Kupata Katiba Mpya Tusipigane Kipumbavu (Tupeane Makavu):
Makamanda watukuka agenda ya kudai katiba mpya ni ya msingi mno. Hii ni kwa maslahi yetu leo na hata kwa watoto wa wajukuu zetu.
Agenda hii haipaswi kufanyiwa mzaha hata kidogo. Ikibidi hata kutiana bakora wenyewe kwa wenyewe ili kuifanikisha itakuwa ni sehemu ya wajibu uliotukuka katika kuipigania.
Katika agenda hii, ni muhimu tukaelewana:
1. Hatuwezi kuwa na adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu kwenye harakati hizi.
2. Lazima tuwe na mkakati unaoeleweka wa mapambano usioshindwa na usiojali nani anatuongoza kwa wakati gani.
3. Lazima tuwe na mkakati kamili wa kuwahami wahanga kama mashujaa wetu mstari wa mbele, magerezani au hata wakiwa wafu.
4. Lazima tuwe na mpango mkakati wa kuwahusisha washirika wengi kwa kadri inavyowezekana, shughuli ni watu.
5. Lazima wigo wa ushiriki upanuliwe kuhakikisha wote walio tayari kujihusisha kwa namna yoyote wanahusishwa kikamilifu katika harakati hizi.
6. Jitihada zote zifanyike kujenga maelewano mema na wengine hata ambao wanaweza kuwa ni mahasimu wetu leo.
7. Tuwekeze zaidi kwenye vinavyotuweka pamoja kuliko kwenye vinavyo tutenganisha.
8. Tuwakemee na kuwadhibiti wajumbe wetu wenye kutenda kupalilia matengano na mitafaruku isiyokuwa na tija.
9. Harakati hizi ziwe kwa manufaa ya umma na si binafsi katika mali, pesa au kisiasa.
Ni wazi kuwa anayepinga jitihada za kupata katiba mpya sasa anaweka kizingiti si kwetu tu, bali hata kwa watoto wa wajukuu zake mwenyewe.
Hapa tuna walalamikaji, wadaiwa (walalamikiwa) na wasiohusika. Kila mmoja na aijue au ajuzwe nafasi yake akapate kujitambua anaposimama.
Kwani pilipili mtu asizozila zimuwashe yeye namna gani?
Angalizo: Mwana mpotevu aliporudi nyumbani kwa baba yake, aliyekuwa mwana mwema alichukizwa kiasi cha kuondoka nyumbani moja kwa moja!
Makamanda tusipigane kijinga. Bila kuyajaza magereza haipo katiba mpya hapa!
Cc:
Cannabis