Kuiper Belt: Behind the certain

Zimbabwe huko walitua kwenye shule moja ya chekechea na wale watoto walisimulia hii kitu.Nilishawahi kuona documentary ya hili tukio siku za nyuma sana na nitaisaka hii kitu.....

Mkuu kwani unafahamu NWO ni kitu gani?
Kama una jina la hiyo documentary naomba unitajie tafadhali,
 
KUIPER BELT

Kadiri tunavyoendelea kuwepo kwenye dunia hii tunaendelea kupata kujua mengi sana kuhusiana na mazingira yetu na yale yote ambayo yanatuzunguka.Ukiacha maswali mengi ambayo binadamu ameshindwa kupata majibu yake bado binadamu huyu ameendelea kupata kujua mengi tu ambayo yanashangaza na kustaajabisha vya kutosha..

Siyo wengi ambao tumeshasikia kuhusiana na kitu kinachoitwa Kuiper Belt.Leo nitaielezea kwa kiasi ambacho nimepata kujua kuhuihusu na nitasema ni kwanini nimeamua kuzungumzia kuhusu Kuiper Belt....

Kuiper Belt ni nini?

Kuiper Belt belt ambao pia hufahamika kama Edgeworth–Kuiper belt ni mkusanyiko wa "vitu"mfano wa mawe ambavyo vimejikusanya kwenye eneo ambalo linaishia eneo la jua letu au kwa kimombo solar system yetu unapoishia mzunguko [Orbit] wa Neptune.Vitu hivi ambavyo ni kama vijimawe vidogo vidogo ambavyo inadhaniwa ni vya barafu vimeizunguka solar system yetu na kufanya kitu kama mkanda hivi ambao umezunguka eneo lote hilo.

Zingatia....

Kwenye mada hii nimeamua kutumia neno la kiswahili "vitu: kwakuwa nimeona ndiyo tafsiri inayoendana vyema na neno la Kiingereza object hivyo popote ninapoandika neno "vitu" basi ifahamike natumia kwa muktadha huo...

Tuendelee....

Kabla ya kugunduliwa kwa mkanda huu kuliwahi kuwepo kwa nadharia nyingi kuhusiana na kuwepo kwa kitu kama hiki kabla ya kuja kugunduliwa.Kilichopelekea kugunduliwa kwa mkanda huu wa hivi vimawe vidogo vidogo na mawe makubwa nje kidogo ya mzunguko wa sayari ya Neptune kulianzia baada ya ugunduzi wa sayari ya Pluto uliofanywa na Tombaugh.Baada ya ugunduzi huo wataalam wa anga walianza kufikiria kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mazingira ya kuwezekana kuwepo kwa vitu [object] nje ya mzunguko wa sayari ya Neptune nje kidogo ya eneo la jua tunalolitumia linapoishia na mtu wa kwanza kutoa ushauri wa kuwezekana kuwepo kwa kitu hiki ni Freckrick C. Leonard....

Mwaka huo huo mtaalam wa masuala ya anga aitwaye Armin O. Leuschner alisema kwamba inawezekana kwamba Pluto ni miongoni mwa mlundikano wa sayari ambazo bado hazijagunduliwa.....

Baada ya miaka mitano ya utafiti hatimaye August 30 1992,Jewitt na Luu walitangaza ugunduzi wa vitu vilivyodhaniwa kuunda Kuiper Belt,jisomee hapa; Discovery of the candidate Kuiper belt object 1992 QB1 ......

Mwaka 1988 katika chapisho lao Tremaine na wenzake walisema kuwa nadharia ya kuwepo kwa vitu vilivyozunguka nje ya mzunguko wa sayari ya Neptune kuwa ni "Kuper Belt" na baadaye hilo ndilo likaja kuwa jina lililotumika kutaja vitu hivyo au ndilo likawa ndilo jina rasmi la kutambulisha mkanda huo baada ya ugunduzi rasmi japokuwa baadhi ya wataalamu wa anga hutumia jina la Edgeworth-Kuiper belt maalum kwaajili ya kumpa stahiki ya kazi ya Edgeworth ya kuanzisha dhana ya kuwepo kwa mkanda huo....

Japokuwa kumekuwepo kwa ubishani wa kutosha baina ya wataalamu wa mambo ya kale kuhusiana na jina la mkanda huu wa ajabu na wa kustaajabisha hii siyo lengo la mada hii kwa leo lakini kwa wengi mkanda huu unajulikana kama Kuiper Belt....

Kutokana na kudaiwa kwamba vitu hivyo vinavyotengeneza mkanda huu ni vya barafu au kwa sehem vina barafu basi moja kwa moja inadaiwa kuwa kunawezekana kuna maisha kwenye eneo hili na hii ndiyo iliyonifanya niandike mada hii.....

Kwenye mkanda huu wataalamu wanadai kwamba kuna vitu [object] vya barafu vinavyokadiriwa kuwa vingi sana vinavyotengeneza mkanda huu ambavyo ni kama vimawe vidogo vidogo na mawe makubwa sana yanayoweza kuonekana kama yana rangi nyeupe kwa kutumia vifaa vya kuangalia angani.Inadaiwa kuwa kuna nyota ambazo zina aina ya vimawe ambavyo vinafanana na vile vilivyogunduliwa kwenye mkanda huu na kusababisha dhana nyingi sana kuhusu vimawe vinavyounda mkana huu wa ajabu kabisa...

kuiperbelt.jpg

Kuiper Belt

Pamoja na yote hayo,wataalamu wa anga wanadai kwamba mkanda huu utatoweka kabisa kwenye eneo la jua letu baada ya miaka 100 ijayo na hautakuwepo tena.Jambo la kushangaza kabisa ni kwamba kituo cha utafiti wa anga cha nchini Marekani kijulikanacho kama NASA kimeripoti hivi karibuni kuonekana kwa vitu visivyotambulika vikielea angali jirani na sayari ya Neptune na vitu hivyo vinaelekea kwenye eneo ambalo dunia yetu ipo.Pamoja na taarifa hiyo,imetolewa ripoti nyingine tena ikisema kwamba kumeonekana kwa vitu [object] vikitokea eneo lililopo jua na kuelekea eneo ambalo mkanda wa Kuiper Belt ulipo na inadaiwa kwamba vitu hivyo ni vingi sana...

