Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,683
- 6,689
Mdee nilikuwa namkubali sana na niliweka wazi hilo siku nyingi. Kuna siku nilikutana naye Wizara ya Ardhi, isingekuwa mshituko wa kumuona ghafla uso kwa uso, ningeweza kumuomba uchumba pale pale.
Ila maamuzi yake ya kudhamiria kabisa yamekosea sana harakati za mageuzi. Binafsi nisingependa kuona akipewa tena uongozi wowote ndani ya CHADEMA. Kama ni kuwa mwanachana, nadhani anaweza kuruhusiwa (ingawa nalo nina mashaka nalo) ila si zaidi ya hapo.
Hawa walioikimbia harakati za mageuzi katika nyakati ngumu ni wa kuwatumia kama mfano maana moja ya mbinu ambayo CCM wameitumia sana kukatisha tamaa harakati hizo ni kwa kuwachomoa watu kutoka upinzani na kuwapa vifursa na zile kampeni uchwara za kuunga mkono juhudi. Inabidi kukata huo mzizi na kuonyesha kuwa hakuna mtu mkubwa zaidi ya harakati za mageuzi. Ukizingua watu wanakuweka pembeni wanakusahau.