Kuhusu unaoitwa uponyaji na tv zetu

Kuhusu unaoitwa uponyaji na tv zetu

Nadhani kilicho bora ni imani yako mwenyewe bila kuangalia mwenzako anafanya nini, kama huamini unachokiona kwa mwenzio just keep silent and do your own business.

Nadhani wewe ukimkuta kibaka anampora bibi kizee ombaomba maeneo ya "Kigogo ya zamani" utapita tu hata bila hata kumsaidia bibi kizee huyo.

Tukirudi kwenye mada:

Mimi nadhani wewe ndiye uliyetakiwa "just keep silent and do your own business" ukatuwaachi 'thread' yetu tuchangie.

Binafsi sipendi kuingilia imani ya mtu, lakini pia sipendi mtu huyu atumie imani yake ya kidini kuwadhulumu watu. Kuna haja ya kufuatilia baadhi ya madhehebu yanayotiliwa mashaka juu ya utapeli.
 
Tusiendekeze ububusa mpaka tukaacha kuona ukweli, njia km hizi ndizo walitumia wakoloni kutawala watu. Ndio maana wazungu wengi walitupa hata kanisa kutokana na kuona wanapelekeshwa kibubusa.

Hakuna kweli yoyote nje ya Kweli ya Neno la MUNGU. YOH 8:32, Hasha, Mungu aonekane kuwa amini (kweli) na kila mtu Mwongo:RUMI 3:4. Tambua hilo.
 
mi hawa wanaojiita manabii na watume sijui wanatumia vigezo vp? hivi hii dunia tuliyonayo kunabinadamu anafafa na mitume na manabii waliopita?kama kweli wanaombea na kupona mbona vipofu,viziwi wpo wengi mashuleni kwa nini wasiende mashuleni mwao wapige maombi mpaka wapone hata kama sio wote watakaopona maana hawacheliwi kukuambia huna iman kuna wenye iman watapona na watu watashudia na kuweka ushuhuda wa kweli.kuna nabii alikuja singida kuna baba mmoja ni bubu wa kuzaliwa na ni kilema alifanyiwa maombi hakupona na kila watumishi wapokuja huwa anaenda na ana iman ya kweli kwa kumuangalia mbona haponi?

visual inspection misleads, anaweza kuwa ni mwanga balaa.
 
visual inspection misleads, anaweza kuwa ni mwanga balaa.

Hata uwepo wa manabii wa nyakati zile, haikuwa na maana kwamba viwete, vipofu, viziwi au wagonjwa walitoweka kwenye hiyo jamii.Hata kipindi cha Yesu wenye matatizo hayo hawakumalizika.Tena hata kipindi cha manabii na mitume wa sasa hao hawataisha.Cha muhimu chunguza ujue siri ya Injili ya Yesu inayookoa!!!
 
Kuna kitu kinanitia shaka kuhusu huu
unaoitwa uponyaji..
Kwanini watu wanaoombewa na kupona ni hawa tunawaona kwenye TV tu?
Toka umezaliwa umewahi kuona kipofu au kilema unayemfahamu akaombewa na kupona? Kwanini zinabaki hadithi tu, ukiwa Songea
utasikia watu wakisema "kuna kilema
Mwanza aliombewa akapona"...ukienda
Mwanza nako utasikia, kuna mtu Arusha
alipona...
Hatuchezewi akili kweli hapa?

Im just thinking!!!!

uponyaji upo kama mungu yupo, na anaeomba anamuomba mungu ambae jina lake linaandikwa kwa herufi kubwa sema uponyaji mwingi wa kwenye TV ni usanii kama unaofanywa na masheikh makaburini wa kufundisha maiti jinsi ya kujibu maswali wakati malaika atapokuja na bonge la rungu kumuuliza maswali maiti ili ayajibu kwa ufasaha vinginevyo akikosea anapigwa rungu la kichwa anazama mpaka ardhi ya saba halafu anachomolewa huko kwa ukucha anaulizwa swali jingine maiti ikichemsha tena inakula rungu za kutosha. ulishawahi kujiuliza yale maji wanayoenda nayo kuzika huwa ni kwa ajili ya nini?
 
Waganga wa kienyeji hawana pa kula siku hizi maana uganga umehamia makanisani. Wateja ni walewale ila maneno yamebadilika kidogo kwa kumtaja Mungu na Yesu.Lakini hawa manabii wamekwenda mbali kwa kuweka matangazo ya biashara katika TV na redio... Wanaenda kisasa zaidi.
Mimi niliona KBC TV.Mchungaji anasema.Anaponya hata wale walio mbali hasa hasa wanaomtizama kwanye TV ili uwe connected ta maombi yake na uponyeke kuna namba za MPESA zinapita kwenye csreen inawataka watume pesa ili wawe connected.wao waita CONNECTION MPESA ili upone.
 
Kwa upande wangu ninaamini uponyaji wa kweli upo vipofu wanaona,viwete wanatembea hata wenye nguvu za giza wanafunguliwa na nimeona kwa macho mengine pia sikatai kwamba kuna movie wengine wanazfanya majukwaani note:tutawatambua kwa matunda yao.
 
There’s nothing in the God Haters “non-theists” tag that specifies "belief", inter-alia, non-theist are Luciferians and worship c darwin (peace be upon him).

Upo sahihi mkuu, samahani sikujua kama niliyekuwa nahojiana naye ni MPINGA KRISTO!!
 
Juzi niliona kipindi cha uponyaji cha anayejiita nabii Malisa, akasema sasa ntawaita viziwi waje niwaombee,wakapita kibao, akamuuliza mmoja ikawa hivi:
malisa: wewe ni kiziwi
jamaa: ndio
malisa:kwa muda gani sasa?
Jamaa: miaka miwili
malisa:unataka kupona?
Jamaa: ndio
malisa akamuwekea mkono kichwani na kumuombea kisha akasema tayari.
Nikasema kama ni movie hawakujipanga, kiziwi anaulizwa maswali anajibu bila hata kuonyesha kama anashida katika usikivu wake
Mh jamani hii kali na tuiite funga mwaka 2012!
 
mambo ya dini ni Imani kali sana, Ya Mungu apewe Mungu ya Wanadamu waachiwe wanadamu wenyewe.
 
Watakuja wengi wengi kwa jina lake,watafanya miujiza kama yeye,lakini msiwaamini kwani hata shetani aweza kufanya miujiza(usiniulize nimetoa wapi)

Umeitoa kwenye msahafu wa shetani, hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia takatifu kuna hayo maneno. Usilolijua wala usicomment, bora unyamaze kaka. Kama Yesu alisema, "And these signs will follow those who believe: In My name they will cast out demons; they will speak with new tongues; they will take up serpents; and if they drink anything deadly, it will by no means hurt them; they will lay hands on the sick, and they will recover (Mark 16:17-18.” Itakuwa hivyo kwa waaminio halisi.

Unajua umefungwa jela (ya rohoni) na shetani (cos ana uwezo huo) mpaka unashindwa kuamini kuwa Jesus is working miracles using people today.
 
kuna ulazima wa wao kujitangaza kwa matv?
Mbona Yesu mwenyewe alikua anawakataza watu aliowaponya kuwa wasitangaze habari kuhusu uponyaji huo?
Msalipo msiwe kama wanafiki...endelea

Ona huyu nae, eti Yesu alikuwa anakataza watu wasitangaze uponyaji wake. Simple question, wakati wa Yesu hakukuwa na simu na mawasiliano yalikuwa magumu sana, watu walijuaje kuwa Yesu anaponya mpaka maelfu ya watu walikuwa wanasafiri toka pande zote za Israel kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.

Uponyaji wa Yesu ulikuwa unafanywa hadharani na sio mafichoni, mtu anafufuliwa live na kila mtu anaona!! Haya nikuulize, huko unakoenda wewe kusali kuna hata vocabulary ya uponyaji inatamkwa, au watu wanaingia na mapepo yao na wanatoka nayo.

