Kuibiwa kwenye Daladala

Kuibiwa kwenye Daladala

Mimi nilikua naskia simu kuwa sabuni,nilikua nawadharau wanaoibiwa.
Mwaka flani hivi nilipita pale kariakoo teja akanionesha simu kali ilikua Huawei.Nikajisemea moyoni ngoja nione hawa maboya huwa wanaiba vipi,nikamvuta pembeni.

Niliikagua simu zaidi ya mara 5,ipo fresh tukakubaliana nimpe 22,000/=.Nilizingatia hatua zote ili nisipigwe,simu nilikua nayo nikampa ela lakini alinilazimisha niiweke kwenye baasha yake sababu watu wataiona.
Nilihakikisha abadilishi kitu,mara tu alivyo nipa nilitoka nduki ghafla nikaanza kukimbizwa na watu wengine wawili lakini nikasikia sauti ya yule teja akisema muacheni.
Nilipanda daladala bila kujua linaelekea wapi huku nikijiona nimewakomesha.Gari ilivyofika muhimbili nikaona ngoja niiangalie simu yangu niliyojipatia bila jasho.

Duuuh,Sikuamini macho yangu....kukuta kipande cha sabuni.

Wale huwa wanatumia NDUMBA
Yani kitendo cha kumpa tena aishike simu bhasi umepigwaaa...!!
 
Kuuziwa sabuni ilitokea nikiwa Form 3 na jamaa angu aisee... Tulienda kununua Housing ya Nokia enzi hizoo ilikuwa unahit balaaa wee sasa tukavutiwa na simu ya tejaa yanii Tukajuaa tumewin jamaa akanipaa niishike me simu aliweka kwenye Bahashaa aisee tupo tushapanda gari nkasema ngoja niibonye bonye kidogoo... Japo sio Mimi nilitoa helaa ilaa nilihisi kulia japo nkaanza kucheka jamaa hakuamini...40000 kwa sabuni
 
Hahahahahaha mkuu sitaki kuamini ya kuwa huwezi kuibiwa
sas kuna huyo kibaka.. nimegombea gari... dirishani... huku gari inaenda... akajifanya mjanja kuchomoa pochi yangu.. nikamdaka mkono... hapo gari inaenda.. sijamuachia.... dereva akataka kusimama.. nikamwambia kanyaga baba... wee vuta wese... yule teja akaanza kuliaa nimuachie..... dereva nae kichwa kibovu anakanyaga mafuta tu.. nilimburuza kama mita 100 hivi.. nikamuachia.. gari ikasimama watu wakaenda kumchek.. mie sina habari nakagua vitambulisho vyangu kama bado vyote vipo
 
Niliibiwa mkufu wa dhahabu wakati najiandaa kuteremka kutoka kwenye daladala nilihisi ni panga limekata shingo kumbe ni kofi lililonishtua na jamaa kuambaa na mkufu nikiwa namuona. Ni kitambo kdg miaka ya 90+
 
sas kuna huyo kibaka.. nimegombea gari... dirishani... huku gari inaenda... akajifanya mjanja kuchomoa pochi yangu.. nikamdaka mkono... hapo gari inaenda.. sijamuachia.... dereva akataka kusimama.. nikamwambia kanyaga baba... wee vuta wese... yule teja akaanza kuliaa nimuachie..... dereva nae kichwa kibovu anakanyaga mafuta tu.. nilimburuza kama mita 100 hivi.. nikamuachia.. gari ikasimama watu wakaenda kumchek.. mie sina habari nakagua vitambulisho vyangu kama bado vyote vipo
Hahahahahaha mkuu kutapeliwa vipi ulishawahi?
 
Mwenyewe mtoto wa manzense rakini niliibiwa kisimu cha tochi daah nilimbaindi aisee
 
kutapeliwa.... hiyo kweli nimewahi... kudadeki... ila nilikuja kuwarudia wale washenzi... nikawachimba mkwaraaaa... ila ndio hivyo nimeshatapeliwa
kipindi hicho nasoma form two.. pale ubungo.. nilienda na bro wangu mmoja hivi kulikuwa na mishemishe.. sasa... wakaja wale wanaouza simu za wizi... ilikuwa ni NOKIA fulani kali kinoma.. nene.. hivi.. sasa kumbe wanazo mbili simu moja ni OG na nyingine ni fake... imetiwa mchanga mbichi katika housing.. sasa tukaingiwa na tamaa.... ilikuwa inauzwa elfu 15..

ishu ilikuwa hivi.. mkono wa kulia katika mfuko aliweka simu og alaf upande wa kushoto aliweka fake.. wakat tunampa hela (tulichanga) akabadilisha .. akatupa ya mkono wa kushoto maana wakati tunaikagua tukajihakikishia ni simu kweli akairudisha mfukoni.. (hapo hatuelewi)... daah tunakuja kushtuka tupo nyumbani... daah.. nilirud na bonge la sime....... mamaeee siku ile ningechinja mtu
 
Vipi ulimkuta mkuu??
 
Mimi ilibaki kidogo teja anichomolee simu huku nagombania daladala maeneo ya mwenge. Machale yalinicheza kugeuka nyuma naona mtu kachomeka vidole kwenye mkoba nilimkata jicho alivyozuga nikabaki kucheka.
Aisee ulipona sana maana jamaa huwa wanakuotea vibaya
 
Aisee hakuna kitu kinaweza kukufanya utamani kuliaa lakini Machozi hayatoki Kama Kugombania siti ya Gari umekaa vizuri kuchek mfukoni hakuna Simuu...!! Aisee ilinikutaa mbagala siku mojaa achaa tuu rohoo iliniuma mpaka safari Nikaairisha...tuambie ni tukio gani la kuibiwa kwenye usafiri unalikumbukaaView attachment 870163
Acha maada za kijinga
 
Vipi ulimkuta mkuu??
sikuwakuta... ila naamini walikuja kupewa taarifa na wale wanaouza vitu chini (wamachinga) maana kuna mmoja nilimtaitisha vibayaaa sana... nilimuwekea sime shingoni anielekeze wale washenzi wanapatikana wapi.. maana wakati tunaongea na wale matapeli.. yule machinga alikuwa anachochea.. tununue... sasa nilirudi nikamkuta palepale... niliimba nae... daah nikikumbuka nasema kweli siku hizi roho mbaya sina
 
Niko zangu Kariakoo kuna teja kajigongesha kwangu kisha akaanza kuniletea zakuleta na mm nikaanza kumpandishia akawa mpole, dah! Sijui huwa wanadawa maana ile napiga hatua kadhaa mbele najipapasa mifukon sina kitu. Aisee, niliumia sana ile hata usingiz sikulala.
Yaani wale wakati mnajibizana huku mkisukumana wengine wanafanya yao, alkua mpole maana aliona wenzie washamaliza kazi,
Mi walining'iniza mguu mmoja juu huku ananitingisha sana kwa sababu naujua mchezo nkawa nawangalia wale wa pembeni wanaosachi wakasepa na jamaa kaniachia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom