Kuhusu kumsamehe Halima Mdee, napingana na John Heche

Kuhusu kumsamehe Halima Mdee, napingana na John Heche

Upo sahihi sana. Na nakuunga mkono katika msimamo wako japo tuna nawazo tofauti.

Siasa za CHADEMA kupindi cha Nbowe, nyingi zilijengwa juu ya Ulaghai. Bado naamini hata Halima Mdee aliingizwa Mkenge na Viongozi wake.

Kama Viongozi walikuwa na uwezo wa kuelekeza watu wajiunge CCM, Kama mtu ameiachia CHADEMA maumivu halafu baada ya mwezi anashiriki kwenye Birthday ya Kiongozi wa chama na wqnqgonga glasi.

Kama viongozi wanakubali michango ya CCM na inawapa hela ya Ukumbi wa kufanyia mikutano ya baraza kuu wanakubali, Halima ni nani.

Halima alikuwa chini ya Uongozi na alitii uongozi ndo maana akafanya alichofanya. Kumbuka Unakuwa kwenye hatari zaidi kama ukiwa sahihi kwenye Uongozi unaoenda kinyume. Alilinda uhai wake hakutaka kufa kama Mzee Kibao

Kumbuka Uongozi ulitutia ujinga Watanzania kwa kusema hawawezi kwenda mahakama kwani mahakama hazitendi haki kuumbe waliogopa ukweli utafichuka. Mbona mahakama imewaondoa chadema kwenye kifungo? Ingekuwa awamu ilopita wangesema tusikqte rufaa mahakama hazitendi haki.

Hata hivyo wote walioshiriki mchezo huo mchafu hawapo tena chadema wala hawaendi kumtembelea Lissu mahabusu.

Haliama alipewa masharti ili kurudi CHADEMA.

1. Ataje ni nani alisaini barua zao.
2. Ni nani alipeleka barua za Viti Maalum kwa msajili wq vyama vya siasa.
3. Waliowasapoti walikuwa wanawapa bei gani.

Hata hivyo hakuna chama kinakataa mwanachama mpya. Halima atakuwa mpya kwani alishafukuzwa.. Chadema hakuna sheria ya mtu akifukuzwa haruhusiwi kujiunga na chadema tena.

Chama ni watu..

Kama mkiristo nimefundishwa kusamehe wote waliotubu. Atuambie mbinu walizotumia iili tusiumizwe tena pia itasaidia kuziba mianya kwenye katiba ili mambo kama hayo yasitokee tena
Naunga Mkono hoja yako.
 
Mbona dkt,Slaa amerudi hatukuona povu jingi kama kwa Halima?CHADEMA ya Sasa siyo ya wajinga.Lakini Halima anaweza kuwa kirusi kibaya akiruhusiwa kurudi CHADEMA
 
Halima alishaonyesha maslahi kwanza, kipindi chote akiwa bungeni alihusika kuunga mkono juhudi, huwezi kuwasamehe kabla yakuweka ukweli wazi.
 
Chawa wa Mbowe ila yuko Chadema!
Kuwa chadema si tiketi ya ktokuwa chawa wa mtu. Kuwa chadema ni pamoja na kuunga mkono maamuzi ya chama hata kama hukubaliani nayo. Otherwise jiunge na chama unachoamini kinakubaliana na wewe. Unaweza kuwa na mawazo binafsi na ushauri bila kudharau misimamo ya chama iliyokubaliwa na wengi. Ndo Demokrasia
 
Halima Mdee namkubali sana, nilimpigia kura 2010 na 2015. Amefanya mazuri 99 baya ni 1 tu asamehewe. Wasiwasi wangu ni ule urafiki wake na Esther Bulaya unanipa shaka.
Urafiki wa Halima na Ester hauhusiani na siasa bali uko kifaragha.
Swali liwe, je wanaweza kufichana habari zozote? I doubt it.
IMG_20260416_130400.jpg
IMG_20260416_130418.jpg
IMG_20260416_130435.jpg
IMG_20260416_130453.jpg
IMG_20260416_130509.jpg
 
