Kuhusu kumsamehe Halima Mdee, napingana na John Heche

Kuhusu kumsamehe Halima Mdee, napingana na John Heche

Kiukweli Mdee ni shujaa wangu, ni chuma cha pua!, ili kukilinda chama kisiparaganyike, ameamua kufa kizungu na tai shingoni kwa kutomtaja ila wenye akili wote wanamjua na ndio maana watamsamehe Mdee bila kumtaja mchawi wao!. Mdee is a jewel, kwa Chadema kuendelea kumfukuza, it has everything to loose and nothing to gain kwasababu Chadema haina mtu wa calibre ya Halima. "Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
P
Cdm sio CUF ya Maalim Seif alipoondoka na CUF ikafubaa. waliondoka akina Zito, Kitila, na kipenzi cha wanacdm Dr. Slaa, mbona cdm haijafa, na chaguzi zinazidi kuporwa kimachomacho kwa ccm kuwashindwa cdm? Hadi Slaa karudi mwenyewe juzi kwa aibu.

Kipi kinachokufanya utake kuonyesha Mdee ni zaidi ya hao? Kwa kukusaidia tu cdm kwa sasa ni zaidi ya chama cha siasa, ni movement, ndio maana unaona hata walipoondoka walioenda kuunga juhudi wakati wa Magufuli, bado cdm ilibaki na ushawishi. Hata Magufuli kuamua kupora chaguzi za 2019 na 2020, ni katika kuficha ukweli halisi wa nguvu ya cdm. Uchaguzi wa juzi 2025 nguvu na mauaji yote ilikuwa ni kupambana na ushawishi halisi wa cdm. Hata Chauma ilitumika kutaka kuimaliza cdm imeshindikana. Huu ni ukweli ambao wanaccm wengi hamtaki ufahamike, lakini kwa uelewa wa kizazi hiki ukweli huu imekuwa ngumu kuuficha.
 
Unaweza ukawa sahihi mkuu kibinafsi TU

lakini kwenye siasa hakuna rafiki au adui wa kudumu

Suala kubwa la chama ni kuongeza umakini sana kwenye mchakato wake wa kupata viongozi

Kama atarudi abaki kuwa mwanachama wa kawaida Kwa muda Fulani huku chama kikiangalia mwenendo wake

Kwa mwanachama mpya haswa anayehamia apewe muda wa kutosha KUJIDHIRISHA ndani ya mfumo wa chama
Kwa hili napingana na wewe. Huyu mtu aliongoza genge lililohujumu chama. Na lengo lake lilikuwa ni kukiua chama. Sema hakufanikiwa.

Walipeleka chama mahakamani na siyo kwa lengo la kupata haki bali kukiumiza chama kwenye rasilimali fedha. Pia kukipotezea muda wa kushughikia mambo muhimu ya chama. Matokeo yake chama kilielekeza nguvu nyingi mahakamani kwa mambo ya kipuuzi yaliyoongozwa na mtu yule yaani kiongozi wa genge lile.

Hata akirudi leo au kesho hawezi tena kuwa yule wa mwanzo. Wanachama na wafuasi wake wamepoteza imani kwake. No one will trust her any more. Kwa kifupi hana mvuto tena kwa chama.

Kama bado anapenda siasa basi aende kule alipo mwenzake wakapige majungu yao huko yaani akaongezee nguvu ya uchawa huko.
 
Kati ya majitu majinga kabisa ya Chadema ni wewe!, mimi sio Chadema, ila kwa vile ni mwandishi wa habari, nina some access ya intel!
  1. Barua iliyowapeleka Bungeni ni bonafide genuine letter na imesainiwa na kigogo wa Chadema ambaye ni officer bearer, Mdee kosa lake ni nini?!.
  2. Niliwashauri kitu toka ile day 1, CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
  3. Mdee ni Mwenyekiti wa BAWACHA, mamlake ya nidhamu ni Baraza Kuu, mamlaka ya rufaa ni mkutano mkuu, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka kumfukuza?! Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?
  4. Kwa taarifa yako, labda ni wewe tuu ndio hujui, JJMnyika na Heche wameisha jua Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?
  5. Katika wanawake wote wa Chadema waliopo, hakuna wa calibre ya Mdee, Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu
Kuna vitu ni vya Chadema wenyewe insider tuu, majitu majinga majinga kama hili, hayavijui!, Mdee kosa lake ni nini mpaka asiweze kusamehewa!, kama ni Chadema waliotangaza ile list ya mafisadi pale Mwembe Yanga na wakamsamehe kubwa lao, na kumfanya mgombea wao, wanashindwaje kumsamehe Mdee?!

Hebu acha hizo!, na kwa taarifa yako, Mdee akisamehewa, 2030 analitwaa jimbo la Kawe kama amelikota kwasababu mimi namjua mgombea wa CCM kawe 2030 ni mwanamke!, Trends Reading: Japo Rais wa 2030 Namjua, Simtaji ili Kumlinda!. Be The First to Know Good News Kawe-2030, MB.ni Mwanamke!, Kawe Itapaa kwa Maendeleo!

P.
Mkuu, mbona umefikisha ujumbe kwa shari Sana?
 
Kwa hili napingana na wewe. Huyu mtu aliongoza genge lililohujumu chama. Na lengo lake lilikuwa ni kukiua chama. Sema hakufanikiwa.
Kukiua vipi? Mbona chama kiliendelea vizuri na shughuli zake wakati wao ni wabunge?
Walipeleka chama mahakamani na siyo kwa lengo la kupata haki bali kukiumiza chama kwenye rasilimali fedha.
Walikipeleka Chama mahakamani kwa sababu waliamini kuwa walionewa walipofukuzwa chamani. Chama chenyewe ndio kilikataa kupokea ruzuku ambayo ilikuwa stahili yake. Halima na wenzake hawakuwa na ubavu wa kukiathiri chama kipesa.
Pia kukipotezea muda wa kushughikia mambo muhimu ya chama. Matokeo yake chama kilielekeza nguvu nyingi mahakamani kwa mambo ya kipuuzi yaliyoongozwa na mtu yule yaani kiongozi wa genge lile.
Kwani huko Mahakamani walikuwa wanaenda kila siku kusikiliza kesi ya wakina Halima?
Hata akirudi leo au kesho hawezi tena kuwa yule wa mwanzo. Wanachama na wafuasi wake wamepoteza imani kwake. No one will trust her any more. Kwa kifupi hana mvuto tena kwa chama.
Sawa. Hata yeye anajua kuwa haitakuwa rahisi kurudisha imani ya wanachama wengi. Ila ukweli ni kuwa huko chini bado kuna watu wana imani nae. Inawezekana pia kuna watu wana hofia kuwa akirudi atawafunika.
Kama bado anapenda siasa basi aende kule alipo mwenzake wakapige majungu yao huko yaani akaongezeko nguvu ya uchawa huko.
Huo ni ushauri mzuri kabisa. Hata hivyo kumbuka wengi waliohamia Chaumma walikuwa mstari wa mbele katika kufukuzwa kwake.

Amandla...
 
Maslahi ya Mdee kuwa ndani ya chama ni makubwa sana kuliko akiwa nje hasa akikataliwa barua yake ya kuomba kurudi ina hasara usiyoweza kuiona moja kwa moja.
Faida yake ni.
1. Wapo wanachama tutavuna kupitia yeye japo hakuna atakaewaona direct. Kuimarisha chama.
2. Kuna faida ya kuwatetemesha upande wa pili,ndio watapoteana zaidi.
3. Mdee ni aset pia ana msimamo ni miongoni mwa wanawake Tz wenye power ya uwasirishaji wa hoja. (Hiyo pia itaifanya CHADEMA kuwa na watu pande zote,kufanya kuogopwa upande wa pili)
=Kwenye duru za kisiasa lazima chama kiwe na watu wengi wenye kuogopwa pindi anapotoa matamko fulani.

