Kuibiwa kwenye Daladala

Kuibiwa kwenye Daladala

Nilikuwa mgeni Dar kipindi hicho. Pale Posta Mpya, kipindi hicho naishi Mwananyamala, kikaja kipanya ile tunagombania kuingia kwenye daladala, bila kujua mkono wangu ukawa umegusa kwenye mfuko wa shati wa abiria mwingine, ambaye wote tulikuwa kwenye process ya kudandia daladala. Jamaa akasema mwizi,mwizi. Duh I was baffled!!!!!, mwili wote ulipata ganzi.
Nadhani kulichoniokoa, abiria waliangalia na kuamini I was not a snatcher, kwa ile innocence look niliyokuwa nayo.
 
Hapa kuna darasa
Japo kadri teknolojia inavyokua ndo nao wanapata mbinu mpya ila kuna la kukutahadharisha
 
dah, nilishindwa maana hata yeye mwenyewe alikuwa analalamika kwamba kuna mteja kampa aangalie laptop halafu huyu mteja haonekani... maana huyo muuzaji alikuwa anaingia ndani na kutoka....
Daah msala huoo..laptop ilikuwa poa lakini??
 
Nilikuwa mgeni Dar kipindi hicho. Pale Posta Mpya, kipindi hicho naishi Mwananyamala, kikaja kipanya ile tunagombania kuingia kwenye daladala, bila kujua mkono wangu ukawa umegusa kwenye mfuko wa shati wa abiria mwingine, ambaye wote tulikuwa kwenye process ya kudandia daladala. Jamaa akasema mwizi,mwizi. Duh I was baffled!!!!!, mwili wote ulipata ganzi.
Nadhani kulichoniokoa, abiria waliangalia na kuamini I was not a snatcher, kwa ile innocence look niliyokuwa nayo.
Aisee Huyo MTU hakufikiria kwamba unaweza kuuliwa mkuu daah
 
Mimi nilikua naskia simu kuwa sabuni,nilikua nawadharau wanaoibiwa.
Mwaka flani hivi nilipita pale kariakoo teja akanionesha simu kali ilikua Huawei.Nikajisemea moyoni ngoja nione hawa maboya huwa wanaiba vipi,nikamvuta pembeni.

Niliikagua simu zaidi ya mara 5,ipo fresh tukakubaliana nimpe 22,000/=.Nilizingatia hatua zote ili nisipigwe,simu nilikua nayo nikampa ela lakini alinilazimisha niiweke kwenye baasha yake sababu watu wataiona.
Nilihakikisha abadilishi kitu,mara tu alivyo nipa nilitoka nduki ghafla nikaanza kukimbizwa na watu wengine wawili lakini nikasikia sauti ya yule teja akisema muacheni.
Nilipanda daladala bila kujua linaelekea wapi huku nikijiona nimewakomesha.Gari ilivyofika muhimbili nikaona ngoja niiangalie simu yangu niliyojipatia bila jasho.

Duuuh,Sikuamini macho yangu....kukuta kipande cha sabuni.

Wale huwa wanatumia NDUMBA
Hahaaaa uliuziwa sabuni 22,000
 
Nilikuwa mgeni Dar kipindi hicho. Pale Posta Mpya, kipindi hicho naishi Mwananyamala, kikaja kipanya ile tunagombania kuingia kwenye daladala, bila kujua mkono wangu ukawa umegusa kwenye mfuko wa shati wa abiria mwingine, ambaye wote tulikuwa kwenye process ya kudandia daladala. Jamaa akasema mwizi,mwizi. Duh I was baffled!!!!!, mwili wote ulipata ganzi.
Nadhani kulichoniokoa, abiria waliangalia na kuamini I was not a snatcher, kwa ile innocence look niliyokuwa nayo.
Haaaahaaa abiria anapogeuka kuwa kibaka ...Lol
 
kipindi hicho nasoma form two.. pale ubungo.. nilienda na bro wangu mmoja hivi kulikuwa na mishemishe.. sasa... wakaja wale wanaouza simu za wizi... ilikuwa ni NOKIA fulani kali kinoma.. nene.. hivi.. sasa kumbe wanazo mbili simu moja ni OG na nyingine ni fake... imetiwa mchanga mbichi katika housing.. sasa tukaingiwa na tamaa.... ilikuwa inauzwa elfu 15..

