Halima ndio nguzo kuu ya Covid 19, ndio mpanga njama mkuu akishirikiana na Usalama wa Taifa na Job Ndugai
Amesababisha usumbufu na maumivu makubwa mno kwa Chama, hatakiwi kabisa na nitapambana kuzuia (Nina
Samahani.
Sitaki nionekane kwa sababu yoyote kuwa mtetezi wa hujuma zilizofanywa juu ya chama, na Halima akiwa ni miongoni mwa watu hao.
Uhusika wa kuwa "mpanga njama mkuu", hili ukilielezea kwa sisi tusiokuwa na ufahamu, pengine tutashawishika kuungana na wewe.
Nakumbuka ulikuwa radhi kukaa kimya wakati ule wa mchuano wa uchaguzi; na wengine tuliodhani "mpanga njama" mkuu na aliyesababisha hao mabinti kujidhalilisha kama walivyofanya anajulikana; na ulikuwa tayari kumkubali kama angeibuka na ushindi!
Hii inatuchanganya sana tunaotazama toka nje ya chama.
Halima, hawezi kujivua uharibifu mkubwa aliochangia kukiingiza chama matatani wakati huo; hadi ukomo wa ubunge wao.
Halima kama bado anayo dhamira ya kuwa ndani ya chama hicho, inabidi ajieleze kikamilifu juu ya uhusika wake na kwa nini ililazimu iwe hivyo.
Halima hawezi kurudishwa ndani ya chama bila kutubu; na hawezi kutegemea kupokelewa kana kwamba hakuna lililotokea.
Asiwe na matarajio ya kurudi na kupewa uongozi moja kwa moja ndani ya chama hicho; ni muhimu aonyeshe dhamira ya kuwa mwanaCHADEMA, na kukitumikia chama kama mwanachama yeyote, bila ya kukimbilia kwenye uongozi tena.
Halima tofauti na wenzake aliowaongoza, ameonyesha kuwa na moyo wa subira; pengine kutokana na kujjutia mchango wake wa kukiumiza chama.
Nitarudia tena, katika yale yaliyonisikitisha sana katika siasa za Tanzania. Moja ni huyu binti, ambaye niliamini kabisa kuwa alikuwa na 'commitment' isiyoyumbishwa kabisa juu ya chama chake.
Ni kitu gani kilichomfanya huyu binti akengeuke kiasi kile? Kumuheshimu kiongozi wake mkuu aliyeamrisha mpango mzima wa kuwaingiza hao mabinti Bungeni?
Halima apewe fursa ya kujirudi, na awe chini ya uangalizi wa chama kabla ya kupewa wadhifa wa uongozi ndani ya chama.
Hayo unayoyajuwa wewe, mimi siyajui; kwa hiyo hadi hapo utakapoweka wazi hayo, sasa hivi sitakubaliana na msimamo wako.