Katiba Mpya ihakikishe Zanzibar inatunza haki ya kutoa Rais wa JMT kwa kupokezena kama ilivyokuwa zamani kabla ya kuja kwa mfumo wa vyama vingi

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,227
5,950
Kwa vile mwenye mamlaka anaelekea kuanza kuruhusu mchakato wa katiba mpya akili yangu inaanza kuelekea kuwaza nini nipendekeze kiwe kwenye katiba mpya. Kwa sasa mapendekezo yangu ni haya machache

URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Kwa vile Tanzania ni muungano zilizo kuwa nchi mbili basi kuwe na fursa sawa kwa kupokezana kwa nafasi ya urais wa JMWT baada ya mhula wa pili kwisha wa rais anayeondoka bila kujali anatoka chama gani. Yaani kama nafasi ni ya Tanzania visiwani kila chama itabidi kipate mgombea wake wa urais kutoka Tanzania visiwani.

MSINGI
Stahiki za binadamu (maana mimi sipendi kutumia haki za binadamu) na sheria ya asili inaelekeza ni lazima kulinda stahiki za wachache na dhaifu inapokuja suala la kugawana fursa na raslimali. Katika mazingira ya vyama vingi na ushindani tunapoelekea yanatengenezwa mazingira ya kuwafanya watu kutoka Tanzania visiwani kupoteza stahiki yao ya kugombea urais.

UTUMISHI UMMA NA UAWAKILISHI KATIKA VYOMBO VYA DOLA
Katiba tuliyonayo inaweka ukomo wa mtu kudumu kwa nafasi ya urais. Hii iwe kwa watu wote isipokuwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na Taasisi za juu za elimu. Ukiwa mtumishi wa umma- mda wako ni miaka 10; mbunge miaka 10; diwani miaka 10; mwenyekiti wa mtaa miaka 10 nk nk .

Sula la mihula liguse pia Taasisi zote zitakazotokana na sheria zitakazotungwa kwa mjibu wa katiba mfano vyama vya siasa, Taasisi za kijamii nk.

MSINGI
Inaonekana sasa utumishi wa umma na nafsi za kuchaguliwa ni raslimali ajira ambayo ni stahiki ya kila mtu. Hatua za makusidi lazima zifanyike ili kuhakikisha kila mtu anapata na kufaidi.

KUUNDWA KWA BUNGE LA MABWANYENYE
Bunge la mabwanyenye linatoa nafasi ya kutumia raia wazoefu na wazeefu kutoa ushauri kwa serikali bila mihemuko kama ilivyo kwenye bunge la kawaida. Kila jambo litakalopitishwa na bunge la kawaida lazima lijadiliwe tena na bunge la mabwanyenye kabla ya kupelekwa kwa rais kusainiwa na kuwa sheria.

Hii itaondoa mihemuko ya uchama. Nafasi za bunge la ubwanyenye ziwe za kuomba na kusailiwa kwa njia ya uwazi na kisha kupigiwa kura na bunge la kawaida. Ukubwa wa bunge la mabwanyeyenye usizidi idadi ya mikoa na usifate ueneo wala ukanda- ufate weledi.
 
Moja ya kitu haitawezekana ni ukomo wa muda kwa wafanyakazi wa uma.
Ila mkuu naionea huruma hii Kodi tutakayo ichezea hapa maana mwisho wa siku bunge ndo litaenda kuamua kipi ni kipi na sio haya maoni ya wananchi
 
kwa nini isiwezekane? Ni suala la kuamaua tu- unakaa miaka 10 unalipwa pesheni unaenda kujiajiri; wengine wanaingia
 
Kwa vile mwenye mamlaka anaelekea kuanza kuruhusu mchakato wa katiba mpya akili yangu inaanza kuelekea kuwaza nini nipendekeze kiwe kwenye katiba mpya. Kwa sasa mapendekezo yangu ni haya machache

URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Kwa vile Tanzania ni muungano zilizo kuwa nchi mbili basi kuwe na fursa sawa kwa kupokezana kwa nafasi ya urais wa JMWT baada ya mhula wa pili kwisha wa rais anayeondoka bila kujali anatoka chama gani. Yaani kama nafasi ni ya Tanzania visiwani kila chama itabidi kipate mgombea wake wa urais kutoka Tanzania visiwani.

MSINGI
Stahiki za binadamu (maana mimi sipendi kutumia haki za binadamu) na sheria ya asili inaelekeza ni lazima kulinda stahiki za wachache na dhaifu inapokuja suala la kugawana fursa na raslimali. Katika mazingira ya vyama vingi na ushindani tunapoelekea yanatengenezwa mazingira ya kuwafanya watu kutoka Tanzania visiwani kupoteza stahiki yao ya kugombea urais.

UTUMISHI UMMA NA UAWAKILISHI KATIKA VYOMBO VYA DOLA
Katiba tuliyonayo inaweka ukomo wa mtu kudumu kwa nafasi ya urais. Hii iwe kwa watu wote isipokuwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na Taasisi za juu za elimu. Ukiwa mtumishi wa umma- mda wako ni miaka 10; mbunge miaka 10; diwani miaka 10; mwenyekiti wa mtaa miaka 10 nk nk .

Sula la mihula liguse pia Taasisi zote zitakazotokana na sheria zitakazotungwa kwa mjibu wa katiba mfano vyama vya siasa, Taasisi za kijamii nk.