Watu wamekuwa wakijiuliza sana ni vitu gani hivi na vinatoka wapi na ni kwanini vinaonekana kwa wingi kadiri siku zinavyosonga mbele.Je vitu hivi ni vitu tu kama tunavyodhania au kuna zaidi?

Tuendelee...

Nyuma ya Kuiper Belt kuna kitu kingine kinaitwa Oort Cloud,hii ni aina nyingine ya mkusanyiko mkubwa sana wa vitu vinavyoelea angani vilivyofanya mkusanyiko wa aina yake.Eneo hili liko mbali sana na eneo la jua letu [Our solor system].Vitu vinavyotengeneza mkusanyiko huu vinafanana na vile vinavyotengeneza mkusanyiko wa Kuiper Belt.Maeneo yote mawili yana mambo yanayofanana kwa namna fulani na ndiyo sababu ya kuandika makala hii kwa siku ya leo ili tujaribu kutafakari kuhusu maeneo haya....

Kutokana na tabia na maelezo yanayohusu maeneo haya ni watu wachache sana wanaofahamu kuyahusu,lakini pia kuna maelezo ambayo hayaeleweki sana kuyahusu.Mfano wataalam wa anga wanasema kwamba Kuiper Belt itatoweka baada ya miaka 100 ijayo,hapo hapo tunaelezwa kuwa Kuiper Belt iko pale kwa mabilioni ya miaka,sasa ni kitu gani kinasababisha mkanda huu uondoke baada ya miaka 100 wakati uko pale kwa billions of years? Swali hili halijaweza kujibiwa ipaswavyo na siyo swali hili tu bali na maswali mengine kama vile sababu ya kuonekana kuna uwezekano wa kuwepo kwa uhai kwenye eneo hilo kwasababu vitu kama mawe madogo na makubwa sana yanayounda maeneo yote mawili ya Kuiper Belt na Oort Cloud yanaonekana yana barafu na sote tunajua kuwa barafu ni maji na sehemu yoyote yenye maji basi kuna uhai....

Kama wale wataalamu wa mambo ya Intelligence wanavyoelewa ni kwamba mara nyingi mahali ambapo kunapokuwa na maelezo yasiyoeleweka au yasiyoshiba na mara nyingi kunakuwepo na hali ya kuficha mambo au jambo.Baada ya watu kutokuridhika na maelezo ambayo wamekuwa wakipewa kuhusiana na maeneo haya mawili,kundi la wataalamu wa anga waliamua kufanya utafiti zaidi ili kujua ni kwa nini maelezo yanapwaya..

Baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu walikuja na dhana ambayo iliwastua watu wengi sana na kupelekea kuzusha mjadala mkubwa sana juu ya maeneo hayo na usalama wa binadamu hapa duniani.Wataalam hao walikuja na maelezo kuwa maeneo hayo yote mawili yamekuwa yakitumiwa na viumbe ambao wengi wamekuwa wakiwafahamu kama Aliens na viumbe tofauti na hao.Maelezo haya yalipingwa sana na wanasayansi na wataalam wa anga wa NASA.Pia hata wataalam wengine nao walipinga kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa uwepo wa hawa viumbe huko kwenye haya maeneo haya....

Kabla ya kuendelea sana nadhani wengi wetu tunafahamu kwamba kwenye galaxy yetu tuna nyota zaidi ya bilioni 100,na kuna bilioni zaidi ya 100 ya galaxy kwenye ulimwengu [univarse] wote.Kwa hiyo unaweza kupiga hesabu kuna nyota ngapi kwenye ulimwengu wote.Ni nyingi sana bila shaka.Wataalam hawa wanasema kwamba,ukiacha kwenye maeneo mawili haya ya Kuiper belt na Oort Cloud,wanaamini kwamba kuna maisha pia kwenye nyota zote hizo ambazo idadi yake ni nyingi sana tena ya kutisha na kote huko kuna viumbe na viumbe hao wana uwezo mkubwa sana na mbali sana kuliko binadamu...

Tuachane na maeneo mengine na turudi sasa kwenye Kuiper Belt na Oort Cloud ambako ndiyo mada yetu ya leo na tunajadili kuhusu aina ya viumbe ambavyo wataalam hawa wamesema vinapatikana humo...

Wataalam hawa wamesema kuwa maeneo haya yanakaliwa na Aliens wa aina zaidi ya 104 na hapa nitakueleza aina chache tu.Mtafiti wa masuala ya Aliens Stewat Swardlow,Steve Qyle na wengine wengi wamewahi kushuhudia kwa nyakati tofauti nyaraka za siri kutoka kwenye serikali tofauti tofauti kubwa duniani kama vile Marekani,China,Urusi,Japan,Ujerumani na nyingine zikionesha ukweli wa uwepo wa viumbe hawa.

Zifuatazo ni 4 kuu na kubwa za Aliens wanaopatikana kwenye mkanda wa Kuiper Belt...

1;Insectoid Aliens
2;Grey Aliens
3;Humanoid Aliens
4;Reptoid Aliens

Aina hizi ndizo ambazo serikali nyingi za dunia zimekubaliana na uwepo wake,lakini kwa siri kwasababu ndiyo aina ya Aliens ambayo imewahi kuonekana hapa duniani.Lakini tujue kwamba,kama nilivyosema hapo juu ni kwamba wataalamu hawa wanasema kwamba kwenye mkanda wa Kuiper kuna mamia ya aina za Aliens lakini wanasema kwamba Aliens aina ya Insectoid ndiyo super power huko...

Insectoid wanadaiwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kuweza kuiongoza au kuirrubuni akili ya kiumbe mwingine afikiri kama atakavyo yeye na hii ndiyo imefanya wakawa na nguvu sana eneo hilo ambalo limezua mjadala na vurugu sana baina ya wataalam wengi.Kwa maana hiyo Insectoid ndiyo aina bora zaidi ya Aliens inayopatikana eneo hilo.

