Naweza vipi kuishi Pasina kuyatilia sana Maanani haya Maisha?

FORTUNE JR

Member
Mar 20, 2021
69
336
Ivi Umewahi kufikiria hili?

Katika miaka mia ijayo, mwaka 2124, sisi sote hatutakawapo hata jamaa na marafiki zetu pia.

Watu wasiojulikana wataishi katika nyumba zetu ambazo tumejenga kwa jitihada kubwa na kwa Majaribu mengi. Watakuwa na vitu vyote tulivyo navyo au Vingine kuvitupa majalalani.

Hata gari, ambalo tumetumia Gharama kubwa, litakuwa mahala fulani kwenye dampo.

Wazawa wetu hawatatukumbuka sisi, na wachache pekee watajua kama tulikwepo.

Ni nani kati yetu anayemjua baba wa Babu wa babu yake?
main-qimg-f3500dfb5a64add26862b455c620254e.jpeg.jpg


Baada ya kifo, watatukumbuka kwa miaka michache zaidi, kisha picha zetu zitahifadhiwa kwenye shelf za kabati za Vitabu.

Miaka michache baadaye, picha zetu na matendo zitasahaulika. Hatutakuwa tena katika kumbukumbu za yeyote.

Kama siku moja ungekaa kufikiria hili , unaweza kuelewa jinsi isivyokuwa na maana kutembea na kuhangaika kwa muda mrefu kwa nguvu kubwa .

Tukifikiri na kuelewa kuwa sisi ni kidoti tu katika historia ya binadamu, Tutaiacha dunia au ulimwengu kama ulivyo , Tutaishi Maisha yetu kwa jinsi ya utofauti zaidi

HUWENDA BADO MNA MASWALI MENGI KWANINI NAANDIKA HAYA

Wakuu ni kwamba leo imenichukua takribani siku nzima ndani ya chumba changu kukaa pasina kutoka nje na pasina kula, nikiwaza na kujaribu kutafuta hasa maana na dhima kuu ya haya maisha Yangu.

Ni hivi wadau, Binafsi nimetokea kwenye Familia yenye maisha Duni kidogo, na kwa kiasi hakuna Yeyote ndani ya Familia au koo kwa ujumla , ambae naweza kujivunia kapiga hatua tofauti ya kimaendeleo.

Binafsi ni wa kwanza kuzaliwa katika familia yangu, Na kipekee nimebahatika kusoma kwa Shida sana,

Wazazi wangu wamepambana sana, Mama yangu kwa kuuza Vitumbua na Maandazi na pia akishilikiana na Baba yangu kwenye kilimo cha Jembe la mkono.

Nachoweza kusema Wazazi waliwekeza kwangu, wakiamini mimi kama mzawa wa kwanza nitafanya kitu na kwa wadogo zangu.

Mara kadhaa nilikua nikisikia Mama akisema "Unajua Babako jana usiku kucha hajalala alikua amekaa tu kitandani akifikiri kwa jinsi gani atakulipia ada ya shule "

Au mara nyingine pia utasikia Mama akisema Unajua siku fulani tulivyokutumia ile hela ya matumizi , tulibaki mikono mitupu kabisa pasina chochote na wadogo zako, na Mara nyingine pia walikosa hata chakula

Na nukuu maneno ya mama
"Mwanangu najua sipaswi kusema haya yote kwako na Baba yako pia hapendi nizungumze haya yote kwako, ila Ukumbuke mwanangu Maisha yetu na ya wadogo zako, yako kwenye misingi yako, Katika kila unalolifanya Kumbuka tuko nyuma yako Mwanangu, kwa Gharama yoyote utasoma.

Hujawahi kutuona mimi au Babako tukienda Kulewa pombe au starehe zozote. Mawazo yetu yote ni kwako mwanangu. Mchana na Kila ifikapo usiku tunakuombea Mwanangu na wewe jiombee daima,

Kuanguka ni sehemu ya maisha ila Chunga usijidondoshe mwenyewe tupo nyuma yako mwanangu"

Haya maneno ya Mama siku zote hayaachi kujiludia kwenye fikra zangu na mara zote yakinijia najihisi machozi .

Kwakua ni dhahiri niliona Juhudi za wazazi wangu. Asubuhi hadi jioni Shambani, Mvua na jua vyao.

Nimefanikiwa kumaliza chuo miaka takribani kadhaa iliyopita, bado sijaajiliwa licha ya kutembeza bahasha isivyokua kawaida,

Kwenye makundi ya Whatsapp nashuhudia shuhuda za wenzangu niliosoma nao jinsi wakielezea walivyopata kazi kwenye kampuni fulani au serikalini, lakini mimi milango bado ni migumu.

nimeenda nje ya boksi pia kwa kuweka kisomo changu pembeni na kuingia shambani na kuzamia huko vilivyo na kwa nguvu zote, lakini shughuli bado ni tete na mtaji ni issue nyingine pasua kichwa.

Toka nikiwa mdogo nimeona na nimefunzwa na Wazazi, katika kila ninalolifanya, na katika kila nyakati yani shida, raha , Njaa au Shibe MUNGU kwanza(nisiache kuomba)
Lakini bado maombi yangu hayazai matunda. Kadili mda uendavyo najiona kukosa nguvu ya kuomba tena😢


Wazazi nawaona wakizidi kuchoka na kuzeeka ilihali bado ile ndoto yao bado sijaitimiza.

Kwakweli natumia mda mwingi kuwaza hasa majira ya usiku pasina kupata usingizi hali ambayo sasa inanipelekea kupata maradhi ya presha na Vidonda vya Tumbo.

Hii hali ndio iliyopelekea leo nijifungie ndani na kutathimini Nilipotoka na mwafaka mzima wa maisha yangu.