Kuwa chadema si tiketi ya ktokuwa chawa wa mtu. Kuwa chadema ni pamoja na kuunga mkono maamuzi ya chama hata kama hukubaliani nayo. Otherwise jiunge na chama unachoamini kinakubaliana na wewe. Unaweza kuwa na mawazo binafsi na ushauri bila kudharau misimamo ya chama iliyokubaliwa na wengi. Ndo Demokrasia
Bado sielewi wataka nini? Ukisoma Uzi wangu nimesema nitashawishi wajumbe, sita dictate hili jambo, zaidi nimesema Nina ushawishi ndani ya kamati kuu n.a. nitautumia
 
Mungu mwenyewe anasamehe itakuwa Chadema? Kama atafuata taratibu asamehemewe
Chadema siyo sawa na Mungu, Mungu hashindani na yeyote, chadema inapambana vita vikali na majitu onevu yasiyojali haki.Aliyewawezesha Wakoma kuongoza ushindi wa wa Israeli dhidi ya Washamu ni nani? DAUDI aliwezaje kumuua Golliath tena kwa jiwe tuu?
 
Huyu hawezi kuruhusiwa kurudi CHADEMA na nitafanya kampeni Maalum kwenye Kamati Kuu kuhakikisha harejeshwi

Halima ndio nguzo kuu ya Covid 19, ndio mpanga njama mkuu akishirikiana na Usalama wa Taifa na Job Ndugai

Amesababisha usumbufu na maumivu makubwa mno kwa Chama, hatakiwi kabisa na nitapambana kuzuia (Nina ushawishi) na nyinyi mnafahamu

Ninazo sababu 10 za kutetea hoja yangu nitazitoa kwenye vikao haiwezekani kufuga majini ndani ya chama, hii itavunja moyo wengi, ni kweli CHAMA ni watu lakini Usaliti wa Mdee hauvumiliki

Kama unampenda mtu kutokana na sura yake basi nenda kanywe naye chai-JK NYERERE
Pascal Mayalla
 
Watu wengine bwana, huyu Erythrocyte si alikuwa upande wa Mbowe na akawa anampiga vita Lissu wakati wa kinyang'anyoro! Kila zama na masahibu yake, na Uzuri ni kuwa Mdee ameyaona makosa yake, akirudi naamini anaweza kuwa mwanachama bora. Ndiyo hatua ya ukomavu katika siasa.
Sahihi kabisa. Ndio maana Heche ameyaona hayo amemruhusu Mdee kuandika barua ya kuomba. Heche ni bonge moja la kiongozi anajua kuendana na wakati
 
Huyu hawezi kuruhusiwa kurudi CHADEMA na nitafanya kampeni Maalum kwenye Kamati Kuu kuhakikisha harejeshwi

Halima ndio nguzo kuu ya Covid 19, ndio mpanga njama mkuu akishirikiana na Usalama wa Taifa na Job Ndugai

Amesababisha usumbufu na maumivu makubwa mno kwa Chama, hatakiwi kabisa na nitapambana kuzuia (Nina ushawishi) na nyinyi mnafahamu

Ninazo sababu 10 za kutetea hoja yangu nitazitoa kwenye vikao haiwezekani kufuga majini ndani ya chama, hii itavunja moyo wengi, ni kweli CHAMA ni watu lakini Usaliti wa Mdee hauvumiliki

Kama unampenda mtu kutokana na sura yake basi nenda kanywe naye chai-JK NYERERE
Kuna watu wamefanya mabaya kuliko Halima Mdee na mkawasemehe. Watu waliandika vitabu kuishutumu Chadema kuhusika na uovu mkubwa mkawasamehe. Pamoja na kosa la Covid 19 lakini hawakusimama hata siku moja kuichafua Chadema. Nadhani huu ni wakati wa kusameheana pande zote. Chadema nayo iombe radhi kwa wale ambao haikuwatendea haki.

Amandla....
 
Back
Top Bottom