Kama hakuna vocabulary ya uponyaji then your fathers transferred to you a wrong belief and you want to transfer it to your children, angalia sana.
 
Kuna kitu kinanitia shaka kuhusu huu
unaoitwa uponyaji..
Kwanini watu wanaoombewa na kupona ni hawa tunawaona kwenye TV tu?
Toka umezaliwa umewahi kuona kipofu au kilema unayemfahamu akaombewa na kupona? Kwanini zinabaki hadithi tu, ukiwa Songea
utasikia watu wakisema "kuna kilema
Mwanza aliombewa akapona"...ukienda
Mwanza nako utasikia, kuna mtu Arusha
alipona...
Hatuchezewi akili kweli hapa?

Im just thinking!!!!

ua a good thinker.
 
Na wote wanao ponywa 'wanakuwa na maneno mazzuri mno yaliyopangwa'
we hushangai hilo?
haitokei mtu akapona akawa hajui kujieleza
kila anaepona anajua kufagilia tu...

Mkuu The Boss, asante hasa hapo kwenye red..

Hivi wote wanaoponywa mbona wanakuwa na logic na maneno kama vile waliandaliwa hotuba? Hatuoni vilaza wasioweza kujieleza wakitoa ushuhuda!

Je Mungu tunayemjua anabagua ziku hizi akiwaponya 'brave people' tu?

Huu ni ujasiriamali!
 
huo ni ujasilia mali utatoaje sadaka kama hawatakutia kwanza hofu? uta ambiwa maombi yako hayawezi kusiklizwa kwakua huja panda mbegu au mbegu uliyopanda ni ndogo.

Mbona kanisa katoroka wanatoa sadaka (mpaka za kuombea wafu) na agizo la Yesu la kuponya wagonjwa is non of their business? Kutoa sadaka according to the bible is for the benefit of the one who is giving. Economics ya Mungu ni anayetoa ndio anayebarikiwa zaidi kuliko anayepokea. Kwa mfano, Marekani wanatoa zaidi na ndio maana they are more blessed kuliko nyie mnaokinga mikono kama kina matonya, mnazidi kudidimia kwenye lindi la umasikini na huku kila siku mnapewa misaada.
 
Waganga wa kienyeji hawana pa kula siku hizi maana uganga umehamia makanisani. Wateja ni walewale ila maneno yamebadilika kidogo kwa kumtaja Mungu na Yesu.Lakini hawa manabii wamekwenda mbali kwa kuweka matangazo ya biashara katika TV na redio... Wanaenda kisasa zaidi.

Kanisa la Freemason wameshindwa kabisa kwenda on TV, hawana Mungu anayeponya, wamebaki na masanamu na kuwaomba wafu.
 
wapo watumishi wa kweli mfano wa t.a.g, e.a.g.t, fpct, n.k pia wapo wasanii mf. huyo malisa, nyaga, suguye,rwakatare

Lazima utakuwa mchawi wewe, hao unaosema wasanii ndio waliokwenda extra mile kwenye maarifa ya Mungu. Yesu alisema huwezi kuwasha taa ukaiweka uvunguni. Wanaokwenda on TV wana confidence na Mungu wao na wanatimiza ile task ya kuwafikia watu wengi kwa injili maana siku zimeisha.

I am a bit disappointed with the likes of TAGs for not going on TV during these last days. People do not understand that the ultimate purpose ya kwenda on TV sio kuponya wagonjwa bali kuhubiri injili, uponyaji ni demonstration of the power of the holy spirit, yaani roho mtakatifu anadhihirisha yale maneno yaliyohubiriwa kwa kuponya wagonjwa.

It is very sad kwamba hizo dhihaka hamuwafanyii akina Nyaga au Malisa bali mnamfanyia aliyewatuma, ambaye ni Yesu.
 
Back
Top Bottom