Ni jambo jema kutumia nishati isiyochafua mazingira na kuumiza watumiaji. Tatizo la wanasiasa wetu kila wanachokipigia debe nyuma yake wanasukumwa na faida binafsi.
Watu wanahoji yafuatayo:
1. Kwanini nishati safi suala la matumizi ya gesi linasisitizwa zaidi huku umeme ukiachwa?
2. Kwanini mitungi ya gesi imetolewa bure baadhi ya maeneo?
3. Kwanini watu walitakiwa kutoa number za NIDA ili kupewa mitungi? Je kuna uhusiano na anayosema Polepole?
4. Kwanini miradi ya usambazaji wa mitandao ya mabomba ya gesi majumbani imesuasua?
5. Kama viongozi wanachukia kweli uchafuzi wa mazingira kupitia nishati chafu kwanini uchimbaji wa makaa ya mawe mikoa ya Kusini umeshika kasi na makaa hayo kuuzwa Kenya kwa maelfu ya tani.
6. Kwanini mradi wa kuweka gesi asilia inayochimbwa Tanzania unasuasua kwa miaka mingi sasa?
7. Juzi tajiri mmoja mkubwa wa biashara ya gesi amechangia chama Shs 10 bilioni. Hii inadhihirisha mafungamano makubwa kati ya viongozi wa siasa na wafanyabiashara wa gesi.
Maswali haya na mengine yanadhihirisha uwezekano wa kampeni ya nishati safi kwa wote kuwa mradi wa baadhi ya viongozi wenye malengo binafsi.