Kuiper Belt: Behind the certain

Hizi issue za alliens nazo zinachanganya sana, kwangu huwa naona kama ni myth tu mpaka pale ntakapoweza kufikiria nje ya hapo,
Kuna taarifa nyingi sana kuwahusu ambazo nazo zinaonekana kama sio za kuaminika sana kulingana na ushahidi wa uwepo wao kuwa mdogo,

Ila kama kweli wapo na kwasababu teknolojia inakuwa kila siku basi nadhani tutaanza kuona uwepo wao kwa njia rahisi zaidi
 
Hizo ni Ngano + visasili
Kama ngano zetu huku kwamba kwenye mito kuna mijoka mikubwa? Mijoka inayozungumza...mijoka inayotema moto?

Hakuna ujenzi mtata kama wa pyramids hapa duniani. Ukiangalia structure, materials na muda zilijengwa. Ila hatusikii kama ni aliens waliojenga! Ila kwenye noti ya fedha waliochapisha hao wanaojiita chotara wa ki-aliens wameweka picha ya pyramid!

Pyramids zilijengwa kwa kutumia sound energy. Ngoma na nyimbo ziligongwa hadi mapande ya mawe makubwa yakawa yanapanda Juu na kujipanga kuform pyramids.

French revolution ni kama white revolution.... Weupe walizika rasmi historia, teknolojia na machapisho na majarida yote ya kisayansi ya watu weusi. Kuanzia hapo ndio tukaanza kukaririshwa..kutishwa hadi kusahau na kupoteza uwezo wetu wa kiasili na teknolojia.

NASA hadi Leo wameshindwa kutoa nadharia zao kuhusu global warming. Ni ujanja ujanja tu watu wachache wanatengeneza vitu/hali za kuogofya ili watengeneze fedha na waweze kutawala.

Kama kuna aliens bhas anaishi vichwani mwetu wote. Anaitwa pineal gland. Ni namna tu ya kumuamsha na kuona what we can't see. All illusions will gone.
 
Invisible ,hii thread bado mnaihariri tangu jana saa tisa alaasiri?
Hili suala huwa nawalalamikia sana mods huko PM mpaka wameniona mimi mkorofi...

Utaratibu wa kupitia uzi kaba ya kuuachia public kwenye jukwaa hili ni utaratibu mzuri sana lakini unakuwa unakera na muda mwingine kukatisha tamaa pale ambapo inachukua muda mrefu sana kufanyiwa moderation...
Yani mtu ukizingatia muda na nguvu uliyotumia kuandaa mada alafu inakuja kuchukua masaa chungu mzima Uzi umefichwa tu.... Dah inakera haswa!
Jamii forums walione hili...

Pia mkuu nikupe pole kwa huyu mpuuzi aliyekuwa anatoa kejeli humu kwa kuhusisha kejeli zake na jina langu... Pole sana kwa usumbufu uliopata!! Niko shocked kwa kweli kuona huyu mtu amejipa "mission" ya kupitia nyuzi za watu na kutoa kejeli huku anahusisha jina langu... Sijajua ana lengo gani haswa!
Pole sana mkuu...

Nimesoma kwa "kuscan" haraka haraka.... Sasa ngoja nisome kwa mara ya pili taratibu nami niinjoi utamu huu...

Good work mkuu!

Pia naomba unitag next time!! Wengine ndio "ulevi" wetu huu..

Cheers!!
 
nilipoona ni mambo ya kuiper belt kidogo nikimbie, mi na miamba mbalimbali
lakini kuona alien tu nikamakinika ,kuanza kutafuta mashine ya kuchambua hayo madini.
eiyer kazi bora hii.
nb:nb cjui ni simu yangu tu ,maana kwenye title naona certain, inapaswa kuwa hivyo au curtain.
ukiweka nyingine, tafadhali nitag
 
umeandka vzuri bro nmeshawah kusoma nakala flan la NASA wakikanusha uwepo wa viumbe wakati huohuo baadh ya mashuhuda kuptia majarida balmbal wameelezea uwepo wa aliens ila umechambua vizur sana sana nmependa na endelea kutupa uzi za kigeographia coz mm n mtaalam wa anga meteorologist so napenda hiz nakala na uchunguzi.
Pamoja sana mkuu,tuendelee kujifunza taratibu....
 
sasa kama hawaongei wanawsilianaje na Marekani?

