Redpanther
JF-Expert Member
- Feb 23, 2019
- 2,813
- 3,768
Habari gani watu wa nguvu..! Poleni kwa Majukumu ya siku nzima na kwa wale walioingia kazini usiku huu, Majukumu mema.
Acha niende kwenye maada, katika karne hii ya 21 kuna mambo memgi yamejitokeza, Mengi mazuri na Mabaya machache.
Moja ya mambo yaliyokuja kwenye karne hii ya 21, ni pamoja ujio wa mitandao ya kijamii ambayo imeshika hatamu sana na ukijumlisha uwepo wa simu janja basi mambo ni Mbwai mbwai tu.
Uwepo wa simu janja umeleta mengi mazuri ikiwemo biashara za mitandaoni na ajira pia kwa wale ambao wanafanya kazi kama freelancer. Changamoto ambayo nimeiona imeikumba jamii yetu ni kwamba, watu siku, inaonekana, wanafurahi sana wanapokuwa wanachati kwenye simu kuliko wakikutana uso kwa uso kufanya mazungumzo.
Nichukulie mfano tu, Mtu mnapokuwa mmekutana kama OUTING na rafiki au marafiki watu wanakuwa busy sana na simu zao kuliko ilivyo kawaida. Kama hapa nimekuja kupata moja moja baridi, kuna jamaa kaja na mtu hapa, sijui ni demu wake au rafiki tu. Kikichonishangaza ni kwamba wameagiza vinywaji na Nyama choma. Baada ha hapo kila mmoja yupo busy na simu .
Sasa kutoka out maana yake nini, yaani mtu mko busy kuchati na misimu yenu. Alfu jamaa anaonekana sijui niaje niaje yaani.
Kuna muda dada anaweka simu chini, jamaa liko busy na simu. Daah, huu sijui ni ushamba au ni nini. Hayanihusu ila imenibidi niseme tu. Mkitoka out, msichat sana ndugu zangu mnaumaliza utamu wa mtoko. Ni hayo tu