ishu ilikuwa hivi.. mkono wa kulia katika mfuko aliweka simu og alaf upande wa kushoto aliweka fake.. wakat tunampa hela (tulichanga) akabadilisha .. akatupa ya mkono wa kushoto maana wakati tunaikagua tukajihakikishia ni simu kweli akairudisha mfukoni.. (hapo hatuelewi)... daah tunakuja kushtuka tupo nyumbani... daah.. nilirud na bonge la sime....... mamaeee siku ile ningechinja mtu
Ulivo wakosa ukabidi ukatie nyanya tu na hilo sime kupunguza hasira
 
Niliibiwa mkufu wa dhahabu wakati najiandaa kuteremka kutoka kwenye daladala nilihisi ni panga limekata shingo kumbe ni kofi lililonishtua na jamaa kuambaa na mkufu nikiwa namuona. Ni kitambo kdg miaka ya 90+

😂😂😂😂 aisee pole sana
 
HII KITU YA SABUNI ILINITOKEA NIKIWA FORM 5 NIKIWA NASOMA SEMINARY MOROGORO,NILITOROKA SEMINARY NIKASEPA ZANGU DAR,MCHANA WAKATI NAGEUZA NIKAPANDA BASI ZA ABOUD,NIKAKAA NA MTOTO MMOJA SHOMBE SHOMBE MKALI BALAA ILA HANA CHAPAAA

ILE NAENDELEA KUMDADISI JAMAA NAUGWADU WANGU TOKA SEMINARY SI AKATOKEA TEJA,TUKAFANYA BIASHARA KAMA KAWA,AKACHUKUA 40000 AKANIPA KIPANDE CHA SABABUNI


SEMA MLE UBUNGO NILISHAWAHI KUKAA MIEZ KAMA MINNE KWA MAZA MMOJA NIKIWA NAUZA GROCERY KIPINDI NASUBIRI MATOKEO YA FORM 4,KWA HIYO MASELA WOTE NIKAWA NAWAFAHAMU NA WAO WANANIFAHAMU SEMA YULE BOYA SIKUMFAHAMU

BAADA YA KUGUNDUA NIMEUZIWA KIPANDE CHA SOAP ILIBIDI NISHUKE KWENYE GARI NA KUMUACHA MTOTO MZURI AKIJUWA TUTASEPA WOTE MORO,NIKAENDA RIPOTI POLISI NAO WAKAZINGUA ETI HATUWEZI CHUKUA HATUA MAANA JAMAA HAWAJULIKANI,NIKASEMA POWA

NIKATAFUTA MASELA WANGU NIKAWAPA RIPOTI WAKASEMA TUPE DAKIKA 15 HELA YAKO ITARUDI

KUSIKILIZIA NIKAENDA BOOKING OFFICE NIKAOMBA WANIBADILISHIE TIKETI NIONDOKE NA BUS LITAKALOONDOKA BAADAE,KWELI WAKANIBADILISHIA

ILE GARI LINASEPA IKABIDI NIPANDE KUWAZUGA JAMAA KUWA NIMESEPA NA GARI ILE ILE KUMBE NIKASHUKIA GETINI NA NIKAINGIA ZANGU CHOONI NIKABADILI NGUO,NIKAINGIA TERMINAL NIKAANZA KUMSAKA JAMAA

