Tafuta pesa ila usisahau kuishi

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,659
4,867
Tunatafuta pesa kila siku, tunazitafuta sana, wakati mwingine mpaka unajionea huruma, huwezi kupumzika kwa kuwa unahisi ukifanya hivyo unaweza kuloose sehemu fulani. Ndugu yangu, tuendelee kutafuta pesa ila tusisahu kuishi.

Kuishi ni jambo jema sana, ninaposema kuishi ni kama kuupoza mwili, kuupa pole kwa mihangaiko ya wiki nzima, hata kama unakuwa bize kiasi gani, bado unatakiwa kuishi.

Mwingine anasema mi’ natafuta pesa halafu naanzaje kula kuku? Natafuta pesa kwa shida naanzaje kwenda klabu? Natafuta pesa kwa shida, naanzaje kununua nguo ya shilingi elfu hamsini? Ndugu yangu, tafuta pesa, fanya kila kitu ila usisahau kuishi.

Mabilionea wenyewe wanaishi. Wanatafuta pesa mwezi mzima halafu baadaye utasikia yupo Dubai kaenda kuishi. Wewe kwa nini hutaki kuishi?

Unatafuta pesa sana ila kuishi ni muhimu. Jipe nafasi ya kukaa na familia kila wikiendi, usijifanye kuwa bize mpaka familia unaisahau.

Mimi nakuwaga bize, tena bize sana mpaka najionea huruma lakini kuna muda ukifika, naamua tu nikae na mama, tupige mastori weee, tule vizuri, tufurahi, ndiyo maana ya kuishi.

Hakuna pesa utakayoipata utaridhika. Elon Musk ni bilionea lakini mpaka leo bado anatafuta pesa, vipi kuhusu wewe? Hutoridhika na pesa, sasa kwa kuwa ni hivyo, usisahau kuishi rafiki yangu.

Maisha hayana garantii bro! Unaweza kutafuta sana pesa, ukasahau kuishi halafu ukafa. Unaacha pesa benki, ndugu wanazichukua na kwenda kuishi kama ambavyo wewe hukutaka.

Wengine hatutaki kuishi kwa kuwa tunahisi baada ya kupata kiasi fulani sasa itatosha, pesa haitoshi mshikaji wangu. Ukiipata lazima utaitaka nyingine tena.

Uchoshe mwili kutafuta pesa ila pata muda wa kuishi. Nenda out, nunua chakula kizuri, kula. Kama mfuko unaruhusu waite washikaji, kodisha yacht, nunua pombe, weka muziki, enjoy life.

Maisha ni haya haya, usipoinjoi muda huu utainjoi lini? Kuna watu ni mabilionea, hawakupata nafasi ya kuishi, sasa hivi wapo hospitalini wanateseka tu, hawawezi kula, kutembea wala kufanya lolote lile.

Tuendelee kutafuta pesa ila tusisahau kuishi.
 
Tafuta kibunda
Tengeneza malengo
Weka akiba
Saidia masikini/yatima
Toa sadaka
Alafuuuuuuu
Kula zizuri
Vaa vizuri
Kula pisi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom