Kuishi na mwanaume mlevi ni mzigo

Kuishi na mwanaume mlevi ni mzigo

Sipendi pombe na namuomba Mungu aniepushie mnywaji wa pombe

Bila shaka unajua mahali pa kumpata mume wa aina hiyo. Nakuombea kila la heri.

Baba yangu alikuwa analewa hadi anaanguka na nikajiapiza sitakunywa pombe. Namshukuru Mungu hata kuonja siionji.
 
Ukitaka asiyekunywa, zaa wako umlee kwny mazingira mazuri akuoe akikua. Unajua nini kama mwanaume hanywi pombe kabisa inawezekana, ila lazima ana ulevi wake sasa usiombe ukute ulevi wake ni mkali kuliko ulevi wa pombe, utajuta
mkuu unaelewa ulichokiandika?..mbona unajichanganya
 
Kwa lafudhi yake unahisi anatokea mkoa gani? maana kuna sehemu inaitw Rombo inatoa kizazi cha walevi

Aliyekudanganya nani me ni mrombo hata harufu ya pombe siijui na walevi sio lazima atoke huku mwezi kama mmoja umepita hivi mkaka wa kipogolo aligongwa pale mtaa ya mwenge kwenye mataa kisa alikuwa kalewa chakari alikiuka sheria za mataa na kutaka kupita kwa ubabe akakutana na lori na kuumia vibaya mpaka kupelekea kulazwa wiki mbili hospitali nae utasema ni mchaga
 
Akili ndogo zimesheheni kwenye hii thread, uchumi wa Taifa unaendeshwa na walevi halafu mwasemaje?

Reginald Mengi anakunywa pombe, nionesheni mwanamke gani humu atamkataa? Tuache unafki.

Mkapa anakunywa pombe, Kikwete anakunywa pombe, Lowasa anakunywa pombe, Magufuri licha ya kunywa amenogea mpaka ameadopt na jina kabisa pombe,

Nitarudi nawahi somewhere kidogo.

Kuna tofauti katika unywaji. Mtu hadi akiitwa mlevi ina maana anakunywa kupitiliza,hao uliowataja wanakunywa kistaarabu ambacho sio kitu kibaya.
 
Umetugusa walevi...... Mtu akikutukana kwa kisingizio cha kulewa ni uongo, pombe haiwezi kukufanya uwe na matusi wakat hulka yako haikuwa ya kutukana,

pombe huendeleza kile ulichokuwa nacho,,,,
miss chagga naomba uje uthibitishe hapa
kwa kweli wanasingizia pombe jamaa hamtaki tu na wala si pombe.... pombe anatumia kama njia ya kufikishia ujumbe tu.... pombe ni pombe... matusi ni jianaume limelelewa hivyo hajui thamani ya mwanamke...

ingekuwa ni pombe nadhani kila mtaa kungekuwa matusi tu watu wanakula maji na midomo yao imejaa hekima..
 
Kweli kabisa my mwanaume mlevi anakera kupitiliza
 
Mimi sitaacha pombe,maana haijawahi kunikosea.Mimi hunywa ijumaa jioni na jumamosi tu.

Jumapili hupumzika na familia baada ya kutoka kanisani. Ninywapo hujisikia raha sana. Sigombani,situkani. Bali huchekesha sana wenzangu.

Maendeleo nyumbani naleta.nasomesha watoto vizuri,kazini najituma,hata kitandani pia.

Kwa kweli nikiacha pombe,nahisi maisha yangu yatabadilika sana.Nitakuwa na stress za kufa mtu.

Sasa hivi yenyewe nimetoka kunywa Shots za Jack Daniels...Pombe sikuachi labda uniache wewe mpenzi.Amina

Tupo pamoja mkuu, pombe nakupenda pombe nipende!
 
We ndo hujaelewa, kuna neno lisiloeleweka hapo
ok labda unisaidie kuelewa...so watu wasiokunywa kabisa(ambao mwenyewe umekiri kuwa wapo),walizaliwa na kulelewa katika mazingira mazuri zen wakaja kuwaoa mama zao??...na nani aliyekwambia kuwa watu wanaokunywa hawajalelewa kwenye mazingira mazuri??
 
Wasiokunywa pombe wanakosa mengi, pombe ina raha....
Jack daniel + amarula
zanzi + konyagi is equal to fire kwa bed

Asiyejuwa maana haambiwi maana wacha waishi kwa kukariri tu, waelewa tutaendelea kuenziwa kwa mahaba mazito na tunasimamia show vile ipasavyo.

Tuna mouth wash za kuondoa harufu midomoni sidhani kama namkera wifi yako na uzuri akipita super market huwa hasahau kuninunulia hii colabo ya Jack Daniel's na Amarura.

Janaume zima saa kumi na mbili kila siku liko nyumbani kama si uzezeta ni nini?

Yakifukuzwa kazi huwa yanatia huruma na kujiingiza kwenye ulokolre kwa sababu hayana connection ni anti social.

Wanaume tuna vikao vyetu vya kupeana michongo na kushauriana.
 
Bila shaka unajua mahali pa kumpata mume wa aina hiyo. Nakuombea kila la heri.

Baba yangu alikuwa analewa hadi anaanguka na nikajiapiza sitakunywa pombe. Namshukuru Mungu hata kuonja siionji.

Mizimu haipendi unapoapa kutokunywa pombe, kunywa ili mizimu ifurahi, baba yako alikua anakunywa ww hutaki? ndio maana tumeacha kuiabudu mizimu ya babu zetu ktk makaburi yao tumeanzisha makanisa ambayo tunaemuabudu hayupo
 
Back
Top Bottom