KUMBE NAE ALIVYOMJINGA AKAJUWA NIMEONDOKA KWELI,SI AKAENDELEA NA BIASHARA YAKE YA KISABUNI NA KARANGA,MARA NIPO NYUMA YA BASI MOJA IVI NAMUONA YUPO MLANGONI ANAUZA KARANGA,AISEE NILIPOMUONA JASHO LILINITOKA KWANZA,NIKAITA MASELA WANGU KIMYA KIMYA NIKAWAAMBIA BOYA NISHAMUONA,ILE JAMAA ANAGEUZA SHINGO TU ANAKUTANA NA WABABE KAMA WATANO IVI WOTE TUMEMZUNGUKA,TUKAMWAMBIA UKIJARIBU KUKIMBIA TU KWENU TUNAPELEKA MZOGA WANAINCHI WENYE HASIRA WAMEFANYA YAO,IKABIDI ATULIE KAMA MAJI MTUNGINI,KILICHOTOKEA ALINYOOSHA MIKONO JUU,NIKAINGIZA MIKONO MFUKONI NIKAKOMBA HADI HELA ZA CHENJI ZA KARANGA,NILICHUKUA 40000 NA NYINGINE KAMA 20000 IVI ZA KWAKE NIKAWAPA MASELA

MIE HUYOOOO,NIKAINGIA KWENYE GARI ILISHAJAZA NA NIKASEPA ZANGU SEMINARINI

NILIJIONA BONGE LA STERING BALAAA
Ila Shombeshombe ndo ukamkosa tena
 
Mimi nilikua naskia simu kuwa sabuni,nilikua nawadharau wanaoibiwa.
Mwaka flani hivi nilipita pale kariakoo teja akanionesha simu kali ilikua Huawei.Nikajisemea moyoni ngoja nione hawa maboya huwa wanaiba vipi,nikamvuta pembeni.

Niliikagua simu zaidi ya mara 5,ipo fresh tukakubaliana nimpe 22,000/=.Nilizingatia hatua zote ili nisipigwe,simu nilikua nayo nikampa ela lakini alinilazimisha niiweke kwenye baasha yake sababu watu wataiona.
Nilihakikisha abadilishi kitu,mara tu alivyo nipa nilitoka nduki ghafla nikaanza kukimbizwa na watu wengine wawili lakini nikasikia sauti ya yule teja akisema muacheni.
Nilipanda daladala bila kujua linaelekea wapi huku nikijiona nimewakomesha.Gari ilivyofika muhimbili nikaona ngoja niiangalie simu yangu niliyojipatia bila jasho.

Duuuh,Sikuamini macho yangu....kukuta kipande cha sabuni.

Wale huwa wanatumia NDUMBA

afadhali wewe ulijipatia sabuni wengine huwa tuntoka kapa kabisa....
 
Daah mimi nilinunua viatu(raba) pale kariakoo jamaa akanifungia fresh tu,kufika home navitoa mfukoni nakuta wameniwekea ndala(malapa) ya rangi tofauti afu yameisha mpk yametoboka kwny kisigino.

Kwa mara ya kwanza ndio nimehadithia leo humu jf kwa aibu niliyokua nasikia,tukio lilitokea 2007.

Najua tukio hilo halihusiani na kuibiwa kwny daladala ila ndo hivyo tena waungwana,tusameheane tu.
 
Wewe kama mimi mkuu, nilipandia ubungo nikashukia Tip Top nlikua nmevaa t shirt fupi kwaiyo simu ilikua inaonekana huku nimechomeka earphones kwa kujiamini kabisa, ile nashuka tu nikasikia Kama navutwa masikio alafu mziki umezima ghafla Sina hili Wala lile najishika mfuko nakutana na paja badala ya simu, asee iliniuma!!
Mkuu umenifurahisha.kwa hiyo ulishtuka ghafla tu mziki umezima!!
Kweli hawa watu wanatishaa
 