Ni ivi wadau naenda kuhitimisha ;

Kama nilivyotangulia awali kwa hoja ya jinsi nilivyong'amua mzunguko wa mwanadamu ni mfupi sana na hupita kama upepo,

Sasa kuna maana gani kuwa na mfululizo wa nyakati za majonzi, Huzuni na misongo ya mawazo ambayo ni chanzo cha maradhi kwangu ilihali nafukuzia upepo na maisha haya ni mpito na mwisho kila kitu na kila historia itaenda kufutika na kusahaulika kabisa

Ni hivi;
Kwa huu mda sasa nitafurahia matembezi ambayo kamwe sikupata muda kabla.

Na haswa nataka nitumie nyakati hizi zinazohesabika na ambazo hazikawii kuisha, kwa kuwa karibu na kujenga upendo mkubwa na familia yangu,

Kwa kushikana mikono ya faraja, kufurahia hizi nyakati bora na nzuri ambazo zitajenga kumbukumbu na kuchora alama ndani yetu kwa kina.
( Those would certainly be the most beautiful and best moments to remember and imprinted deep within ourselves. )

Mapambano ya utafutaji yataendelea( With no regrets). Nitakalopata nitashukuru, nitakalopoteza nitaliacha liende pasina majuto, na nitalokosa sitaki liniumizi (no much expectation)

HUU MDA NITATUMIA KUISHI NA KU ENJOY HIZI NYAKATI FUPI NILIZONAZO NA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI WAKATI WA MUNGU UKIFIKA NITAUPOKEA. Hii dunia sio yetu, tumejiegesha tu .😒
 
Remember, IT'S ALL RISKY
Everything is risky, your life itself is risky. The moment you were born it got more risky so stop blaming, your life is 100% your responsibility just find your purpose

To find your purpose in life just ask yourself two valuable questions;
What struggle do you choose in your life
What pain are you willing to go through in your life

Jiulize na ujijibu, life's to short to be unhappy
 
Remember, IT'S ALL RISKY
Everything is risky, your life itself is risky. The moment you were born it got more risky so stop blaming, your life is 100% your responsibility just find your purpose

To find your purpose in life just ask yourself two valuable questions;
What struggle do you choose in your life
What pain are you willing to go through in your life

Jiulize na ujijibu, life's to short to be unhappy
What are massage 🙌
 
Ushauri wangu wa kwanza kabisa kwako na kwa watu wa aina yako ni huu " sahau kabisa hayo maneno ya mama ako , ni sumu mbaya sana hiyo itakuua. Dingi ako anajua hilo ndio maana hajawa akipenda mama ako aongee na wewe vitu hivyo. Pambana kwakua unapaswa kuyajenga maisha yako binafsi. Mengine yatafuata.

my personal belief system always inaniambia kwamba "msaada wa kwanza mkubwa unaoweza na unaopswa kuwapa wazaz wako ni WEWE KUWEZA KUJIMUDU MAISHA YAKO MWENYEWE KWANZA.. wazaz wako walikusomesha uwe (wewe) na maisha bora. Trust me wao hata wakifa na hali hiyo they will not regret but wakifa hali wakijua bado ninyi (wewe) hamna uwezo wa kuyamudu maisha yenu bado, amini kabisa watakufa vifo vya majuto makubwaa sana kana kwamba misheni yao hapa dunian wanaondoka wakiwa wamshindwa kuifanikisha.

FAnya kujitafuta wewe kama wewe... by the way utaweza vipi kuyamudu maisha ya wengine kama yako tu huwez ku deal nayo..

Potea kabisaa go find your life...
 
Atleast umegundua hayo mapema, hata upambane vipi mwisho wa siku ni kujilisha UPEPO! Yote ni UBATILI mtupu, usijipe hata sekunde moja ya kujuta, ishi maisha yako!
 
Dunia nzima ingewaza kama weww hata simu unayotumia isingegundulika,tafuta hela acha kujipamoyo
 
Ishi kama utakufa kesho, hii itakufanya uishi kwa hofu ya MUNGU na utafanya ibada zaidi. Pia ishi kama hautakufa hii itakufanya ufanye bidii kujijenga kiuchumi zaidi.
Kumbuka kusambaza furaha ndani ya familia yako na jamii iliyo karibu nawe, usisahau kujipa furaha mwenyewe.
 
Ushauri wangu wa kwanza kabisa kwako na kwa watu wa aina yako ni huu " sahau kabisa hayo maneno ya mama ako , ni sumu mbaya sana hiyo itakuua. Dingi ako anajua hilo ndio maana hajawa akipenda mama ako aongee na wewe vitu hivyo. Pambana kwakua unapaswa kuyajenga maisha yako binafsi. Mengine yatafuata.

my personal belief system always inaniambia kwamba "msaada wa kwanza mkubwa unaoweza na unaopswa kuwapa wazaz wako ni WEWE KUWEZA KUJIMUDU MAISHA YAKO MWENYEWE KWANZA.. wazaz wako walikusomesha uwe (wewe) na maisha bora. Trust me wao hata wakifa na hali hiyo they will not regret but wakifa hali wakijua bado ninyi (wewe) hamna uwezo wa kuyamudu maisha yenu bado, amini kabisa watakufa vifo vya majuto makubwaa sana kana kwamba misheni yao hapa dunian wanaondoka wakiwa wamshindwa kuifanikisha.

FAnya kujitafuta wewe kama wewe... by the way utaweza vipi kuyamudu maisha ya wengine kama yako tu huwez ku deal nayo..

Potea kabisaa go find your life...
Asante sana mkuu, kwa ushauri murua na time yako.
 
Back
Top Bottom