Happy Women's Day: Una ujumbe gani kwa wanawake leo Siku ya Wanawake Duniani?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu mpo salama?

SIKU YA WANAWAKE.jpg

Siku ya Kimataifa ya Wanawake tarehe 8 Machi, ni muhimu katika kutambua jitihada, harakati na mchango wa Wanawake Duniani kote

Tunasherekea mafanikio ya Wanawake katika nyanja mbalimbali za Maisha kama vile mafanikio binafsi, kihistoria, kiuchumi, kisayansi, kisiasa na kiutamaduni, pamoja na kuhamasisha juhudi za kuleta usawa wa kijinsia Duniani kote

Una dada, mama, shangazi, rafiki ama binti wanaokuzunguka katika mazingira yako, ambao naamimi wanamchango mkubwa katika kufikia hapo ulipo.

Leo katika Siku ya Wanawake una lipi la kuwaambia?
 
Maisha ni magumu! Kuolewa sio ticket ya kubweteka kuacha kufanya kazi kwa kisingizio cha mama wa nyumbani nalea watoto.

Unaweza kua mama wa nyumbani lakini ukafanya biashara hapohapo na kuingiza chochote kitu mfano; Kufungua duka la mahitaji ya nyumbani, kuuza mabarafu juice au ice cream, kuuza vitafunwa asubuhi, kuuza mkaa

Maisha ni magumu! Ili kuyalainisha inabidi kushirikiana na wakina baba kuweka chochote mezani.

Happy Women's Day!🤍💫
 
Siku ya Kimataifa ya Wanawake tarehe 8 Machi, ni muhimu katika kutambua jitihada, harakati na mchango wa Wanawake Duniani kote

Tunasherekea mafanikio ya Wanawake katika nyanja mbalimbali za Maisha kama vile mafanikio binafsi, kihistoria, kiuchumi, kisayansi, kisiasa na kiutamaduni, pamoja na kuhamasisha juhudi za kuleta usawa wa kijinsia Duniani kote
Kauli Mbiu Siku Ya Wanawake 2024 inalenga Kuchochea Ushirikishwaji wa wanawake katika jamii ili kuongeza kasi ya maendeleo

Nia ya kaulimbiu hii ni kumpa mwanamke thamani ili kuchochea maendeleo na kuihamasisha jamii kumshirikisha mwanamke katika maendeleo.

Je una ujumbe gani kwa Wanawake unaowafahamu (Mama, Mke, Mpenzi, Rafiki na Mtoto wa Kike)?
 
Hongera kwa kwao.

Ujumbe

Wajitahidi kuwekeza katika kushirikiana na sio kushindana.

Watu wawili wanoshirikiana wanaweza kupiga hatua kwa haraka kuliko watu miamoja wanoshindana

Wakizingatia hili wanawake wataishi maisha ya kupiga hatua Sana na sio Kama ilivyo sasa hivi wanashidana nani ni bora .

Be achiever ,be builder be smarter
 
Umenena vyema Mkuu
 
Maisha ni magumu! Kuolewa sio ticket ya kubweteka kuacha kufanya kazi kwa kisingizio cha mama wa nyumbani nalea watoto.

Unaweza kua mama wa nyumbani lakini ukafanya biashara hapohapo na kuingiza chochote kitu mfano; Kufungua duka la mahitaji ya nyumbani, kuuza mabarafu juice au ice cream, kuuza vitafunwa asubuhi, kuuza mkaa

Maisha ni magumu! Ili kuyalainisha inabidi kushirikiana na wakina baba kuweka chochote mezani.

Happy Women's Day!🤍💫
Kama umeolewa Njombe, Mufindi au Lushoto ndani ndani huko hayo mabarafu au ice cream utamuuzia nani mkuu🙅‍♂️
 
Back
Top Bottom