Hawa viumbe ni hatari sana kwa maisha ya binadamu na karibia kila kundi la Aliens lina ajenda yake kuhusiana na binadamu na dunia hii.Kama nilivyosema kuwa kuna aina nyingi ya Aliens,hapa nitaeleza makundi machache ya Aliens na ajenda zao dhidi ya dunia na sisi wakaazi wake....

Mantids Aliens

IMG_3107.jpeg
sk-2017_04_article_main_desktop.jpg

Hawa wao wanadai kuwa dunia hii ni yao na waliishi hapa kwa miaka mingi kisha wakaondoka kwenda kutafuta maisha maeneo mengine na sasa wanahitaji kurudi.

Lionestic being Aliens

Hawa wanafanana sana na binadamu lakini pia wanafanana na Simba.Nimekosa picha ya kuonesha namna wanavyoonekana lakini inastaajabisha sana.Hawa lengo lao ni kuondoa mtindo wa kisiasa ulioko hapa duniani.Hawa wao watasubiri hadi tumeshamalizana sana na ndipo watakuja na kuondoa kabisa mtindo huu wa siasa ulioko hapa duniani....

Humanoid Aliens

Alien-Main-654348.jpg
64043.jpg

Hawa ni miongoni mwa Aliens wengi na wenye uwezo mkubwa sana na wa hatari.Inadaiwa kwamba miongoni mwa aina za hawa humanoid Aliens ipo aina ambayo inafanana kabisa na binadamu na unaweza kukaa naye kwenye kiti na usijue kama siyo binadamu.Hawa wanaamini kuwa dunia hii iko chini ya mamlaka yao na ni eneo lao.Wanataka kuisafisha dunia yote na kuhakikisha hakuna binadamu anabakia hapa.Wanaamini wana haki ya kufanya yote na chochote watakacho na ajenda yao kubwa ni kuondoa binadamu kwa kuwamaliza hapa duniani.Kwa mujibu wao ni kwamba binadamu ni jamii isiyokuwa halisi hivyo haistahili kuwepo kwasababu ni hatari kwa jamii hii kuendelea kuwepo.

Kwa ufupi sana hao ndiyo Aliens walioko maeneo hayo na ajenda yao kutuhusu kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbali mbali.Lakini kuna jambo lingine kutoka Japan...

Princess Kaoru Nakamaru

Princess-Kaoru-Nakamaru-2009-mep0f0q757in0dos2z36rtxlodmhgj8vodn3qxsa48.jpg

Princess Kaoru Nakamaru kushoto akiwa na Miriam Delicado walipokutana mwaka 2009 kwa mahojiano...

Huyu ni binti kutoka familia ya kifalme ya Japan ambaye aliwahi kusema kwamba amewahi kusafiri sana maeneo mbali mbali huko angani akiwa na Aliens.Miongoni mwa mambo ambayo amesema kwamba anatamani sana kuyasema ni ukweli kuhusu historia ya kweli ya Japan ambayo anasema inakwenda hadi kwenye Israel ya kale.miongoni mwa taarifa za kustua sana ni kwamba baadhi ya maelezo yanaonesha kwamba Aliens ni wa kuwa nao makini sana maana wakati mwingine wanaweza kutumia binadamu kama chakula....

Aliens hawasemi kwa kutamka kama sisi bali wao huwasiliana kwa kusoma mawazo yako na ya Aliens wenzao tu.Wana uwezo mkubwa sana wa kufanya hivyo hivyo hawahitaji sauti ili waweze kuelewa unataka kufanya nini dhidi yao au katika mazingira uliyopo.

Huyo ndiye Princess Kaoru Nakamaru...

Je,yote hii maana yake ni nini?

Ninatambua uwepo wa watu wenye msimamo kuwa masuala mazina ya Aliens ni hadithi za kufikirika na ni upuuzi tu.Ninafahamu pia wale ambao wana misimamo kuwa Aliens wapo lakini kila mmoja ana msimamo wake kulingana na kiwango cha taarifa alicho nacho,hivyo wapo ambao wanaufahamu mkubwa sana,wengine kiasi na wengine mdogo...

Yote hayo yanakuja kutokana na aina ya maisha tuliyonayo.Kimsingi kila mmoja wetu ana haki ya kufikiri na kukubaliana vyote ambavyo anaamua kukubaliana nayo lakini ukweli na uhalisia unaweza kuwa kinyume kabisa na namna ambayo sisi au mimi nimeamua kukubali.Unaweza kudhani kuwa uwepo wa Aliens ni upuuzi na ujinga kwasababu ni hadithi lakini hilo halitaweza kuondoa ukweli kuwa wapo,kama kweli wapo.Kitendo cha wewe kukubali uwepo wa Aliens bila kujali kiwango cha wewe kuwajua hakuwezi kuwafanya wakawepo,kama kweli hawapo...

Wewe unafikiria nini?

Aliens ni hoax?
Kuiper Belt ni hoax?
Au Aliens wapo lakini hakuna Kuiper Belt?
Au kuna Kuiper Belt lakini hakuna Aliens?

Lakini kuna "ushahidi" wa uwepo wa Kuiper Belt lakini pia kuna "ushahidi" wa uwepo wa Aliens...

Sasa je ni nini cha kufanya?

Mawazo na mtazamo wangu...

Hapo juu nimeelezea matokeo ya utafiti wa maeneo ambayo yapo angani ambayo mimi na wengi wanaosoma hapa hatuna uwezo wa kwenda huko tukadhibitishe.Lakini hilo halitufanyi tukatae au tukubaliane tu kirahisi tunahitaji tufanye jambo zaidi na jambo hili ni kufikiri na kutafakari [reasoning] ili tuone kama yanaleta mantiki haya yote....

Kwa miaka kadhaa kumekuwepo na taarifa za kitengo cha sayansi za anga cha Marekani maarufu kama NASA kukubali uwezekano wa uwepo wa viumbe wa ajabu huko angani.Lakini si hivyo tu kule Marekani kuna sheria inayohusiana na kuelekeza kuhusu mawasiliano baina ya raia wa Marekani na viumbe wa angani huko ambayo ni Title 14, Section 1211....

