Kuhusu Mkataba na DP World: Serikali sasa ikutane na viongozi wa Vyama vya Upinzani

Dr Restart

JF-Expert Member
Jul 15, 2021
3,295
17,137
Wasalaam Wakuu.

Baada ya Bunge kuunga Mkono azimio la Serikali kuingia Mkataba na Kampuni ya DP World, mengi yamekuwa yakisemwa.


Leo tar 12 Juni 2023, Waziri Prof Mbarawa alikutana na viongozi wa dini mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu juu ya mkataba wenyewe. Na kuondoa sintofahamu na hofu iliyotanda ndani ya jamii juu ya tetesi za bandari yetu kuuzwa.

Kwanza nikiri ni jambo zuri na lenye afya kutoa elimu juu ya swala husika. Viongozi hao walipata nafasi ya kuzungumza na kutoa maoni yao. Na pengine serikali inaweza kuyafanyia kazi.

Lakini, serikali imekosea haswa katika kuchagua ni ndege yupi wa kuanza naye. Hii ni kwa sababu, hoja hizo ziliibuliwa na Wanaharakati pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani haswa CHADEMA, CUF na ACT.

Ingelikuwa vema serikali ikaanza nao na kuwasikiliza kisha baadae kufata viongozi wa dini.

Hii ni kwa sababu jambo lenyewe linaonekana kujaa siasa za hapa na pale. Na nyumba za ibada, mara nyingi tumekuwa tukiusia mambo ya kisiasa yasichanganywe na mambo ya imani za watu.

Viongozi wa vyama vya upinzani lilikuwa kundi muhimu sana katika kukutana na kuwasikiliza maoni kabla ya serikali kuingia kwenye mikataba hiyo hivi karibuni. Kwa kuwa nchi ni yetu sote, si vema kuwabagua kwa minajili ya vyama vyao na msimamo wao.

Lakini, bado serikali haijachelewa katika hilo. Hima watoe mualiko kwa viongozi wa vyama vyote vya kisiasa kufika na kufahamu kwa undani haswa kilichomo katika mikataba hiyo. Wapokee maoni yote na iahidi kuichambua na kuchukua yale yote yenye nia njema kwa mustakabali wa taifa letu.

Viongozi hao pekee ndiyo wenye nafasi kubwa ya kuondoa maruweruwe yaliyojaa ndani ya jamii kwa sasa. Na sehemu kubwa ya Watanzania inaonekana kuegama upande huo ambao viongozi wa upinzani wanauzungumzia.

Nawasilisha hoja mezani.
 
Back
Top Bottom