Inaonekana bado kuna maeneo ambayo hatujayaelewa kikamilifu, na ningependa kuhakikisha tunatumia muda wetu vizuri na kwa ufanisi zaidi.
Kama kuna vitu huvijui, kubali kuna vitu vya ndani ya Chadema wewe huvijui!. Kwani barua iliyowapeleka Bungeni wewe umeiona?. Nani kakuambia imesainiwa na Mbowe?.
Naomba uniamini mimi, wabunge wale wameteuliwa kwa barua bonafide genuine from office bearers wa Chadema, hakuna fojari yoyote ndio maana Chadema hawakuripoti popote kuwa kuna jinai yoyote!,
Mimi sikujui wewe ni nani huko Chadema lakini mimi nazungumza face to face na mabosi wako Lissu , Heche na JJ Mnyika. Hili nimelizungumza kwa kirefu na JJ Mnyika, karibu umsikie J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake
P
Barua halisi ya Chadema ni ipi, ni kikao gani cha kamati kuu kiliteua Wabunge wa viti Maalum, kilifanyika wapi na lini?

Kudhani unajua kila kitu ni kichaa, jiangalie Mzee, hakuna mjinga hapa jf unayeweza kumpiga fix kibwege
 
Erythrocyte Katiba ya CHADEMA inasemaje kuhusu mwanachama aliyepoteza uanachama na anataka kurudi?

Kama Katiba ina utaratibu, ufuatwe. Nadhani kuna kuomba na kujadiliwa katika vikao vya kichama.

Ikifika katika vikao ndipo maswali na hoja zinapojadiliwa kwa uzito wake, mwombaji akihojiwa na kujitetea
Kuna mawili, akubaliwe arudi kundini au akataliwe kwa vikao halali na kwa ''natural justice''

Mkianza utaratibu wa hisia ''emotion'' na kangaroo court mtaishia kuparurana bila sababu.

Wenje alijulikana msaliti akipeleka mabunda ya pesa ya kijana wetu kwa TL, lakini alipochaguliwa aliruhusiwa katika vikao kwasababu katiba inasema hivyo. Kilichomuondoa CHADEMA ni guilty conscience ! siyo hasira za watu
Kama umenielewa vizuri, sijazuia chochote nilichosema ni kwamba nitashawishi Wajumbe akataliwe na ninazo sababu 10 za kusisitiza hilo
 
Inaonekana bado kuna maeneo ambayo hatujayaelewa kikamilifu, na ningependa kuhakikisha tunatumia muda wetu vizuri na kwa ufanisi zaidi.

Barua halisi ya Chadema ni ipi, ni kikao gani cha kamati kuu kiliteua Wabunge wa viti Maalum, kilifanyika wapi na lini?

Kudhani unajua kila kitu ni kichaa, jiangalie Mzee, hakuna mjinga hapa jf unayeweza kumpiga fix kibwege
Mimi nawashangaa watu wanaosema wakina Halima walikuwa na baraka za kimaandishi zakiongozi au viongozi wa Chadema. Kwa jinsi Marehemu Ndugai alivyokuwa hampendi Mbowe asingekalia barua yeyote ambayo inaonyesha unafik wa Mbowe au Chadema. Inawezekana kuna forgery ambayo walitaka kuitumia lakini wakagundua mapema kuwa ingewalipukia. Kwangu mimi huu uongo ni sawa na ule wa kusema Mbowe alikuwa anatumia pesa za Abduli kujaribu kumhonga Lissu. Zote hizi ni majaribio ya kuivuruga Chadema. Zote ni uongo mtupu. Kinachonisikitisha ni kuwa Chadema inaingia kirahisi katika mtego wanaowekewa na CCM.

Amandla...
 
Anasagana na Kalamu
Samia mhalifu na kalamu ni watu wasioweza kuhusiana kwa njia yoyote ile. Hata mafuta na maji vinaweza kuchanganywa vikawa pamoja, kama 'cream' za kujipaka' lakini siyo mtu mwovu na laghai kama Samia kuwa karibu kwa njia yoyote ile na kalamu

Kalamu hawezi kuwa karibu na shetani.
 
kumchukulia hatuna Mimi nawashangaa watu wanaosema wakina Halima walikuwa na baraka za kimaandishi zakiongozi au viongozi wa Chadema. Kwa jinsi Marehemu Ndugai alivyokuwa hampendi Mbowe asingekalia barua yeyote ambayo inaonyesha unafik wa Mbowe au Chadema. Inawezekana kuna forgery ambayo walitaka kuitumia lakini wakagundua mapema kuwa ingewalipukia. Kwangu mimi huu uongo ni sawa na ule wa kusema Mbowe alikuwa anatumia pesa za Abduli kujaribu kumhonga Lissu. Zote hizi ni majaribio ya kuivuruga Chadema. Zote ni uongo mtupu. Kinachonisikitisha ni kuwa Chadema inaingia kirahisi katika mtego wanaowekewa na CCM.