Sheria hii inazungumzia kuhusu masuala haya ya kuwasiliana na hawa viumbe..

Kwa namna ya kawaida kabisa,ni jambo lisilowezekanika mambo haya yakawa ni hadithi halafu kukawa na matukio kama haya.....

Lakini sio hayo tu.Hapo juu tumeona baadhi ya ajenda mbali mbali za hao Aliens ambazo ni kuwaondoa binadamu katika dunia hii kwa kuwaangamiza.Kwa sisi ambao tunafuatilia mambo nje ya yale ambayo yamekuwa yakitangazwa tunafahamu sana vita iliyopo baina ya kundi moja dogo na kundi kubwa sana la binadamu kwa kundi dogo kutengeneza namna mbali mbali za kupunguza idadi ya binadamu hapa duniani kama siyo kumuondoa kabisa kwa kutengeneza maradhi fake na kuleta tiba ya maradhi hayo ambayo ni ya kumuangamiza huyu huyu binadamu.Jambo hili linafanana sana na ajenda za hao Aliens kama zilivyoelezwa na watafiti....

Ieleweke kwamba kwangu mimi ni kweli kabisa kuna kundi moja la watu ambalo linatengeneza dawa,maradhi na mtindo wa maisha ambao utamuangamiza kabisa huyu binadamu.Sijui kama ni hao Aliens aina ya Humanoid ndiyo wanafanya haya kwasababu tumeambiwa hapo juu kuna wengine unaweza kukaa nao na usijue,lakini kutokana na ajenda yao naweza kuunganisha dots na kuona kuna ka ukweli fulani hivi kwenye hili maana kuna mfanano wa mambo....

Yote katika yote,sijui kama ni kweli jambo hili liko hivi,inawezekana kukawa hakuna ukweli wote lakini nina uhakika hakuna uwongo wote hii ina maana kuna ukweli mkubwa tu pia,lakini kwangu mimi ni kwamba Aliens wapo na wapo hapa hapa duniani na pia wanahusika sana na maendeleo ya teknolojia iliyopo sasa hivi.Nitakuja kusema siku nyingine kuhusu maendeleo ya teknolojia yaliyopo hapa duniani na kule inakotoka lakini kwa leo niseme tu kuwa kuna mahusiano makubwa sana na jambo hili na maendeleo ya kiteknolojia tuliyonayo binadamu hapa duniani....

Binadamu leo ni kama watumwa.Kuna kundi la viumbe linamuendesha sana binadamu kuanzia namna anavyofikiri hadi kutenda.Sisi ni watumwa.Tumetengenezewa maisha fake na system fake zinazotufanya tuendelee kuwa watumwa.Watetutemngenezea siasa,wametutengenezea mtindo wa maisha ambao ndani yake tunajitesa sana na kuhangaika na mambo yasiyokuwa na maana na kutufanya tuone maisha haya ni kitu cha maana sana wakati kuna mengi makubwa zaidi ya hayo,hili nitalizungumza kwa kina siku nyingine,lakini kuanzia kufikiri,kuvaa,kutenda na yote sisi ni watumwa,tunaendeshwa kwa remote kutoka mahali fulani....

Haya yote,uwepo wa viumbe ambao wana uwezo zaidi kuliko binadamu na yote ni kuonesha kuwa binadamu yupo hatarini lakini hawezi kuwa hatarini kama hakuna uwezo wa kutoka kwenye hatari hiyo,je unasdhani ni ipi?

Tukutane wakati mwingine wakuu....

BTW,
Nitaendelea kuwa naandika makala kila nikipata wakati ili tuwe tunajuzana moja baada ya lingine kuhusu yale yasiyosemwa....

Tuendelee kuwa pamoja wakuu....
Kaka nimeisoma makala yako kwa umakini mkubwa kadiri ambavyo Mola wa ulimwengu amenijaalia.Mimi,wewe na wao sisi sote ni binadamu na hatujakamilika mkamilifu ni Mola peke yake,kwahiyo ukikuta kosa katika andiko langu ni sababu ya ubinadamu wangu.

Katika huu ulimwengu kuna jambo la umuhimu na umuhimu zaidi,na kuna kinyume chake pia.Kwa mujibu wa makala yako kama ulivyoeleza umesema ya kuwa umetoa ushahidi juu ya uwepo wa hao viumbe na ukanukuu ya kuwa wapo takribani sampuli 104,na ukatutajia chache miongoni mwazo.Kiukweli hata kwa mwenye akili ndogo na uelewa dhaifu kama wangu hatokububali kama wewe hapo umetuthibitishia uwepo wa hao viumbe.

MAELEZO MACHACHE JUU YA TAMKO "USHAHIDI"

Tamko ushahidi kiasili ni tamko la kiarabu lenye maana ya kushuhudia yaani kukiri.Ushahidi una mapito mengi sana mpaka ukafikia kiwango cha kuitwa ushahidi.Nataka nikupe mfano,kamwe kipofu hawezi kukupa ushahidi wa kuona,hapa nina maana pana sana,upofu upo wa kimaumbile na upofu wa kimaana.Mfano asie msomi ni muhali kukupa ushahidi wa kisomi na mfano wake.Ushahidi pia unapitia katika masimulizi kutoka kwa watu wenye kuaminika,wasomi,wenye ujuzi wa kupambanua jema kutokana na baya na mfano wake.Pia kuna ushahidi wa kuona,lakini ni ule ushahidi ambao nani ameona.Mfano wa tukio moja lililo ona na watu wanne kwa wakati mmoja na kila shuhuda kati yao akakupa maelezo tofauti juu ya kutokea kwa tukio hilo.Hapo ndipo utakapo staajabu suala zima la kuchukua habari na kuihakiki pia.Kwa ufupi hapa tunaona kuna ushahidi wa kuona,kusikia lakini kwa kukidhi vigezo.