MSINGI
Inaonekana sasa utumishi wa umma na nafsi za kuchaguliwa ni raslimali ajira ambayo ni stahiki ya kila mtu. Hatua za makusidi lazima zifanyike ili kuhakikisha kila mtu anapata na kufaidi.

KUUNDWA KWA BUNGE LA MABWANYENYE
Bunge la mabwanyenye linatoa nafasi ya kutumia raia wazoefu na wazeefu kutoa ushauri kwa serikali bila mihemuko kama ilivyo kwenye bunge la kawaida. Kila jambo litakalopitishwa na bunge la kawaida lazima lijadiliwe tena na bunge la mabwanyenye kabla ya kupelekwa kwa rais kusainiwa na kuwa sheria.

Hii itaondoa mihemuko ya uchama. Nafasi za bunge la ubwanyenye ziwe za kuomba na kusailiwa kwa njia ya uwazi na kisha kupigiwa kura na bunge la kawaida. Ukubwa wa bunge la mabwanyeyenye usizidi idadi ya mikoa na usifate ueneo wala ukanda- ufate weledi.
Hiyo ya kupokezana haikuwa imepangwa ilitokea tu.
Aliye kuwa ameandaliwa ni Sokoine
 
Siku nyingine uwe unaleta taarifa za kuaminika.
Baba na mama yake ni watanganyika huo uzanzibar ameutoa wapi huyu mzaliwa wa kivule pwani
Unaweza kutwambia wazazi wa baba na mama yake Samia walitoka wapi?
 
Yule kazaliwa kule by default ni mzanzibar haijalishi wazazi wake wametoka wapi.
Kwa hiyo haya yote uliyoleta yanahusiana nini na mada tunayojadili
Pili kwa maelezo ya Mzee mwinyi alienda mkuranga kujifunza dini kwa nduguze; wewe unasema alizaliwa mkuranga- unataka tukuamini
 
Alienda zanzibar kujifunza dini, mkuranga kuna nani wakumfundisha dini wewe juha!?
Utoke Zanzibar ukajifunze dini mkuranga tabla lasa wewe kumbe.
 
Soma kitabu cha Mwinyi na usichanganye kutukuuza uarabu kama wanavyofanya mapemba wengi na ujuzi wa dini ya uislam
 
Hicho kitabu hujasoma umehadithiwa ndio maana umesahau mwinyi kazaliwa mkuranga kaenda zanzibar kujifunza dini.
 
Kwa vile mwenye mamlaka anaelekea kuanza kuruhusu mchakato wa katiba mpya akili yangu inaanza kuelekea kuwaza nini nipendekeze kiwe kwenye katiba mpya. Kwa sasa mapendekezo yangu ni haya machache

URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Kwa vile Tanzania ni muungano zilizo kuwa nchi mbili basi kuwe na fursa sawa kwa kupokezana kwa nafasi ya urais wa JMWT baada ya mhula wa pili kwisha wa rais anayeondoka bila kujali anatoka chama gani. Yaani kama nafasi ni ya Tanzania visiwani kila chama itabidi kipate mgombea wake wa urais kutoka Tanzania visiwani.

MSINGI
Stahiki za binadamu (maana mimi sipendi kutumia haki za binadamu) na sheria ya asili inaelekeza ni lazima kulinda stahiki za wachache na dhaifu inapokuja suala la kugawana fursa na raslimali. Katika mazingira ya vyama vingi na ushindani tunapoelekea yanatengenezwa mazingira ya kuwafanya watu kutoka Tanzania visiwani kupoteza stahiki yao ya kugombea urais.

UTUMISHI UMMA NA UAWAKILISHI KATIKA VYOMBO VYA DOLA
Katiba tuliyonayo inaweka ukomo wa mtu kudumu kwa nafasi ya urais. Hii iwe kwa watu wote isipokuwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na Taasisi za juu za elimu. Ukiwa mtumishi wa umma- mda wako ni miaka 10; mbunge miaka 10; diwani miaka 10; mwenyekiti wa mtaa miaka 10 nk nk .

Sula la mihula liguse pia Taasisi zote zitakazotokana na sheria zitakazotungwa kwa mjibu wa katiba mfano vyama vya siasa, Taasisi za kijamii nk.

MSINGI
Inaonekana sasa utumishi wa umma na nafsi za kuchaguliwa ni raslimali ajira ambayo ni stahiki ya kila mtu. Hatua za makusidi lazima zifanyike ili kuhakikisha kila mtu anapata na kufaidi.

KUUNDWA KWA BUNGE LA MABWANYENYE
Bunge la mabwanyenye linatoa nafasi ya kutumia raia wazoefu na wazeefu kutoa ushauri kwa serikali bila mihemuko kama ilivyo kwenye bunge la kawaida. Kila jambo litakalopitishwa na bunge la kawaida lazima lijadiliwe tena na bunge la mabwanyenye kabla ya kupelekwa kwa rais kusainiwa na kuwa sheria.

Hii itaondoa mihemuko ya uchama. Nafasi za bunge la ubwanyenye ziwe za kuomba na kusailiwa kwa njia ya uwazi na kisha kupigiwa kura na bunge la kawaida. Ukubwa wa bunge la mabwanyeyenye usizidi idadi ya mikoa na usifate ueneo wala ukanda- ufate weledi.
Hauwezi kutoa rais kwa kupokezana nje ya mfumo wa vyama vingi, ndani ya mfumo wa chama kimoja unaweza.
 
Back
Top Bottom