Nalileta hili ili wanaume mjitathimini.
Nilikuwa sehemu fulani kijijini mkoa wa pwani, wakati narudi jioni hii njiani alipanda baba mmoja alikuwa kanywa pombe ila siamini kama kalewa, ambae kwa maelezo yake anakaa sinza, wakati tumeenda umbali mrefu karibu masaa mawili ghafla simu yake ikaita, akapokea ile simu neno aliloanza nalo ni "kwa nini muda wote hujanitafuta?? unanitafuta saa hizi wakati jua linaaga, mngese .............. sana wewe mwanamke, nimekuwekea charge hadi kwenye.........................(papuchi) yaani yakamtoka matusi yote then akakata sim, yaani gari zima turiboreka hakuna hata aliyemsemesha, kaona hiyo haitoshi kaanza kumsema mkewe madhaifu yake yote ndani ya gari, yaani anatoa maneno mazito mazito, kwa kweli wanawake wote tulinywea kama tumemwagiwa maji, baada ya hapo dada mmoja aakamwambia baba kwanini unashindwa kumsitiri mwanamke unaeishi nae??????? ndio kama aliwasha moto, mzee akasema yoteeeee yaliyomo na yasiyokuwemo loh!!, jamani mzee alizaliwa 1942 lakini, maneno aliyokuwa anatukana mmmh!!!!!!!! kweli nikaamini mwanaume mlevi ni mzigo, haraka nikamtathimini nikagundua:
- kwanza ni mwanaume mchafu mchafu hadi basi.
- Ni aina ya wanaume wanyanyasaji ambao anaweza kumsimanga mwanamke hata kwa chakula.
- wababa wa aina hii ndio chanzo cha wanaume kuwa wa sasa kurithi unyanyasaji.