Kuchati kwenye simu wakati mmetoka 'out' na mtu ni kero

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
2,813
3,767
Habari gani watu wa nguvu..! Poleni kwa Majukumu ya siku nzima na kwa wale walioingia kazini usiku huu, Majukumu mema.

Acha niende kwenye maada, katika karne hii ya 21 kuna mambo memgi yamejitokeza, Mengi mazuri na Mabaya machache.

Moja ya mambo yaliyokuja kwenye karne hii ya 21, ni pamoja ujio wa mitandao ya kijamii ambayo imeshika hatamu sana na ukijumlisha uwepo wa simu janja basi mambo ni Mbwai mbwai tu.

Uwepo wa simu janja umeleta mengi mazuri ikiwemo biashara za mitandaoni na ajira pia kwa wale ambao wanafanya kazi kama freelancer. Changamoto ambayo nimeiona imeikumba jamii yetu ni kwamba, watu siku, inaonekana, wanafurahi sana wanapokuwa wanachati kwenye simu kuliko wakikutana uso kwa uso kufanya mazungumzo.

Nichukulie mfano tu, Mtu mnapokuwa mmekutana kama OUTING na rafiki au marafiki watu wanakuwa busy sana na simu zao kuliko ilivyo kawaida. Kama hapa nimekuja kupata moja moja baridi, kuna jamaa kaja na mtu hapa, sijui ni demu wake au rafiki tu. Kikichonishangaza ni kwamba wameagiza vinywaji na Nyama choma. Baada ha hapo kila mmoja yupo busy na simu .

Sasa kutoka out maana yake nini, yaani mtu mko busy kuchati na misimu yenu. Alfu jamaa anaonekana sijui niaje niaje yaani.
Kuna muda dada anaweka simu chini, jamaa liko busy na simu. Daah, huu sijui ni ushamba au ni nini. Hayanihusu ila imenibidi niseme tu. Mkitoka out, msichat sana ndugu zangu mnaumaliza utamu wa mtoko. Ni hayo tu

giphy.gif
 
Tukubali tu mambo yamebadilika. Ukiwa na smartphone dunia yote ipo kiganjani. Unachat na marafiki zaidi ya 20 kwa wakati mmoja.
 
Hilo ni tatizo. Na mkiwa naongea unashangaa anaitika, "mmmh, kweli, aaah sana, naona, eeh kweli" hamuwezi kabisa kusocialize au kuongea ishu ya maana.

Mimi huwa nauliza .. eeeh nini ?? Kwa sura serious no way, siwezi vumilia ujinga wa hivyo.
 
Dah kweli kabisa mkuu mnajikuta hadi mnaondoka mlichokiongea hamna,kila mtu yupo busy na simu.

Nimekuwa namuangalia mdada, anajitahidi sana anaweka simu chini. Kuna moja iliwahi nitokea mimi nikiwa nimetoka na Mama la mama, alizingua mie sikupenda. Tumetoka out tunafika hivi si kawakuta classmate wake ambao yeye binafsi anasemaga wanamsnitch sana sasa kafika kawakuta counter pale akakaa japo anapiga story niliyekuja naye akaniweka nikakaa pekee yangu alfu ndio akaja. Nikamwuliza kwa umetoka kuja kuonana na hao ama..!?? Nilimwambia umenikata stimu nikaingia zangu JF.
 
Aisee kwahiyo ukawekwa benchi kwanza? 😀😀
 
Nichukulie mfano tu, Mtu mnapokuwa mmekutana kama OUTING na rafiki au marafiki watu wanakuwa busy sana na simu zao kuliko ilivyo kawaida. Kama hapa nimekuja kupata moja moja baridi, kuna jamaa kaja na mtu hapa, sijui ni demu wake au rafiki tu. Kikichonishangaza ni kwamba wameagiza vinywaji na Nyama choma. Baada ha hapo kila mmoja yupo busy na simu
emoji3064.png
. Sasa kutoka out maana yake nini, yaani mtu mko busy kuchati na misimu yenu. Alfu jamaa anaonekana sijui niaje niaje yaani.
Kuna muda dada anaweka simu chini, jamaa liko busy na simu. Daah, huu sijui ni ushamba au ni nini. Hayanihusu ila imenibidi niseme tu. Mkitoka out, msichat sana ndugu zangu mnaumaliza utamu wa mtoko. Ni hayo tu
Niliwahi kusema kwamba janga kubwa baada ya covid19 ni social media ,hii issue kisaikolojia ni zaidi ya janga mfano mdogo tuu hapo ungekua na WhatsApp ya Huyo Dada ungekuta status ya hizo bia+nyamachoma,Tutumie werevu tuliopewa na Mwenyezi MUNGU kutawala hiizi technolojia maana itachkua nafasi ya vitu Vingi sana katika maisha yakawaida
 
Sasa kwanini utoke OUT na mmoja? Si unajifungia tu ndani siku nzima ili ikiwezekana u socialize na watu zaidi ya milioni kutoka nchi zote duniani?
Kwa hiyo mt asijibu meseji za watu wengine kwa sababu yupo na DEMU???
Yaani mchepuko/malaya/mdangaji/mpinga vizinga anifanye mimi nisijibu meseji za watu wengine??? Kkkkk be serious!
 
Kwa hiyo mt asijibu meseji za watu wengine kwa sababu yupo na DEMU???
Yaani mchepuko/malaya/mdangaji/mpinga vizinga anifanye mimi nisijibu meseji za watu wengine??? Kkkkk be serious!

So unao tokaga nao out ni madanga au Malaya tu basi hujawahi kutoka out na mtu wako ambaye mko naye kwa serious relationship ?
 
Back
Top Bottom