwa na kukosa kazi kuwa free asubuh mpaka jion huna hata pakwenda kupoteza muda,kukosa kampani,kutokua na kipato chochote ILA ZINGATIA HILI ONDOA SHAKA YATAPITA TAFUTA KIBARUA CHA ASUBUH MPAKA JION UKIRUD HOME UMECHOKA HUTOWAZA WALA KUHISI UMECHOKA KUISHI
 
Mean kwamba mtu uwe busy kiasi usiwe na muda wa kujitafakari!!!? are you serious gee?
 
Hii Hali husababishwa na kukosa kazi kuwa free asubuh mpaka jion huna hata pakwenda kupoteza muda,kukosa kampani,kutokua na kipato chochote ILA ZINGATIA HILI ONDOA SHAKA YATAPITA TAFUTA KIBARUA CHA ASUBUH MPAKA JION UKIRUD HOME UMECHOKA HUTOWAZA WALA KUHISI UMECHOKA KUISHI
Hii ni sawa na kujipombesha, ikikutoka bado changamoto iko pale pale.
 
Hii ni changamoto ya maisha yetu, unaowaona wanakusonga si hao tu, vipi na makampuni yanayohakikisha pesa yako inakwenda kwao?

Serikali je, inayotaka mgawane mapato, wakati mwingine hata kabla hujapata hicho kipato, inakulazimisha uilipe, tena kwa makisio yao wala si uhalisi.

Ndio maisha yetu, uamuzi ni wako, ukae pweke, usijishughulishe ili wengine wasidoee, au fanya kazi, ishi na watu kwa machale, ukibarikiwa upate mwenza asiyekunyonya n.k. mengine ujisajaulishe tu kama hayatokei vile. Kila la kheri, na maisha mema!
 
Mental I'll sio lazima ujiue au uwe na ichiz Fulani. Mkuu una mood disorder, Yani unapitia furaha na huzuni za vipindi. Ukiwa na furaha kupita kiasi unaweza kumsaidia hata adui yako hela ya kula au kugawa mshahara wote.

Inafika kipindi unahuzunika tu from nowhere Tena bila rational thoughts. Unaweza kukumbuka tu demu wako hujamkuta bikira so watu walikuwahi ukaamnza kulimwaga chozi.

Inbox me nikushauri
 
hata mm huwa inanitokea! ila nimeshapata kujua sababu ya hii hali kwa upande wangu ko nimekubaliana na hali napambana na hali yangu coz no one cares watu wako busy na mambo yao hata familia unayoitegemea can't help! ushauri wangu kuwa busy jaribu kufanya vile vitu unapenda na vinakufurahisha hasa pale unapokuwa free ama unapojihisi upweke inaweza ikasaidia.
 
Mental I'll sio lazima ujiue au uwe na ichiz Fulani. Mkuu una mood disorder, Yani unapitia furaha na huzuni za vipindi. Ukiwa na furaha kupita kiasi unaweza kumsaidia hata adui yako hela ya kula au kugawa mshahara wote.

Inafika kipindi unahuzunika tu from nowhere Tena bila rational thoughts. Unaweza kukumbuka tu demu wako hujamkuta bikira so watu walikuwahi ukaamnza kulimwaga chozi.

Inbox me nikushauri
Advice?
 
Habari,

Je, kuna mtu hufikia hatua akawa katika hali niliyonayo muda huu? I mean kwamba kuna wakati ukifika nikitafakari maisha yangu nahisi kama kukata tamaa, yaani kuhisi uchovu tu from no where.

Yaani sijui niiweke vipi ila kuna muda tu ukifikaga tafakuri ya maisha hunijia, najikuta nayaangalia maisha yanavyoenda na kuanza kujiuliza kwanini ninaishi na ndipo unagundua vitu vinavyonitoa kwenye mood ya hamasa ya kuishi.

Mungu ananibariki silali njaa, I pay my own bills on time, ila nikirudi katika kutafakari haya maisha tunayoyaishi wanadamu, nikitafakari kuhusu kifo, magonjwa, umasikini, ajali, fake people surronding us because of what we have waki-pretend kama wanatupenda ila tukiishiwa hatuwaoni, ukifanikiwa pia inabidi uwe makini maana maadui wanakuwinda pia nk, yaani ni kama mtu umekuja duniani kwa ajili ya kuteseka tu hadi ufe, basi nikiwaza hayo ndo najikuta napoteza kabisa mood ya kuishi.

I have tried kuiepuka hiyo kitu ila tafakuri hainiachi, nakuwa na furaha ya muda halafu baada ya hapo narudi kwenye tafakuri. Kuna muda tu nitajikuta mwenyewe mahali nikiwa na huzuni na mawazo on why sasa ninaishi si bora tu nisingekuwepo?

Wakati mwingine nikawaza labda kuwa na upweke wa u-single kunafanya niwe hivi na labda pengine nikiwa na mpenzi nitaachana na hii hali lakini sivyo, ni baada ya kuona hata huyo mpenzi anakuja kwangu ikiwa kama kuna kitu cha kumpa na kama sina basi sitomuona tena karibu yangu.

Sasa je, furaha na upendo ya kweli ya maisha ni nini? Basi nikiwaza hayo najikuta tena nikitokwa na mood ya kuishi kabisa.

Nani mwingine hupitia hali hii? Majibu yake ni nini kwako? Tupeane uzoefu ebu.
wee ishi kama kuku,kuku anamuona mwenzake anachinjwa lakini anenda kula vipande nvya nyama vilivobaki pamoja na damu iliyoganda,ata sisi binadamu,tunaenda kuzika lakini tunaendelea kuishi kwa mtumaini!!
 
Back
Top Bottom