Kuhusu unaoitwa uponyaji na tv zetu

Kuhusu unaoitwa uponyaji na tv zetu

Shikilia imani yako kwa uthabiti mkubwa. Dini sasa ni ujasilia mali, na wachungaji ni wajasilia mali kama wengine.
 
Siyo wote ni wasamii, penye mazuri na mabaya yapo.
 
Juzi niliona kipindi cha uponyaji cha anayejiita nabii Malisa, akasema sasa ntawaita viziwi waje niwaombee,wakapita kibao, akamuuliza mmoja ikawa hivi:
malisa: wewe ni kiziwi
jamaa: ndio
malisa:kwa muda gani sasa?
Jamaa: miaka miwili
malisa:unataka kupona?
Jamaa: ndio
malisa akamuwekea mkono kichwani na kumuombea kisha akasema tayari.
Nikasema kama ni movie hawakujipanga, kiziwi anaulizwa maswali anajibu bila hata kuonyesha kama anashida katika usikivu wake

Duuh, hapa pana kazi. Ni watu waliokuwa wamekaa jirani nao ndio waliwastua kuwa viziwi mnaitwa au walikurupuka tu wenyewe?!
 
Acheni majungu watu wanapona kweli
Sio majungu. mchukue bubu yoyote ama kiwete ambaye unamfahamu tangu zamani, mpeleke kwa waombezi km mzee wa Upako ama Rwakatare au yoyote anaedai kuwaponya watu hao. Akiweza kuombewa na kutembea ama kuongea tafadhali tuletee ushahidi hapa
Jf
 
hahahah sina coment.. hata mm niliona ile ya Nabii Malisa, ila sina coment
 
mi hawa wanaojiita manabii na watume sijui wanatumia vigezo vp? hivi hii dunia tuliyonayo kunabinadamu anafafa na mitume na manabii waliopita?kama kweli wanaombea na kupona mbona vipofu,viziwi wpo wengi mashuleni kwa nini wasiende mashuleni mwao wapige maombi mpaka wapone hata kama sio wote watakaopona maana hawacheliwi kukuambia huna iman kuna wenye iman watapona na watu watashudia na kuweka ushuhuda wa kweli.kuna nabii alikuja singida kuna baba mmoja ni bubu wa kuzaliwa na ni kilema alifanyiwa maombi hakupona na kila watumishi wapokuja huwa anaenda na ana iman ya kweli kwa kumuangalia mbona haponi?
 
ki ukweli na mimi huwa inanishangaza.maana kuna walemavu wengi na vipofu wengi.kama watu wana uwezo wa kuwaombea na kupona,kwa nini wasijitolee na kuwasaidia hao watu.kuna kijana mmoja namfahamu yaani ni tapeli kabisa,naijua back ground yake,ni tapeli mzoefu na yeye amekuwa pastor.kuna siku nilimtembelea,alivyokuwa nje akawa anaongea kikawaia tu,story za ki shakaji.hee kuingia nae ofisini,mara sauti ikabadilishwa na bwana asifiwe nyingi,kama mtu anaeombea hivi.ki ukweli nilishangaa,ila nikaona ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe,ingawa sikupenda
 
Vilema wangapi waliombewa na Mtume wa Allah wakapona? Je, Allah alipo mwombea Mtume wake, kuna ushaidi wowote kuwa yule Mtume alipona? Astaghafurillah. Achenu kusema vitu ambayo Allah wa Islam vilimshinda alipo jaribu kumwombea kipenzi chake na kufa kifo cha aibu cha kulishwa sumu na yule DADA WA KIYAHUDI.
ahsante nimekusikia,ila sitopenda kubishana na wewe.topic tunaiongelea hapa na unayoyasema wewe ni vitu tofauti
 
Kuna kitu kinanitia shaka kuhusu huu
unaoitwa uponyaji..
Kwanini watu wanaoombewa na kupona ni hawa tunawaona kwenye TV tu?
Toka umezaliwa umewahi kuona kipofu au kilema unayemfahamu akaombewa na kupona? Kwanini zinabaki hadithi tu, ukiwa Songea
utasikia watu wakisema "kuna kilema
Mwanza aliombewa akapona"...ukienda
Mwanza nako utasikia, kuna mtu Arusha
alipona...
Hatuchezewi akili kweli hapa?

Im just thinking!!!!
Safari ndefu sana. Changa la macho? Am also just thinking!
 
Yaani hakuna kitu ambacho huwa kinaniudhi na kunitia kinyaa kama ninapowaona hao manabii feki hasa huyo Malisa.Hebu mwenye habari za kakobe kwa sasa alipo anafanya nini tofauti na hapo nyuma atumwagie hapa,kulikoni kanisani kwake anaendeshaje ibada sasa hivi ni kwa majivuno kama zamani au vp.
 
Juzi niliona kipindi cha uponyaji cha anayejiita nabii Malisa, akasema sasa ntawaita viziwi waje niwaombee,wakapita kibao, akamuuliza mmoja ikawa hivi:
malisa: wewe ni kiziwi
jamaa: ndio
malisa:kwa muda gani sasa?
Jamaa: miaka miwili
malisa:unataka kupona?
Jamaa: ndio
malisa akamuwekea mkono kichwani na kumuombea kisha akasema tayari.
Nikasema kama ni movie hawakujipanga, kiziwi anaulizwa maswali anajibu bila hata kuonyesha kama anashida katika usikivu wake

Ha ha ha haaaaaaaaaaaaaa, hii kali kwa kweli. Mimi huwa ndo nachanganyikiwaga. Na kuanza kujiuliza wale manabii wa uongo ndo wameanza kuonekana?
 
hata mimi huwa najiuliza hivyo hivyo, maana sijawahi sikia kbs mtu ninaemfahamu amepata uponyaji zaidi ya hao wa tv.
 
Juzi niliona kipindi cha uponyaji cha anayejiita nabii Malisa, akasema sasa ntawaita viziwi waje niwaombee,wakapita kibao, akamuuliza mmoja ikawa hivi:
malisa: wewe ni kiziwi
jamaa: ndio
malisa:kwa muda gani sasa?
Jamaa: miaka miwili
malisa:unataka kupona?
Jamaa: ndio
malisa akamuwekea mkono kichwani na kumuombea kisha akasema tayari.
Nikasema kama ni movie hawakujipanga, kiziwi anaulizwa maswali anajibu bila hata kuonyesha kama anashida katika usikivu wake

baaass!
 
Back
Top Bottom