Kuishi na mwanaume mlevi ni mzigo

Kuishi na mwanaume mlevi ni mzigo

Apologise lady

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2013
Posts
5,980
Reaction score
3,115
Nalileta hili ili wanaume mjitathimini.

Nilikuwa sehemu fulani kijijini mkoa wa pwani, wakati narudi jioni hii njiani alipanda baba mmoja alikuwa kanywa pombe ila siamini kama kalewa, ambae kwa maelezo yake anakaa sinza, wakati tumeenda umbali mrefu karibu masaa mawili ghafla simu yake ikaita, akapokea ile simu neno aliloanza nalo ni "kwa nini muda wote hujanitafuta?

Unanitafuta saa hizi wakati jua linaaga, mwanamke, nimekuwekea charge hadi kwenye (papuchi) yaani yakamtoka matusi yote then akakata simu, yaani gari zima turiboreka hakuna hata aliyemsemesha, kaona hiyo haitoshi kaanza kumsema mkewe madhaifu yake yote ndani ya gari, yaani anatoa maneno mazito mazito.

Kwa kweli wanawake wote tulinywea kama tumemwagiwa maji, baada ya hapo dada mmoja aakamwambia baba kwanini unashindwa kumsitiri mwanamke unaeishi nae? Ndio kama aliwasha moto, mzee akasema yote yaliyomo na yasiyokuwemo loh!, jamani mzee alizaliwa 1942 lakini, maneno aliyokuwa anatukana mmmh! Kweli nikaamini mwanaume mlevi ni mzigo, haraka nikamtathimini nikagundua;


  • Kwanza ni mwanaume mchafu mchafu hadi basi.
  • Ni aina ya wanaume wanyanyasaji ambao anaweza kumsimanga mwanamke hata kwa chakula.
  • Wababa wa aina hii ndio chanzo cha wanaume kuwa wa sasa kurithi unyanyasaji.
 
Nauchukia sana ulevi maana nikikumbuka ulivyomtesa baba kwa kuwa mama ndiye aliyekuwa mlevi napatwa na hasira niwaonapo walevi
 
Mimi sijawahi tumia na siwezi kuwa na urafiki na mlevi, kuoa mlevi ndo kabisaaa haitatokea hata kama tumebaki wawili duniani bora nioe sabuni
 
Apologise lady

Nitaamini utakaponiambia ulijuaje kazaliwa mwaka 1942.....

Baaaas....
 
Last edited by a moderator:
Mimi sijawahi tumia na siwezi kuwa na urafiki na mlevi, kuoa mlevi ndo kabisaaa haitatokea hata kama tumebaki wawili duniani bora nioe sabuni

Mlevi ni mzigo kuanzia kwenye bar anayokunywa mpaka kwa taifa ila kijana umuombe mungu wako sana. Mimi Mungu wangu alishasema anayedhani amesimama na aangalie asianguke. Usijitape sana shetani asije akakushangaza. Kama umepata neema ya kuchukia pombe basi shukuru na uwaombee walevi wapone.
 
Mimi sijawahi tumia na siwezi kuwa na urafiki na mlevi, kuoa mlevi ndo kabisaaa haitatokea hata kama tumebaki wawili duniani bora nioe sabuni

Heee....makubwa bora uoe sabuni?? sabuni itazaa watoto?
 
Kweli nikaamini mwanaume mlevi ni mzigo

Sio peke yako,tuliokuwemo ndani ya gari ile walifurahia kile kitendo.Hata na mm hakunifurahisha nilitamani nimwambie dereva amshushe ila nilimuheshimu umri wake.

Nilichogundua.
Mzee ana stress sana za maisha.
Inawezekana keshakatamaa na maisha.
 
mlevi ni mzigo kuanzia kwenye bar anayokunywa mpaka kwa taifa ila kijana umuombe mungu wako sana. Mimi Mungu wangu alishasema anayedhani amesimama na aangalie asianguke. Usijitape sana shetani asije akakushangaza. Kama umepata neema ya kuchukia pombe basi shukuru na uwaombee walevi wapone.

Mkuu nilipokuwa 17 ningeweza vuta na kunywa sababu ya ujana, sasa hivi ni mzeee najielewa naanzaje anzaje onja kitu uzeeni?
Sina rafiki mlevi, siendi Bar, sijihusishi na mambo ya usiku eti nitakunywa bia, siendi club wala harusi yenye bia....
Am at a safe zone

Heee....makubwa bora uoe sabuni?? sabuni itazaa watoto?

Tuko wawili tu duniani mtoto wa kazi gani?
 
Namshukuru MUUMBA kilevi wala sigara ndogo wala kubwa havijaingia kwenye kinywa changu .

Kama unavuta na mlevi ntakaa na wewe mbali maili 1000 maana sihitaji hata kunusa harafu za hayo makitu hahahahah.

" Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako...kwa Maelezo zaidi endelea kuvuta"
 
Back
Top Bottom