SAYANSI NA VISASILI,PAUKA PAKAWA NA NGANO ZA KUSADIKIKA

Sayansi ya leo imekuwa kama hadithi na stori za vijiweni huku zikitiliwa nguvu na mapicha picha ya kubuni,kutilia nakshi dhana zao.Mimi baada ya kuupata ukweli juu ya suala la mtu kwenda mwezini,hapo ndipo nilipoinua kalamu yangu na kufumba macho yangu juu ya suala la kuamini tena mambo ya anga.Sijakuilia katika kukaririshwa,nimekulia katika uhakiki wa habari na wapi nikachukue habari.

Kuna ukweli ambao kila mtu mwenye akili timamu anapaswa kuujua ya kuwa si kila kinachezungumzwa na sayansi au wanasayansi kina ukweli,la hasha kufikiri kwa mtindo huo ni kufikiri kwa kitoto.Sayansi imekuwa yao kwa ajili yao wenyewe wanasayansi kufurahisha nafsi zao,kwani wanajua ya kuwa watu wa leo ni vigumu sana kuhoji na hata kama wakihoji hoja zao zitawafikia wakina nani na lini ? Kujadili ya maana muda huo hatuna tuna muda wa kusaka umbeya mitandaoni na kumsema fulani.Mwanachuoni mmoja alipata kusema "Itafikia zama jambo la kufanya kwa wiki moja litafanya kwa muda wa mwaka".Hakuziona zama zetu wala hakuiona kesho yake,bali elimu aliyopewa ikamuakisia ya mbeleni kwa idhini ya Mola aliye juu.Ukweli wa kauli yake uko wazi mithili ya tulionavyo jua la saa sita mchana.Leo tumeshughulishawa na mambo ya kijinga na kuacha kufanya mambo ya msingi,mwisho wake tunapotaka kufanya mambo ya msingi tunakuwa na uchache wa taarifa juu ya jambo husika,na tukianza kufanya basi nanga inapaa.

SAYANSI HAINA UWEZO WA KUJIBU AU KUELEZEA SUALA LA UWEPO WA VIUMBE FULANI NA UHAI WAO

Sayansi haina uwezo kutuelezea juu ya uwepo wa maisha ya viumbe fulani na ukweli juu ya viumbe wao.Sayansi imejengeka katika misingi ya nadharia na kufanya majaribio,yaani aidha ianze nadharia lifate jaribio au lianze jaribio ifate nadharia.Sayansi inafanya na mwanadamu ambaye si mkamilifu,swali ni vipi upate ukamilifu kutoka kwa kisicho kikamilifu ? Swali hili ni jepesi mno.Sayansi haiamini mpaka kitu kionekane na nadra sana ukihisi.

Sitaki kujua walitumia nini au walitambua lini,sababu msingi ukianguka na jengo limeanguka.Picha wazitoazo wanasayansi juu ya masuala yote ya anga achilia mbali kuhusu hii ngano ya Aliens si halisi ni picha za kubuni.Hivi kwa maendeleo wayasemayo ni kweli wangekuwepo hao viumbe tungekosa picha zao halisi au hata video zao ?

Ukweli ni kwamba walijua jambo hilo halipo ndio maana wakaamua kummwagia sifa kiumbe huyo asiyekuwepo ya kuwa anaakili nyingi sana za kumzidi bina damu.Ili ukitokea kuhoji jambo hilo wasikupe jibu lenye kueweka.

Pindi wanasayansi walipojigonga juu ya swali je ni jua linazunguka dunia au dunia inazunguka jua ? Hapo ndipo utakapo ona makanjanja ya sayansi.

JE NI YUPI ADUI MKUBWA WA BINADAMU ?

Hili ni swali la msingi sana kujiuliza juu ya kile ulichokiwasilisha.Kutokana na ngano hii ya kisayansi inaonyesha kwa wazi ya kuwa hawa ndio maadui wakubwa sana wa binadamu,kitu ambacho si kweli.Adui mkubwa wa binadamu ni SHETANI kama vile Allah alivyotueleza katika Qur'an.(Natumia Qur'an sababu ndio kitabu ambacho nakisoma na ndio muongozo wangu).

Sasa labda waje hapo baadae wakanushe tafiti yao ya kuwa kiumbe walie mkusudia ni SHETANI wa kijini na sio hawa Aliens,hiyo ni baada ya kufanya utafiti zaidi ya miaka 100,hivi ndio wasemavyo waitwao wansayansi.Na kama wakiseama hivyo itabidi wajibu maswali haya.SHETANI wa kijini ni mmoja anaitwa ibilisi na yeye ndio ana kazi ya kuwaletea wasi wasi binadamu na kuwashawishi kufanya maovu.Zaidi ya hapo shetani ni sifa kwayo anaweza kuwa nayo binadamu na majini pia.

NI KWELI WAPO VIUMBE ZAIDI YA HIVI VILIVYOPO ULIMWENGUNI NA HATUVIJUI,TENA NAVYO VIPO VIWILI VIWILI

Huu ni ukweli mwingine ambao ni dharura mwanadamu kuujua.Mola mlezi anasema mwenyewe ya kuwa na katika viumbe msivyovijua viko viwili viwili,au kama alivyosema Allah.Na Allah anaendelea kuumba ila katika hao viumbe tusio wajua ni sisi hatuwajui na hatuwezi kuwaelezea sababu hatuwajui.Kwahiyo sual la ugunduzi juu ya viumbe tusivyovijua ni halipo sababu hatuvijui.Sasa hili suala la Aliens limetoka wapi ?

NGANO YA ALIENS IMEKOSA SIFA ZA KIELIMU NA UHAKIKI WA HABARI

Suala la Aliens limekosa sifa hizo hapo juu.Sababu watoaji habari hawana sifa ya kuaminiwa kutokana na misingi yao dhaifu walijijengea.

BINADAMU NDIO MMBORA WA VIUMBE

Kutokana na nususi za kiimani na ndizo nususi za kweli na zenye kuaminika sababu maandiko yaliitangulia sayansi kitambo sana.Nususi hizi zinasema hakuna kiumbe mmbora kuliko mwanadamu hata majini hawafikii ubora wa binadamu.