Na wamejuaje nia zao?
huyo princess aliwapata wapi mpaka kusafiri nao
Kuhusu kuwasiliana nao nimeliongelea kwenye mada,unaweza kupitia hili...

Kuhusu hayo mengine nimejibu kwenye post iko page ya pili au ya tatu hivi,ngoja nitaangalia ni namba ngapi kisha nitakueleza....
 
Hongera mkuu Eiyer kwa makala nyingine nzuri na ya kusisimua.
Hawa aliens unaowaongelea wana uhusiano wa moja kwa moja na wanefili uliokuwa ukiwasimulia kwenye makala zako za nyuma? Je,kama hawahusiani ajenda zao,utendaji wao unakinzana na shughuli za Mungu juu ya mwanadamu? Je,inawezekana hawa viumbe ni tokeo la malaika waasi? La mwisho na la msingi kabisa,naomba uwe unanitag kwenye posti zako maana zinanivutia.
Mkuu,swali hili la kama kuna uwezekano wa kuhusiana kati ya Wanefili na Aliens nimeulizwa na mkuu mmoja hapo juu na nimemuambia kuwa nitaendelea kuandika makala kila nitakapokuwa napata muda na tutakuwa tunaunganisha dots taratibu na tutakuwa tunaelewa mkuu wangu....

Lengo langu ni kwamba kila mmoja awe anapata hitimisho yeye mwenyewe na siyo kutoka kwangu...

Jambo hili naomba pia liwe kwenye maswali yako yote mkuu wangu maana sitaki kuwawekea maneno midomoni mwenu.Kila siku mambo mapya yanaendelea kugunduliwa na pia kila siku taarifa mpya zinapatikana na inawezekana kile tunachokijua leo kikawa tofauti kesho hivyo tuendelee kupeana habari mkuu....

Pamoja sana kiongozi wangu....
 
Kwa ninavyoona USA ina mipango ya kiovu juu ya binadamu, wanachofanya ni kutufanya tuamini kuwa Aliens ni viumbe toka space ili vikianza kuleta uharibifu tukose cha kulalamikia. Mi nionavyo USA imelenga nchi za kimaskini hasa huku Africa ambapo teknolojia ni duni waweze kutufanyia ukatili wa kupora mali zetu kwa kutumia "Robots" afu waseme aliens. Hakuna mambo ya viumbe, sijui aliens, zote hizo ni hila za wazungu, mara utasikia Aliens kaonekana Zimbabwe kabeba Ng'ombe! Kumbe ni roboti linaloendeshwa na Mitambo. Tujichunge sana wakati ndo huu wa vita.
Safi sana mkuu kwa kuendelea kutafakari na taratibu tutaendelea kupata ufahamu mzuri zaidi..

Tutakuwa tunaandika makala hizi hili kuendelea kufikirishana ili tusiwe nyuma na dunia nyingine mkuu...
 
Wakati mwingine naanza kufikiria vibaya kidogo na kwenda mbal..najaribu kuwaza kwamba kwani huku JF kuna watu wamechaguliwa kua wao tuu ndio wakuandika kitu fulan??? Alafu huyu anaesema kazi hii muachie fulan....ni kwel ni third party ama ni huyo huyo ambae anajidai ni shabiki kuongeza kick??
Mkuu

Usiwe na wasiwasi maana namfahamu The bold ni mtu wa namna gani.The Bold ni mtu ambaye anapenda sana maendeleo na anajua kuwa maendeleo huja kwa kufikiri chanya.Huyo jamaa mawazo yake ni hasi na ni adui wa maendeleo....

