Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: JamiiForums inatambua mchango wa wanawake kwenye ulimwengu wa Digitali

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,204
5,032
Kuelekea siku ya wanawake Duniani, Jamii Forums inatambua umuhimu wa wanawake kushiriki katika sekta mbalimbali kwa kuwa wana uwezo na juhudi za kufanya kazi kwa ufanisi na inajivunia ufanisi na jitihada zinazooneshwa na wanawake katika kutimiza majukumu yao.

Mwanamke anapaswa kuaminiwa kupewa fursa na nafasi katika kila sekta kwani ana uwezo wa kuleta matokeo chanya. Iwapo ujuzi anaoapewe nafasi bila kubaguliwa bali sifa na vigezo ndio vimpe nafasi.
 
chanya. Iwapo ujuzi anao apewe nafasi bila kubaguliwa bali sifa na vigezo ndio vimpe nafasi.
Ni wakati wa kuwaamini katika kila sekta, dhana za zama za giza hazina nafasi katika ulimwengu huu teknolojia .
 
Sawa, lakini kwenye sekta ya ustawi wa familia wapunguze kuvuruga familia(sababu chanzo cha migogoro mingi ndani ya familia ni wao hata Biblia Methali 14: imeandika Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Wajitambue na kuishi majukumu yao wanapokuwa Wake na Mama wa familia, waache tabia za kutaka miliganisho isiyo na tija kwenye ustawi wa familia na jamii nzima ambayo zaidi zaidi huwa ndio chanzo cha migogoro na mivurugano kwenye familia na jamii.. Hakuna Ustawi wa familia Hakuna Ustawi wa jamii.
 
Kuelekea siku ya wanawake Duniani, Jamii Forums inatambua umuhimu wa wanawake kushiriki katika sekta mbalimbali kwa kuwa wana uwezo na juhudi za kufanya kazi kwa ufanisi na inajivunia ufanisi na jitihada zinazooneshwa na wanawake katika kutimiza majukumu yao.

Mwanamke anapaswa kuaminiwa kupewa fursa na nafasi katika kila sekta kwani ana uwezo wa kuleta matokeo chanya. Iwapo ujuzi anaoapewe nafasi bila kubaguliwa bali sifa na vigezo ndio vimpe nafasi.
Hivi hizi vitu zinamaana yeyote kweli au kufata mkumbo wa wanasiasa katika mambo yao lukuki ya kutengeneza headline lakini hayana Tija kwa mwananchi wa kawaida. Lini mwanamke hajaaminiwa na nani anatakiwa kumwamini???

Mie naona kama mfumo mwingine wa ubaguzi na kugawa watu ili watawaliwe kiurahisi, zamani ilikuwa watu wanabaguliwa kwa rangi, kabila na sasa jinsia.

Hivi dunia yenye usawa sawa kwa watu wote haiwezekani, humu JF jinsi mbona sio kigezo na tunaishi tu.
 
Back
Top Bottom