Kufananisha Dar es Salaam na Arusha

Kufananisha Dar es Salaam na Arusha

We sema tu umesha-miss kwenu Daslam bafu linaishia kifuani ukioga kichwa kinaonekana nje, mvua ikinyesha unapanda juu ya bati , Tv na masufuria unazikuta mtoni
Mbona hata huku kwenu mambo ndio hayohayo bro....nyie watu wa Arusha wajanja sana huko Dar mnajifanyaga huku hakuna hizo saga nineshangaa sana mambo niiyoyakuta huku😂
 
Kwema jamani

Jana na leo niko viunga vya jiji la Arusha,Yule aliyeubatiza huu mji Geneva of Africa atafutwe,akamatwe,achapwe bakora 13,ANYONGWE!....THE CITY IS OVERLY HYPED samahani washkaji zangu wooote wa A- town mkiongozwa na big Glenn .
Wakatabahu
Jo.
We hasidi aliyeita Arusha Geneva ya Africa ni Bill Clinton nenda mfuate Marekani. Umetoka na ushamba ulikotoka Arusha utaielewa wapi. Rudi huko kwenu ushambani.
 
Halafu mbona vijana wengi wana makovu ya visu halafu wanaongea lugha siilewi kuna nini huku jamani?
Ndiyo wajanja wa A town hao, Vipi lakin Vijana wa Dar na Vijana wa uko Arusha wapi kuna vijana Ma handsome boy ?
 
Nimeenda zangu arusha nikajichanganya kupiga misele ya hapa na pale saa 12 jioni mara nipo kwa morombo nikashangaa nyama choma pale na wale wamasaiii mishale ikasogea mara saa tatu na midakika hapo magetoni ni ngaramtoni

Basi dandia vigari vyao vile vidunchu kama kiberiti nikashuka posta ndio mwisho... oyaaa hiyo posta night sio kali lakini imeshakuwa dorooo, mjini kumetepeta raia ni wakuhesabu na usafiri kipengele boda boda zinapita hata hazina time na wewe, nilikanya mguu mpaka mianzini miksa mvua inanyesha, miksa kuloa miksa jogging. mianzia nakutana na mduanzia boda anataka buku 4. daah

Yani nili laani sana hiyo arusha. hakuna maajabu kabisa zaidi ya watoto wakike wazuri weupe wanapenda kusuka rasta ndeeefu
Chuga ikifika saa 3 hupati city bus, haha
Mji wa kisenge sana
 
Kama Arusha hujaipenda si urudi zako gongolamboto mkapakane majasho
Nlifika gongo la mboto kipindi cha mvua aloh hapafai unapita chini ya sgr maji + matope ndo maana watu wa dar wanachuki na arusha kwasababu wanaona hatuteseki kama wao😀
 
Watu sio wengi sana na pia wanafanya shughuli tofauti ni tofauti na daslm wengi ni kutoka asubuhi na kurudi wakimaliza kazi Arusha saa hizi mtu anaenda/kurudi Porini.
Watu wanaojifanya wanaringa na dar ni watu waliotoka mikoani wakaenda dar ukubwani kwao wanaona dar kama Paris 😀 si ajabu anaona foleni ni maendeleo
 
Kusema ukweli wazawa wa Arusha ni washamba na limbukeni sana ila Arusha kama Arusha imekaa poa sana, kama umeenda Kwa lengo la vacation utaenjoy sana ila kama ni mpitaji then utapachoka haraka sana
Umekutana wewe na washamba ambao umewaona
Watu wa arusha wangekua limbukeni wasingekua wanapokea wageni namna hyo
Wageni wote wanaotoka nje kuja tz wanaipa arusha marks kubwa kwa hospitality
Shida yenu mnajuaga kile kikundi cha wadudu ndio taswira ya Arusha fika Arusha hata wewe utawatafuta walipo
Nmezunguka nchi yote hii hamna sehemu utapata huduma bora na customer care kama Arusha
Hata watu wakitaka kufungua sehemu classic mikoa mingine watatafuta wahudumu kutoka Arusha kwasababu wao tayari wanaexposure ya kuhudumia wageni
Fanya research
 
Kiukweli kabisa Arusha kwa Dar bado sana, na huu msimu ndio inazidi kuwa bado sana tena sana.

Nimekulia Arusha, nipo Arusha ila huu mji vijana (wa 2000s) ni washamba sana na hodari kwa mambo ya kijinga.
 
Back
Top Bottom