Kimsingi ninachoandika ni tofauti sana na anachokiandika The Bold hivyo hakukuwa na shida yoyote ya huyo ndugu kupata shida....

Hata kama vingefanana hakukuwa na shida yoyote vile vile maana kunapokuwa na changamoto ndipo kunakuwa na vitu bora zaidi.Hebu fikiria kungekuwa na mwanamuziki mmoja tu duniani ingekuwaje....

All in all ninaheshimu mtazamo wake na pia ninaheshimu sana michango ya watu wengine pia....

Tupo pamoja sana mkuu...
 
Hao alliens wanaonekana nchi za mbele tu huko?

Viongozi mashuhuri duniani wamewaona ila viongozi wa Afrika sijaona aliekutana nao!

Umesema kuna kundi la binadamu wachache wenye nia ovu Juu ya wengi. Yes ni kikundi cha watu wachache..waoga na makatili kupindukia.

Wanaua watu kupitia mifumo ya afya, mazingira(global warming), uchumi, vita etc..sasa wametumia njia zote na bullet yao ya mwisho ni hiyo ya alliens baada ya ile ya secret society kufeli.

Hao aliens, kama wapo ni viumbe tu wa kutengeneza maabara through cross breeding. Kama walivyo robots.

Tunajua kikundi hicho cha wachache kinakazana kufanya depopulation, psyco operations, mind control hadi tunapoteza WILL power na kuanza kuogopa vitu vya ajabu.

Na NWO ndio inaelekea kufeli sasa .
Nilishawahi kukutana na taarifa ikionesha kuwa hata huku Afrika hao Aliens walishawahi kuonekana na tukio la karibuni zaidi ni la kwenye shule moja kule Zimbabwe....

Mkuu,kuna mambo mengine ukiyajua kuwahusu hawa Aliens maswali yanapata majibu taratibu tu na yanaisha,acha tuendelee kujifunza kuhusu haya kisha tutaendelea kupata ukweli zaidi mkuu....

NWO ni ishu pana sana mkuu na sidhani kama ni sawa kusema tu kirahisi kuwa imeshashindwa,tuendelee kujifunza mkuu....
 
Kwa kweli mleta mada amenifanya nifikiri nje ya box
Mkuu

Hili ndilo lengo langu haswa na nimefarijika sana kuona watu wanafikiria nje ya box maana tunapotoka nje ya box tunapata kujua mengi sana na kufikia tunapata majibu ya maswali mengi sana....

Karibu sana mkuu kwenye ulimwengu wa kufikiri nje ya box,ni ulimwengu unaostaajabisha na kufurahisha sana japokuwa wengine wanaogopa...
 
Kiukweli kama Mungu alituumba na aliumba ulimwengu wote, alafu akatuumba binadamu peke yetu tu na hakuna binadamu au viumbe wengine sehemu nyingine ya ulimwengu, basi Mungu atakua alifanya kazi chini ya kiwango.

Haiwezekani ulimwengu wote huu tuwe peke yetu tu.It doesn't make sense
Vitabu vingi sana vya kale ukiacha hivi vya kiimani vimeandika kuhusu uwepo wa viumbe wengine ukiacha hawa tunaowajua wanaoonekana kwa macho....

Yapo mengi sana humu duniani mkuu...
 
Kifupi ni kuwa kuna chombo kilianguka huko milimani uswis,ambapo watu 11 watalii wa kizungu walikiishuhudia na Mmoja kupiga picha,baada ya muda kiliondolewa hicho chombo kwa siri kubwa lkn ktk hicho chombo kulikua na viumbe hao watatu ila walikuta wawili mmoja kaenda wapi yukp wapi haijulikani,mchezo unaanzia hapo na wale mashuhuuda wote 11 wanatakiwa kuuwawa haraka mmno kabla hawajamhadithia MTU.... In SIRI inawezekana wapo kweli hapa duniani unaweza kukitafuta mie ninacho
Hizi taarifa zinazuiwa kwa gharama yoyote na sijui ni kwanini....