Niko zangu Kariakoo kuna teja kajigongesha kwangu kisha akaanza kuniletea zakuleta na mm nikaanza kumpandishia akawa mpole, dah! Sijui huwa wanadawa maana ile napiga hatua kadhaa mbele najipapasa mifukon sina kitu. Aisee, niliumia sana ile hata usingiz sikulala.
Nilishuhudia tukio kama hili.. inawezakana ulikuwa ni wewe labda. ilikuwa mtaa wa congo kariakoo. kijana aliye valia jeans mapana alikuwa anakuja kwambele yangu ghafla kuna jamaa akampiga kikumbo na kumpita kidogo nakuanza kulalamika jamaa nae akageuza shingo nyuma kujibu mapigo ya maneno. hilo ndio likawakosa akatoka mwingine mbele yake kama anampita akachomoa simu kwa ustadi mkubwa sana kutoka kwenye mfuko wa jeans. yule mwizi mwingine alivyoona jamaa yake amekamilisha akawa mpole. tukio lilitokea kwa haraka sana. sikuweza fanya chochote sababu jamaa walikuwa wengi
 
Nilishuhudia tukio kama hili.. inawezakana ulikuwa ni wewe labda. ilikuwa mtaa wa congo kariakoo. kijana aliye valia jeans mapana alikuwa anakuja kwambele yangu ghafla kuna jamaa akampiga kikumbo na kumpita kidogo nakuanza kulalamika jamaa nae akageuza shingo nyuma kujibu mapigo ya maneno. hilo ndio likawakosa akatoka mwingine mbele yake kama anampita akachomoa simu kwa ustadi mkubwa sana kutoka kwenye mfuko wa jeans. yule mwizi mwingine alivyoona jamaa yake amekamilisha akawa mpole. tukio lilitokea kwa haraka sana. sikuweza fanya chochote sababu jamaa walikuwa wengi
Mkuu mimi ilikuwa mitaa ya msimbaz. Ila jamaa wanafanya kwa ustadi mkubwa sana, tuwe makini.
 
