Kujianika mbele ya hadhara kisa unaongea na simu ni uzwanzwa!

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,167
11,487
Nilikuwa nasafiri kutoka Dodoma kuja Dar! Njiani jamaa anaongea na simu mwanzo mwisho na kujionyesha anafanyakazi gani na matumizi ya hela na miradi aliyonayo na mahusiano na blahblah nyingi!

Gari zima lilijua yeye ni nani hadi ikawa kero na kutuboa! Mpaka jamaa mmoja kamtolea mbovu ya kwamba anatukera na kutupigia kerere na kwamba hakuna mtu anataka kujua habari zake hivyo afunge domo lake! Woote kwenye basi tulimpigia makofi! Juzi napanda usafiri wa umma! Mmama mmoja mwanzo mwisho tulimkoma jinsi alivyokuwa anajishaua kwa mali na ukwasi alionao na namba ya watu wanaomtegemea, na blahblah nyingi hila nashukuru niliteremkia njiani nikasema Asante Mungu maana si kwa kukereka kule!

Sasa leo nipo sehemu ya open space kuna watu wengi tu wamepumzika na wanaongea mambo yao kwa sauti ya chini kiasi kwamba jirani hawezi kusikia. Kaja jamaa pembeni kakaa na wadada wawili! Daah! Si kwa majisifu hayo sijui hiki kitambi nimejaribu kukipunguza kimekataa! Mara mimi laki moja kwa siku hainitoshi na n.k! Sasa watu wa namna hii dishi limeyumba au nini?

Hawawezi kujiongeza na kujiuliza habari zao ni kero kwa wengine?
 
Nilikuwa nasafiri kutoka Dodoma kuja Dar! Njiani jamaa anaongea na simu mwanzo mwisho na kujionyesha anafanyakazi gani na matumizi ya hela na miradi aliyonayo na mahusiano na blahblah nyingi! Gari zima lilijua yeye ni nani hadi ikawa kero na kutuboa! Mpaka jamaa mmoja kamtolea mbovu ya kwamba anatukera na kutupigia kerere na kwamba hakuna mtu anataka kujua habari zake hivyo afunge domo lake! Woote kwenye basi tulimpigia makofi! Juzi napanda usafiri wa umma! Mmama mmoja mwanzo mwisho tulimkoma jinsi alivyokuwa anajishaua kwa mali na ukwasi alionao na namba ya watu wanaomtegemea, na blahblah nyingi hila nashukuru niliteremkia njiani nikasema Asante Mungu maana si kwa kukereka kule! Sasa leo nipo sehemu ya open space kuna watu wengi tu wamepumzika na wanaongea mambo yao kwa sauti ya chini kiasi kwamba jirani hawezi kusikia. Kaja jamaa pembeni kakaa na wadada wawili! Daah! Si kwa majisifu hayo sijui hiki kitambi nimejaribu kukipunguza kimekataa! Mara mimi laki moja kwa siku hainitoshi na n.k! Sasa watu wa namna hii dishi limeyumba au nini? Hawawezi kujiongeza na kujiuliza habari zao ni kero kwa wengine?
Pambana uwezavyo mwanao aitwe wakishua la sivyo atakuja kuwa na hizo tabia ulizotusimulia bwana mmbeya

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
akina pro janabi wanaposema magonjwa ya akili ni tatizo kubwa hapa nchini manawaona wanoko.

yaani mtu anakaa na akili zake akidhani watu wanataka kujua kazi yake,nyumba yake,mke wake,watoto wake,pesa zake.

wengine tunakata simu ukipiga kwenye gari.
 
Nunua ear pods zitakisaidia kutosikika mbwembwe za hao washamba na wangese pia.
Pia ukiwa na ear pods zitakusaidia siku ukilala na mtu anayekoroma.
 
Nilikuwa nasafiri kutoka Dodoma kuja Dar! Njiani jamaa anaongea na simu mwanzo mwisho na kujionyesha anafanyakazi gani na matumizi ya hela na miradi aliyonayo na mahusiano na blahblah nyingi! Gari zima lilijua yeye ni nani hadi ikawa kero na kutuboa! Mpaka jamaa mmoja kamtolea mbovu ya kwamba anatukera na kutupigia kerere na kwamba hakuna mtu anataka kujua habari zake hivyo afunge domo lake! Woote kwenye basi tulimpigia makofi! Juzi napanda usafiri wa umma! Mmama mmoja mwanzo mwisho tulimkoma jinsi alivyokuwa anajishaua kwa mali na ukwasi alionao na namba ya watu wanaomtegemea, na blahblah nyingi hila nashukuru niliteremkia njiani nikasema Asante Mungu maana si kwa kukereka kule! Sasa leo nipo sehemu ya open space kuna watu wengi tu wamepumzika na wanaongea mambo yao kwa sauti ya chini kiasi kwamba jirani hawezi kusikia. Kaja jamaa pembeni kakaa na wadada wawili! Daah! Si kwa majisifu hayo sijui hiki kitambi nimejaribu kukipunguza kimekataa! Mara mimi laki moja kwa siku hainitoshi na n.k! Sasa watu wa namna hii dishi limeyumba au nini? Hawawezi kujiongeza na kujiuliza habari zao ni kero kwa wengine?
Acha kufuatilia mambo ya watu
Mmbea sana wewe..! Kitu kimetokea kwenye basi hadi jf kimefika bila shaka wewe ni mpemba wewe!
 
Back
Top Bottom