ZIADA

Maelezo hayo ni maoni machache katika yale niliyotaka kuyatoa,na wakati mwingine nikipata muda nitakuja na maswali juu ya kile ulichokiwasilisha.

SIKU NYINGINE KIONGOZI TUELETEE USHAHIDI JUU YA UWEPO WA HAO VIUMBE.NAJUA USHAHIDI HAUNA WALA HAUTAKUWA NAO.

HITIMISHO

Hakuna viumbe viitwavyo Aliens kwa sifa hizo na maelezo hayo na sayansi haina uwezo wa kuelezea uwepo wa kiumbe chochote na chenye kuishi bila kukidhi vigezo vya uhakiki wa habari.Bali kuna majini,na watakuja kudhihiri viumbe viitwavyo YAAJUJ WA MAAJUJ navyo ni katika uzao wa Adamu,yaani binadamu kama sisi sema wanasifa z uharibifu na mfano wake.
 
Katika huu ulimwengu kuna jambo la umuhimu na umuhimu zaidi,na kuna kinyume chake pia.Kwa mujibu wa makala yako kama ulivyoeleza umesema ya kuwa umetoa ushahidi juu ya uwepo wa hao viumbe na ukanukuu ya kuwa wapo takribani sampuli 104,na ukatutajia chache miongoni mwazo.Kiukweli hata kwa mwenye akili ndogo na uelewa dhaifu kama wangu hatokububali kama wewe hapo umetuthibitishia uwepo wa hao viumbe.
Mkuu

Kwenye makala yangu kwanza nimeanza kuzungumzia kuhusu uwepo wa aneo ambalo kisayansi lina ushahidi wake....

Ninafahamu kwamba hakuna picha halisi za Aliens na jambo hili haliwezi kufanya wasiwepo.Sijasema kwamba picha nilizoweka ni halisi......

Sijui kama unaelewa kuwa hadi kitu kikubalike au kiwe kimethibitishwa ni mpaka taasisi zilinazokubalika na serikali duniani kukubaliana na suala husika.Mfano ni kwamba kama kitengo cha sayansi ya anga cha Marekani ambacho kinakubaliwa na serikali ya Marekani na dunia kwa ujumla kikikubaliana na uwepo wa sayari fulani basi jambo hilo hukubaliwa ramsi na kuanza kufundishwa mashuleni.Suala hili la Aliens halijakubaliwa na hao wanasayansi isipokuwa wanasayansi binafsi na walioamua kufanya utafiti wao binafsi ndiyo wanakubaliana na suala hili...

Unapaswa ulielewe jambo hilo kwasababu inaonekana unadhani kuwa jambo hili linakubalika rasmi duniani.Pamoja na hayo kuna watu wengi tu ambao wamehojiwa na kusema wameshawaona hao Aliens,huo ni ushahidi labda uwe hauukubali.....

Kwasababu hii hoja yako ya kulikataa jambo hili kwa kuegemea dhana yako ya kutokukubaliana na wanasayansi linakosa mashiko kwasababu uwepo wake hauegemei kauli za wanasayansi pekee kwani wapo mashuhuda pia....

Suala lako la kufikiri kuwa binadamu hawezi kujua uwepo wa viumbe wengine mahali pengine sijalielewa vizuri hasa limesimamia wapi.Kujua ni kufanya nini kwani? Naona hapo umesema kuwa ukamilifu hauwezi kutoka kwenye kutokukamilika,kwani kujua jambo ni ukamilifu?

kuwepo kwa Aliens na kuonekana kuwa adui ya binadamu hakumuondoi Shetani kuwa adui wa binadamu .Naona wengi wanachanganya jambo hili kwa kudhani kuwa uwepo wa Aliens unamfanya Shetani asiwepo....

Hao Aliens wanaweza kuwa ni product ya huyo huyo Shetani vile vile mkuu hivyo usidhani kuwa uwepo wa Shetani kunaondoa uwepo wa Aliens na kinyume chake....

Hivi mkuu ubora wa binadamu ni nini au uko wapi?

Msingi wa makala hii naona hujauelewa kabisa ndiyo maana unaendelea kudai ushahidi.Unaweza kuisoma upya ukaelewa zaidi mkuu....
 
Kiongozi ninapo sema misingi ya sayansi ndio kikwazo cha kufikia ukweli muhimili namaanisha mzee.Unaposema ya kuwa kutokuwepo picha za Aliens hakuondoi uwepo wa Aliens.Kauli hii si yakisomi na niayakukata tamaa,rejea katika misingi ya sayansi ndio ujibu hoja yangu.Kielimu kama huna ushahidi wa unachokiegemea hauna ruhusa ya kuongea.Kama picha picha halisi ya Aliens haipo kwanini wanatuchorea picha za kufirika ?

Mzee tabia ya ukweli unamea popote.Leo kuna mifano mingi ya juu ya mengi tusiyoyaona na wala hatujawi kupewa mfano wa picha za hayo mengi lakini tunayaamini na kuyashikilia kwa meno ya magego.Sababu kuna ushahidi makini juu ya hayo mambo mpaka umepelekea tukayaamini.

Na suala lako la wewe kusema ya kuwa yawezekana ya kuwa hao Aliens wanaweza kuwa majini ni uvivu wa kufikiri,ina maana ni jinsi gani unajaribu kuihujumu elimu na ukweli halisi,kama jambo hulijui kwanini usiulize au usiwaulize hao wanaoandika habari za Aliens ?

Swali litakuja Je unaweza kutupa uhusiano uliopo kati ya majini na hao Aliens,kama utakuja au unadhani ya kuwa hao Aliens wanaweza kuwa Majini.

Msingi wa ELIMU,ni kujifunza kwanza kabla ya kutenda na kusema.

Ukija kutaka kujua ubora wa binadamu hapa nakupa hoja za kiakili wala si hoja za kiufunuo hoja ambazo ni za hakika.Binadamu ndio viumbe waliopewa akili,na utambuzi wa kung'amua mambo na ubora wa binadamu unakuja kutokana na mambo anayayafanya na majuto anayokuja kujutia baada ya kufanya uzembe fulani.