Amandla...

Pascal Mayalla ndiye anayesambaza huo upumbavu humu JF.
 
Kati ya majitu majinga kabisa ya Chadema ni wewe!, mimi sio Chadema, ila kwa vile ni mwandishi wa habari, nina some access ya intel!
  1. Barua iliyowapeleka Bungeni ni bonafide genuine letter na imesainiwa na kigogo wa Chadema ambaye ni officer bearer, Mdee kosa lake ni nini?!.
  2. Niliwashauri kitu toka ile day 1, CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
  3. Mdee ni Mwenyekiti wa BAWACHA, mamlake ya nidhamu ni Baraza Kuu, mamlaka ya rufaa ni mkutano mkuu, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka kumfukuza?! Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?
  4. Kwa taarifa yako, labda ni wewe tuu ndio hujui, JJMnyika na Heche wameisha jua Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?
  5. Katika wanawake wote wa Chadema waliopo, hakuna wa calibre ya Mdee, Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu
Kuna vitu ni vya Chadema wenyewe insider tuu, majitu majinga majinga kama hili, hayavijui!, Mdee kosa lake ni nini mpaka asiweze kusamehewa!, kama ni Chadema waliotangaza ile list ya mafisadi pale Mwembe Yanga na wakamsamehe kubwa lao, na kumfanya mgombea wao, wanashindwaje kumsamehe Mdee?!

Hebu acha hizo!, na kwa taarifa yako, Mdee akisamehewa, 2030 analitwaa jimbo la Kawe kama amelikota kwasababu mimi namjua mgombea wa CCM kawe 2030 ni mwanamke!, Trends Reading: Japo Rais wa 2030 Namjua, Simtaji ili Kumlinda!. Be The First to Know Good News Kawe-2030, MB.ni Mwanamke!, Kawe Itapaa kwa Maendeleo!

P.
Leo umetumia lugha ngumu sana braza!
 
Huyu hawezi kuruhusiwa kurudi CHADEMA na nitafanya kampeni Maalum kwenye Kamati Kuu kuhakikisha harejeshwi

Halima ndio nguzo kuu ya Covid 19, ndio mpanga njama mkuu akishirikiana na Usalama wa Taifa na Job Ndugai

Amesababisha usumbufu na maumivu makubwa mno kwa Chama, hatakiwi kabisa na nitapambana kuzuia (Nina ushawishi) na nyinyi mnafahamu

Ninazo sababu 10 za kutetea hoja yangu nitazitoa kwenye vikao haiwezekani kufuga majini ndani ya chama, hii itavunja moyo wengi, ni kweli CHAMA ni watu lakini Usaliti wa Mdee hauvumiliki

Kama unampenda mtu kutokana na sura yake basi nenda kanywe naye chai-JK NYERERE
Acheni tabia za ajabu... Chama chochote cha siasa mtaji wake watu. Msiwatenge wala kuwabagua watu! Waacheni wanaotaka kuja waje muunganishe nguvu mfike vijijini kule ambako ndiko kuna wapiga kura!
Chama cha siasa ni daraja! Wakaribisheni watu kwa wingi tuvuke hapa tulipo!
 
Kama umenielewa vizuri, sijazuia chochote nilichosema ni kwamba nitashawishi Wajumbe akataliwe na ninazo sababu 10 za kusisitiza hilo
Una kila haki ya kuwashawishi watu kumkataa Halima. Ni wajibu wako. Itaonyesha maturity ya Chadema kama watakusiliza na wataendelea kukuheshimu hata kama hawakubaliani nawe.

Amandla...
 
Back
Top Bottom