Nilikuwa nasimuliwaga visa km hivyo sasa nami nisimulie wengine.
1:Matapeli wa kujifanya waganga.
Nimetoka Zakhiem kuweka Pesa Nmb zamani ilikuwa jiran na BBon oil station.
Mfukoni nina simu ya ku slide mpyaa ina week 2.
Basi natembea kwenda maeneo ya kipati sikupanda Gari.
Nikakutana na jamaa mmoja kavaa kanzu akanisimamisha akaniambia anamuulizia mama Flani maarufu wa hapo zakiem anauza kuku,
Nkamwambia simjui, wakati tunaendelea akatokea Jamaa mmoja kwa Nyuma kama anatupita,akamsimamisha mble yangu akamuuliza swali lile lile yy akasema anapajua japo sio sana.
Aksema "naomba mnisindikize ntawapa Japo pesa kidogo nisaidieni manake nimetoka Bagamoyo na ni muhimu kukutana nae leo kabla hajaondoka"
Nikamwambia jamaa mpeleke akasema "hii riziki ya pesa tugawane wote kama vipi twende tutagawana nunu kwa nusu."
Nikasema poa
(Safari ikaanza kwa miguu)
Mgeni:Mimi ni mganga maarufu naitwa mjukuu wa Babu kwetu ni Tanga shughuli zangu nafanyia Bagamoyo,Nimesaidia wengi akiwemo huyu Mama tunaeenda kwake,Alikuja na mtaji mdogo nikasafisha nyota sasa ni mfanyabiashara mkubwa anauza kuku na mayai.
Hapa nimekuja kuchukua Pesa zangu kwake.
Jamaa wa pili; Anhaaaa kumbe wewe unasafisha Nyota?
Mgeni fake; Ndiyo.
J2(Jamaa wa pili): Sasa ss hapa tunakusaidia kukupeleka huko kwa Mama,Je na ww unaweza ukatusaidia?
M_Fake:Ndio nyie ntawasaidien Bure.
J2;Akanigeukia
Mwanangu deal hilo tutatoka mwanangu kumbe tunatmbea na mtu maarfu huyu Babu tufanye mpango atusaidie.
1gb😀aah Kweli Bana!
M Fake:Sasa kati yenu kama mnafanya biqshara ndogondogo nitawasaidia..Kwanza una kitu laini hapo...
1gb:Kitu cha namna gani?
M-Fake:Mfano Karatasi ivi,au Rambo.
1gb:Sina.
J2;Mi ninayo karatasi.
M-Fake;Nipe
Yule jamaa wa pili akatoa karatasi akampa mgeni fake,M fake akanipa..akaniambia ana majini ya utambuzi yanafanya kazi wakati wowote..akaichana karatasi vipande viwili akanipa mm na j2,akatuambia tutafune.
Hapo kutoka zakiem tunashafika Kizuiani..afu nikawa kama nashtuka afu some time najisemea embu ngoja nione.
Nikawa simuelewi huyu mshikaji wa pili.
Mganga fake:Usimeze hyo karatasi,Ikilainika tema kwnye mkono hiyo karatsi afu angalia uniambie kuna nini.
Nikawa wa kwanza kutema.
Tobaaaaaaàaa!!!!!!!
Nikaona ni nywelenywele zimechanganyika na karatasi.
Akaniuliza vipi,Nikamwambia nilichoona
M-Fake:Unaonekana una matatizo makubwa lkn ntakusaidia
Jpili Akaulizwa na ww umeona nn akasema damu imechanganyika na Usaha.
Akasema msiogope nitawasaidia.
M-fake:Sasa kuna masharti majini hayapendi kuona vitu vigumu vigumu mkiwa navyo.
Kabla sijapandisha inabidi mtoe mviweke mahala pamoja.
J2:Hatuja elewa vitu gani?
M-Fake:Kama vile vitu vya silver kama una Vitu vigmu mfukni eiza simu,betry n.k
Akaendelea Sharti la pili
inabdi kila mmoja nimtibie peke yake..atahesabu miti ya mivinje Kumi mbele ndo tiba itafanyika maana kupata pagale(Jumba bovu) au Mbuyu sio rahisi, Si kweli Jamani?
Wote: Ndio.
Nikamuuliza Iyo mivinje na ipi?
Akasema j2:NI IZI nguzo za pembeni za umeme utahesabu Kumi mbele ndo tiba tutafanyiwa kila mtu kivyake.
1gb;Mmhhh sawa.
Hapo tushafika maeneo ya Saint Anthon tunaelekea 7 saba kwa Mpili
Hapo ndo kama ufahamu ukawa unakuja nikajisema moyoni hawa inawezekana wako Pamoja.
wakati naendelea kutafakari huku tunatembea...
Jamaa wa pili 2:Akatoa mfuko laini (AKatoa na simu yake akaiweka humo na vikolokolo vingine)
Aaaaargh kuona hivyo nikamwambia Jama mm sina kitu.
Akasema sio simu unayo..
Nikamwambia mm sitoi,Atibiwe yy mm nisha ghairi.
Tukawa tushafika Stendi 77 nikawaambia mm safari yangu imeishia hapa,Siendi kokote na simu sitoi.
Mganga fake akasema mbona tumekaribia,Ukihesabu mivinje kumi ni hapo mission tu ndo tiba itaanzia hapo.
Nikamwambia Kamtibie huyo mm nishaghairi..
Nikavuka zebra kwenda ng'ambo nilipovuka nikasimama nikavuka nikawapungungia mkono,Mimi huyoooo nikasalimika sikuibiwa chochote.
Fundisho
Ukipewa kitu chochote na mtu usiyemfahamu usitafune chukua weka mfukoni mwambie utakula baadae.
Lkn pia huwa wanatumia ndumba maana mm ilifika time nikawa sijielewielewi baada ya kutafuna kikaratasi..
ukiona hujielewi usifanye lolote utakaloambiwa,
ww jibu lako liwe sijui,hapana,sitaki.