Taratibu tukiendelea kutafiti tutajua tu mkuu....
 
Hili suala huwa nawalalamikia sana mods huko PM mpaka wameniona mimi mkorofi...

Utaratibu wa kupitia uzi kaba ya kuuachia public kwenye jukwaa hili ni utaratibu mzuri sana lakini unakuwa unakera na muda mwingine kukatisha tamaa pale ambapo inachukua muda mrefu sana kufanyiwa moderation...
Yani mtu ukizingatia muda na nguvu uliyotumia kuandaa mada alafu inakuja kuchukua masaa chungu mzima Uzi umefichwa tu.... Dah inakera haswa!
Jamii forums walione hili...

Pia mkuu nikupe pole kwa huyu mpuuzi aliyekuwa anatoa kejeli humu kwa kuhusisha kejeli zake na jina langu... Pole sana kwa usumbufu uliopata!! Niko shocked kwa kweli kuona huyu mtu amejipa "mission" ya kupitia nyuzi za watu na kutoa kejeli huku anahusisha jina langu... Sijajua ana lengo gani haswa!
Pole sana mkuu...

Nimesoma kwa "kuscan" haraka haraka.... Sasa ngoja nisome kwa mara ya pili taratibu nami niinjoi utamu huu...

Good work mkuu!

Pia naomba unitag next time!! Wengine ndio "ulevi" wetu huu..

Cheers!!
Mkuu heshima kwako....

Mkuu ni kweli kwamba hata mimi nakubaliana na uongozi wa JamiiForums kwenye suala la kuweka utaratibu wa kukagua threads ambazo zinawekwa kwenye jukwaa hili kwasababu ni jukwaa la kipekee sana....

Lakini naona huo utaratibu una shida maana thread inakaa muda mrefu mafichoni hadi "mudi" inapotea kabisa.Ninakuelewa sana unapoongelea kuhusu kutokwa jasho kwenye kuandaa makala au mada kama hizi,unazurira sana huku na huko mtandaoni,unatumia muda mrefu na gharama zingine halafu wanakuja kuutunza tu uzi huko kwa siku kadhaa,dah inaboa sana....

Nadhani ni vyema hawa wakuu wakaliangalia tena hili suala....

Kuhusu huyo jamaa aliyetumia jina lako usijali mkuu,ninamuelewa sana alichokifanya na sababu ya kufanya,nimemsamehe na ninaomba nawe umsamehe pia kwa kutumia jina lako bila ridhaa yako na najua ni kiwango gani amekukwaza.Ujuwe kazi unayoifanya hapa ni nzuri sana na inawafanya watu wanakuwa "addicted" na mtu akisha kuwa hivyo haya ni matokeo yake....

Utamu na umahiri wa kazi yako mkuu ndiyo sababu na ninakubaliana na hilo maana wewe siyo mtu wa mchezo mchezo.Pamoja sana mkuu wala usiwe na tatizo....

Tupo pamoja kiongozi tuendelee na huu "ulevi" wetu mkuu....
 
nilipoona ni mambo ya kuiper belt kidogo nikimbie, mi na miamba mbalimbali
lakini kuona alien tu nikamakinika ,kuanza kutafuta mashine ya kuchambua hayo madini.
eiyer kazi bora hii.
nb:nb cjui ni simu yangu tu ,maana kwenye title naona certain, inapaswa kuwa hivyo au curtain.
ukiweka nyingine, tafadhali nitag
Shukrani mkuu kwa pongezi zako...

Ni kweli hilo neno nimelikosea na nimejaribu kulihariri [edit] lakini nimeshindwa,naomba sana Invisible au Paw mnisaidie jambo hilo tafadhalini....
 
69 Reactions
Reply
Back
Top Bottom