witnessj
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 28,839
- 47,746
HaaahaaaaMimi nilikua naskia simu kuwa sabuni,nilikua nawadharau wanaoibiwa.
Mwaka flani hivi nilipita pale kariakoo teja akanionesha simu kali ilikua Huawei.Nikajisemea moyoni ngoja nione hawa maboya huwa wanaiba vipi,nikamvuta pembeni.
Niliikagua simu zaidi ya mara 5,ipo fresh tukakubaliana nimpe 22,000/=.Nilizingatia hatua zote ili nisipigwe,simu nilikua nayo nikampa ela lakini alinilazimisha niiweke kwenye baasha yake sababu watu wataiona.
Nilihakikisha abadilishi kitu,mara tu alivyo nipa nilitoka nduki ghafla nikaanza kukimbizwa na watu wengine wawili lakini nikasikia sauti ya yule teja akisema muacheni.
Nilipanda daladala bila kujua linaelekea wapi huku nikijiona nimewakomesha.Gari ilivyofika muhimbili nikaona ngoja niiangalie simu yangu niliyojipatia bila jasho.
Duuuh,Sikuamini macho yangu....kukuta kipande cha sabuni.
Wale huwa wanatumia NDUMBA
....Mi juzi kati teja pale pale round about msimbazi akanionesha samsung kali kinoma anauza 30 elfu....huwaga nasikiaga zile storee zao za sabuni!
Nami nikamvuta pembeni nikatoa hela nikamwambia nipe hiyo simu hela hii hapa ( huku namshikisha mkononi
Akagoma eti mbona na haraka sana
nisubiri ainfungie kwenye bahasha ya kaki coz wameiba dukani, nikamwambia nipe hivo hivo mi na pochi naidumbukiza fasta! Duuh teja likagoma akaanza kutukana na kufoka mara akanirushia hela angu
....nikajua huyu boya ntakuwa nimemkamata pabaya! Nikaokota mshiko wangu huku mateja mengine yanacheka huyoo nikasepa!