2:Karume-Ilala(Wahuni)
Dada yetu alikuja kuosha macho town.
Sasa siku anaondoka kabla ya siku 3
Tukapanga tukachukue mazaga zaga Ilala(Mchikichini).
Hao Mm nikiwa na Dadaangu wawili akiwemo Mgeni..
Tukashuka Kariakoo (Stand ya zamani:Mbgl-KKoo)
Tukanyoosha barabara ya uhuru Hapo tunaenda Karume.
Mimi mbele sista zangu nyuma nimevaa ki modo simu imetuna inaoneka ki urahisi.
Tukafika maeneo ya china plaza(Zamani halikuepo)
Mbele kidogo Sina hili wala li
le natembea km kawaida fastafasta town sinaga muda wa kuburuza miguu, Jamaa akanipush Akanishika mkono
karibu na Bega,Akawaka huku ananitikisa kiasi kwamba mwili wote una shakeshake..
"Ms*ng* unatembea huangalii mbele,Mambo gani ya kis*ng* una umiza watu."
Sasa pembeni alikuwepo mshikaji amesimama karbu na mm pale ninapo tikiswa anasoma gazeti kafunika sura,kitendo cha kuanza kutikiswa jamaa akaniwahi aka leta mkono kwenye jinsi (kumbuka hapo natikiswa na nikitendo cha nusu dakika yote hayo yanatokea)
Nikamwona mshikaji nikamuwahi...
Nikamshika mkono akauvuta Fasta
Acha nimtukane yule kibaka msoma gazeti..yule mwingne akajiondokea sikumkariri hata sura.
Nikanusurika pia hapo..
Dada zangu walishuhudia tukio kwa nyuma yangu..
kuona ivyo
aaaaargh mbona wakanipa niwawekee simu pesa kila kitu nikabeba mm..
ahahahahaaaaaa nikaibuka stering siku hyo.

3:Teja na Sandals
Ukiwa unaenda Home(Mkoa)
Lazima ufanye shopping..ma zawadi nini na kadhalika.
Baaaaasi nikaenda kufanya shopping na kuna vitu nilikuwa nimeagiziwa nikaenda k/koo kununua.
Nimemaliza kununua vyote mfukoni nina salio km 20000 na chenchi
Basi naenda stendi Teja akanifuata
"Oyaa mzazi Sendo hii apa makini ni dondoshee buku ten nijikatae"
Likaibunua binua likaikunja km linaivunja...kweli nikaiona imetulia nzuri afu ni ngozi matata.
Nikamwambia elfu tano hii apa..
Nipe niondoke
Tukabishanabishana hapo mwisho nikamwongeza mia 2.
Akasema poa ngoja nikuwekee mfukoni.
Akatoa mfuko nyuma akaweka.(Kimsingi hakuweka wakati anatoa mfuko nyuma hua kuna mwenzake anajifanya anapita hapo anapopeleka mkono wenye vuatu nyuma huko nyuma anapewa na mwenzake mfuko ambao unaviatu vibovu bovu ndo anauleta mbele tyr kukuliza)


Akafunga tena freshi nikampa nikachukua mzigo nikatembea km hatua saba nikasema ngoja nihakikishe kabla sijafika mbali,ile nagusagusa kwa nje kabla ya kufua nikaona mbona mbonyeo km sio wa sandals nikafungua
"""Eshhhhhhh bwana eeeeeeeeeeh!!!!"""""