Binadamu ndio aliepewa dhamana ya Elimu kuitumikia na kuifanyia kazi.Bibadamu ndio amepewa uwezo wa kuwatawala viumbe wengine,viumbe ambao kwa ukubwa ni zaidi ya mara hamsini kuliko mwanadamu mwenyewe.Mifano juu ya hili iko mingi na ukikataa itabidi uituhumu akili yako mzee.

Kuhusu kutokuielewa makala yako,maneno hayo si sahihi sababu,nimegusia mambo muhimu juu ya udhaifu wa sayansi na nikakupa maana ya tamko ushahidi.Jaribu kuiweka huru akili yako pia ujenge hoja kwa umakini,tuendelee kupeana faida....
 
Kaka msingi wa hoja zangu umemili kuwajibu wale wanaokubaliana na jambo hilo hasa hao wanasayansi.Suala la kusema kuna watu wamehojiwa na wameshawahi kuwaona ndio ikawa hoja juu yako juu ya kuthibitisha uwepo wa viumbe hao ? Huo ni uchache wa maarifa ya uhakiki wa Habari mzee.Uliza kwa sababu gani ? Jibu ni rahisi sana.Mathalani tukio la Zimbabwe linazungumzia juu ya ushahidi wao ya kuwa waliowaona hao viumbe ni watoto ? Swali la msingi kwanini wamehusishwa watoto na watu wa sehemu hiyo ? Pili,mtoto ni mtu na ni binadamu,pia,je mtoto ana nafasi gani juu ya kufanyiwa kazi kile anachokisema ? Katika masharti juu ya ushahidi wa mtu kuwa na nguvu na kufata hatua ya piliya kufanyiwa kazi,ni lazima huyo anayetoa ushahidi awe ni baleghe yaani amepevuka na sharti la ziada ni awe na uwezo wa kupambanua mambo kwa lugha za uhakiki wa habari tunasema awe na uwezo kumaizi mambo.

Sasa unapoleta ushahidi uliotokana na watoto unatakiwa kuangalia ndani zaidi ya utoto wao.Mara ngapi watoto waliona paka pori wakasema yule ni simba ? Na suala la wao kuchora walichokisema eti ukakijengea hoja ? Ajabu ilioje juu ya dunia hii.
 
Kaka niliandika katika hoja zangu ya kuwa misingi ya kisayansi ina udhaifu mkubwa sana katika kufikia hitimisho la jambo fulani ndio maana leo akisema A kesho watasema B.

Kwahiyo mimi najadili misingi ya kisayansi na matokeao yake na wewe unajadili matokeo ya sayansi bila kuijua misingi yao,hili ndio tatizo lililopo kati yetu.

Tengeneza kiti chako kwako ndio ukipambe mzee.
 
Kwenye kufikiri kuwa hoja yangu msingi wake ni sayansi tu ndipo penye tatizo na kwasababu hii nakuambia hujaelewa nilichokisema na hata ulichokinunuu ...

Mkuu kwanini usirudie kusoma huenda ukaelewa?

By the way,sayansi inadanganya wenye mambo yote au baadhi tu?
 
Kaka msingi wa hoja zangu umemili kuwajibu wale wanaokubaliana na jambo hilo hasa hao wanasayansi.Suala la kusema kuna watu wamehojiwa na wameshawahi kuwaona ndio ikawa hoja juu yako juu ya kuthibitisha uwepo wa viumbe hao ? Huo ni uchache wa maarifa ya uhakiki wa Habari mzee.Uliza kwa sababu gani ? Jibu ni rahisi sana.Mathalani tukio la Zimbabwe linazungumzia juu ya ushahidi wao ya kuwa waliowaona hao viumbe ni watoto ? Swali la msingi kwanini wamehusishwa watoto na watu wa sehemu hiyo ? Pili,mtoto ni mtu na ni binadamu,pia,je mtoto ana nafasi gani juu ya kufanyiwa kazi kile anachokisema ? Katika masharti juu ya ushahidi wa mtu kuwa na nguvu na kufata hatua ya piliya kufanyiwa kazi,ni lazima huyo anayetoa ushahidi awe ni baleghe yaani amepevuka na sharti la ziada ni awe na uwezo wa kupambanua mambo kwa lugha za uhakiki wa habari tunasema awe na uwezo kumaizi mambo.

Sasa unapoleta ushahidi uliotokana na watoto unatakiwa kuangalia ndani zaidi ya utoto wao.Mara ngapi watoto waliona paka pori wakasema yule ni simba ? Na suala la wao kuchora walichokisema eti ukakijengea hoja ? Ajabu ilioje juu ya dunia hii.
1;Unachokifanya hapa ni kutaka kuonesha kuwa wanasayansi ni watu waongo na ambao hawajawahi kufanya jambo lolote la maana kiasi kwamba ni wa kupuuzwa sana.hii siyo kweli hata kidogo na inawezekana labda kwako ni waongokwa kiwango hiki.Unaweza kutueleza kuwa ni waongo kwenye mambo yote?

2;Kimsingi watoto huwa wanasema kweli kabisa na ushahidi wao huwa unakubalika sana mahakamani hadi ithibitishwe walirubuniwa au kulazimishwa kwa njia mbali mbali kusema waliyosema.Dhana yako ya ushahidi wa mtu hadi abalehe ni dhana ya wapi sijui....

Bado sijaona sababu ya kufuatilia maelezo yako kwa kina hadi sana labda ukinipa maelezo ya kueleweka....
 
Kiongozi ninapo sema misingi ya sayansi ndio kikwazo cha kufikia ukweli muhimili namaanisha mzee.Unaposema ya kuwa kutokuwepo picha za Aliens hakuondoi uwepo wa Aliens.Kauli hii si yakisomi na niayakukata tamaa,rejea katika misingi ya sayansi ndio ujibu hoja yangu.Kielimu kama huna ushahidi wa unachokiegemea hauna ruhusa ya kuongea.Kama picha picha halisi ya Aliens haipo kwanini wanatuchorea picha za kufirika ?
Unaniambiaje nirejee misingi ya sayansi wakati wewe huitaki hiyo sayansi?

Sina ushahidi namna gani?
Mzee tabia ya ukweli unamea popote.Leo kuna mifano mingi ya juu ya mengi tusiyoyaona na wala hatujawi kupewa mfano wa picha za hayo mengi lakini tunayaamini na kuyashikilia kwa meno ya magego.Sababu kuna ushahidi makini juu ya hayo mambo mpaka umepelekea tukayaamini.
Haya maelezo yako yanakinzana na maelezo yako hapo juu,hebu rejea uone namna unavyo0jikinza....
Na suala lako la wewe kusema ya kuwa yawezekana ya kuwa hao Aliens wanaweza kuwa majini ni uvivu wa kufikiri,ina maana ni jinsi gani unajaribu kuihujumu elimu na ukweli halisi,kama jambo hulijui kwanini usiulize au usiwaulize hao wanaoandika habari za Aliens ?
Nani amesema kuwa hao Aliens wanawezekana kuwa ni majini?

Unasoma ninachoandika vizuri mkuu?
Swali litakuja Je unaweza kutupa uhusiano uliopo kati ya majini na hao Aliens,kama utakuja au unadhani ya kuwa hao Aliens wanaweza kuwa Majini.
Hili swali lako halina mashiko kutokana na msingi wa swali hili ambalo ni hiyo kauli yako hapo juu kuwa siyo ya kweli...
Msingi wa ELIMU,ni kujifunza kwanza kabla ya kutenda na kusema.

Ukija kutaka kujua ubora wa binadamu hapa nakupa hoja za kiakili wala si hoja za kiufunuo hoja ambazo ni za hakika.Binadamu ndio viumbe waliopewa akili,na utambuzi wa kung'amua mambo na ubora wa binadamu unakuja kutokana na mambo anayayafanya na majuto anayokuja kujutia baada ya kufanya uzembe fulani.

Binadamu ndio aliepewa dhamana ya Elimu kuitumikia na kuifanyia kazi.Bibadamu ndio amepewa uwezo wa kuwatawala viumbe wengine,viumbe ambao kwa ukubwa ni zaidi ya mara hamsini kuliko mwanadamu mwenyewe.Mifano juu ya hili iko mingi na ukikataa itabidi uituhumu akili yako mzee.
Kutawala maana yake nini kwa namna unavyoelewa wewe?

tuanzie hapo halafu uone namna unavyokuna kushindwa kutetea hiki unachoandika hapa...
Kuhusu kutokuielewa makala yako,maneno hayo si sahihi sababu,nimegusia mambo muhimu juu ya udhaifu wa sayansi na nikakupa maana ya tamko ushahidi.Jaribu kuiweka huru akili yako pia ujenge hoja kwa umakini,tuendelee kupeana faida....
Akili yangu iko huru sana,tatizo ni kwamba matatizo yako unayaonea kwangu kitu ambacho ni tatizo zaidi....

Wewe peke yako ndiye unasema umegusa mambo muhimu bila kujua kuwa unaweza kuona ni muhimu wakati kiuhalisia ikawa siyo....
 
Unaniambiaje nirejee misingi ya sayansi wakati wewe huitaki hiyo sayansi?

Sina ushahidi namna gani?

Haya maelezo yako yanakinzana na maelezo yako hapo juu,hebu rejea uone namna unavyo0jikinza....

Nani amesema kuwa hao Aliens wanawezekana kuwa ni majini?

Unasoma ninachoandika vizuri mkuu?

Hili swali lako halina mashiko kutokana na msingi wa swali hili ambalo ni hiyo kauli yako hapo juu kuwa siyo ya kweli...

Kutawala maana yake nini kwa namna unavyoelewa wewe?

tuanzie hapo halafu uone namna unavyokuna kushindwa kutetea hiki unachoandika hapa...

Akili yangu iko huru sana,tatizo ni kwamba matatizo yako unayaonea kwangu kitu ambacho ni tatizo zaidi....

Wewe peke yako ndiye unasema umegusa mambo muhimu bila kujua kuwa unaweza kuona ni muhimu wakati kiuhalisia ikawa siyo....
Kiongozi twende taratibu sasa,naona unaelekea kunielewa.Nimekwambia urejee misingi ya sayansi ili ujue ni yapi mapungufu ya sayansi na usiendelee kujadili matokeo ya sayansi sababu mafikio yako yatakuwa ni kubebeshwa uongo ulio mwepesi na kushindwa kuujua uongo huo.Misingi ndio asasi ya kujua hatima ya jambo husika,misingi imara huleta natija madhubuti.Sayansi siikubali hasa sayansi ya mambo ya anga kutokana na misingi yake.Natilia mkazo urejeetena na tena kwenye misingi ya sayansi ili ujue uozo wa sayansi.

Maelezo yangu kamwe hayapingani na ukiona yanapingana basi tambua kuna mambo mawili juu yako.

1.Kwanza ituhumu akili ya kuwa imeshindwa kuyadiriki mawazo na kuyaelewa ndio maana ukafikia hitimisho la kusema ya kuwa yana kinzana.Hapa naweza kukupa mfano juu ya kauli kwayo kwa uelewa mdogo utaweza kusema ya kuwa kauli hizi zina kinzana.Tazama kwa makini kauli hizi.

a) Nilijifunza shari niijue ili nisifanye shari na

b) Haifai mtu kujifunza kufanya mambo maovu.

Mwenye uchache wa kufikiri na kung'amua mambo hapo lazima atasema kauli hizi mbili zinakinzana.Swali la msingi litakuja ni wapi zinakinzana kauli hizo.Tusipende mteremko lazima tuzishughulishe kauli zetu.

2.Pili kuona kwako kauli zangu kama zinakinzana,lazima uituhumu elimu yako kuwa haina uwezo kung'amua mawazo yangu au hoja nilizo zihudhurisha hapo juu.
 
69 Reactions
Reply
Back
Top Bottom