Ni yeboyebo mbili zimetembelewa mpk kisigino kime surrender kimesagika mpk baaaasi...
duuuu nikayatupa hapo hapo kugeuka silioni teja......
"Pumbaafu nimeibiwaje?"
nilikuja kuielewa hiyo mbinu baadae baaada ya kucheki vidio mtu akiibiwa hapohapo kariakoo kwa style km yangu.
Siku nyingine niliporudi nikamwona wala sikumletea noma nikamwacha tu,mi sipendagi kuanzisha noma nilimuona akiendelea na mchezo wake..
mara nyingi tu nikawa namuona na mchezo uleule.

4:Nagundua Mbinu ya kujilinda na wezi wa mifukoni na roba.
Kabla sijaachishwa na Yesu kunywa ulabu.
Nilikuwa na simamia Grocery flan ya pombe.
nikajikuta automaticaly nikawa mlevi nikaipenda pombe wana wakawa wananipa ma offer n.k.
Ikawa wakati flan tunatoka kwenda club na wana ila muda wa kurudi utajijua mwenyewe.
Sasa nikawa mara nyingi nikishuka stand mpk kufika home sina nauli ya bodaboda.
Kwa kuogopa kupigwa roba na wahuni nikawa nachukua chupa ya bia naipasuapasua.
Vipande vya chupa navitia mfukoni kwa uangalifu mkubwa.
Lengo.. atakae kuwa wa kwanza kupiga ndole atatoka na damu na majeraha😆😆😆.
Kwaiyo nikajikuta mm saa 8,9,10,Mimi natembea tu bila wasiwasi najua mifuko za nyuma/mbele zote nimetia majipande ya chupa ukiingiza mkono utajiju.
Simu ipo boxaniiiii
utajijuuuuu....

Aiseee kwa bht nzur sikuwahi kukabwa.
Tangu nilipo nilipo buni ulinzi wa mavyupa.
Teh...teh..teh...

Bonus story
TEJA ALIZWA KWA UTAPELI WA SIMU SABUNI.

Siku moja nipo ndani ya Bus nikawa nyuma ya seat ya Mama mmoja.
Akaja teja dirishani
"Oya simu matata kali kinoma mpya na box lake ili hapa nipe 30 Maza"
Mama yule akamuuliza wew iyo simu unauza kweli?
Jamaaa" ndiooo maza.
Akamwambia mie staki matatizo ukileta ujinga nitakuzingua kinoma mm mwenyewe kauzu.
Teja:Weee maza vp hii biashara..
Maza:Hebu nipe dirishan niione hiyo simu yenyewe.
Akampa.
Maza:Umesema bei gani?
Teja; 30 tu maza aaaah!!

Yule Mama hakumrudishia ile simu akatoa Pesa akampa dirishani.
Teja akapokea.
"Mama lete nikuwekee kwenye box lake.."
Yule Mama akakataaa katakata
teja acha aanza kutukakana...
watu kicheko ndani ya basi hatari.
Teja akaanza kumfosi Mama amuoongeze japo 20000
Mama Akagoma..
Daaah teja akawa kajichezea rough mwenyewe..
Yule mama akakaza akajipatia simu kali kwa 30000.

Angerudisha angefungiwa kipande cha msabuni.
alikuwa analijuwa hilo yule Mama.
Nikagundua teja akikuuzia gadgets ukiikagua usimrudishie akuwekee kwenye bahasha au mfuko.
Hapo ndo unabadilishiwa kwa techniques za kiteja.
Mkiwa wawili mpe simu mwenzio aishike ikiwa uchi, ww mlipe pesa teja.
hapo utamuweza japo hawachelewagi kugaili ama kulianzisha zengwe..

Like 90 Itapendeza.
Hapo chini minya like basi.
 
Aisee nilikuwa na toka temeke mwisho naenda kariakoo na katika mfuko WA shati niliweka bahasha kama 10 zikiwa na barua.unajuwa tena enzi ya post office.kabla ya simu.gari ilikuwa nyomi.vichwa hadi dirishani.nilibanwa mbavu ile mbaya.ile nashuka tu kariakoo. Nikipapasa mfukoni.barua hazipo.amesepa zake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom