Kuazima gari ni ustaarabu?

Kuazima gari ni ustaarabu?

Kwa wamiliki wa gari sio magari ni ngumu au haiwezekani kuazimisha maana hilo gari likiaharibiki na mmiliki wake huingia maradhi kama anaumwa mkewe vile!
 
Mkuu jigili, use your common sense..
Mimi nina gari lakini ni mtu mmoja tuu kati ya marafiki zangu naweza kumpa gari langu japo nina marafiki wengi.
Sababu za msingi ni kama ifuatavyo;
  • Hata kama ni rafiki yako, usimpe gari, badala yake kama unaweza na una nafasi, mpeleke mwenyewe. Unapoendesha gari lako unajua how to take care.
  • Hebu fikiria una rafiki unampa gari. Inatokea inapata ajali alafu mtu mwenyewe hana hata hela ya matengenezo unapigiwa simu gari iko mtaroni utafanyaje? kumdai huwezi, ukimwacha roho itakuuma.

Mimi kuna baadhi ya miji nikienda siweki bajeti ya taxi kwa vile kuna washkaji nikifika naazima gari natumia kwa shuguli zangu hadi siku naondoka. Pia baadhi ya jamaa zangu wakija mji niliopo wanafanya the same. Kikubwa sio kuazimana gari, ni unamuazima nani gari. Gari ina insurance, unayemuazima ni mtu wako wa karibu unamjua vizuri jinsi anavyoendesha na tabia zake. Kama ni mvuta sigara siwezi kumpa, kama anapenda sifa na kukimbiza hovyo au anapakia machangudoa lazima unakuwa unamjua vizuri. Lakini kama jamaa yangu kaja kwa shuguli zake then anahitaji gari jioni atembelee jamaa zake, atoke out na washkaji zake wakati Mimi situmii gari muda huo nampa.
 
Last edited by a moderator:
gari anaazima hadi ridhiwani kikwete sembuse wewe mlalahoi? au hamkusikia ridhiwani akisema msione anabadilisha magari tu hayo ni mambo ya kimjinimjini tu, yeye anamiliki toyota Camry moja tu.

wazungu walishapita kote huku ambako sisi leo mishipa ya shingo inatutoka na ndio maana walibuni rent car self driving, ili kuondokana na kumtukuza mtu kwa sababu ya makopo haya.

Mkuu siku nyingine unaandikaga point
 
sasa mimi nina jamaa yangu ana gari yake na akisafiri huipaki kwangu kwa sababu kwake hana parking ili kuokoa gharama za ulazaji magari na ufunguo uniachia pia.

lakini mpaka anarudi gari yake huikuta iko vilevile ninachokifanya uwa namsaidia kuiwasha injini asubuhi iungurume na kuizima. that's it.
 
Mkopo wa gari hata Sijaumaliza,halafu nikuazime ukatongozee wazaramo!!akyanani haiwezekani nakataa kabisa

kigari cha million 7 tu mpaka upate mkopo? basi ujuwe unafosi tu hujafikia uwezo wa kumiliki gari.
 
gari anaazima hadi ridhiwani kikwete sembuse wewe mlalahoi? au hamkusikia ridhiwani akisema msione anabadilisha magari tu hayo ni mambo ya kimjinimjini tu, yeye anamiliki toyota Camry moja tu.

wazungu walishapita kote huku ambako sisi leo mishipa ya shingo inatutoka na ndio maana walibuni rent car self driving, ili kuondokana na kumtukuza mtu kwa sababu ya makopo haya.
Teh teh! Gari sio MATA..ko Kila mtu anayo, tunajua hupendi unavyopangwa na kukanyagwa kwenye ma DCM,ni Ukapuku 2 utafanyaje? tunajua na wewe unatamani kumiliki kopo la 50m teh! teh! teh!
 
Kuna jirani yangu amekuja leo kwangu anaazima gari awapeleke jamaa zake kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Jirani mwenyewe japo namfahamu kwa sura lakini hata jina lake silifahamu kwa sababu si miongoni mwa majirani ambao tuna ukaribu sana.Swali likanijia huyu bwana anafunga safari kuja kuazima gari kama fyekeo hivi akipata nalo ajali atakuja na maelezo gani?
Lazima tujifunze kuishi kwa kile mwenyezi Mungu alichotukadiria
kama hamjazoeana siyo ustaarabu.Na hata waliozoeana
ustaarabu unaangaliwa kwa mambo yafuatayo
1.sababu inayokufanya uazime gari
2. Gari unalirudisha katika hali gani,nikimaanisha uzima usafi na mafuta siyo mtu anakupa gari yake likiwa na tank full au nusu unamrudishia likiwa hamna kitu,hata kama mmezoeana huo sio ustaarabu.
 
... jirani yako ana socialist mentality. In a capitalist society you have to think twice.

Ndo tatizo la kuishi kwenye capitalist society and now we are in imperialism, mtu ana malori 40 at the same time kuna mtu hajui atakula nini kwa siku hiyo..! And there is no way
 
Kuna jirani yangu amekuja leo kwangu anaazima gari awapeleke jamaa zake kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Jirani mwenyewe japo namfahamu kwa sura lakini hata jina lake silifahamu kwa sababu si miongoni mwa majirani ambao tuna ukaribu sana.Swali likanijia huyu bwana anafunga safari kuja kuazima gari kama fyekeo hivi akipata nalo ajali atakuja na maelezo gani?
Lazima tujifunze kuishi kwa kile mwenyezi Mungu alichotukadiria

Mie bnafs gar langu sikupi kama sio rafk yangu,jiran itokeee mkeo ameshikwa uchungu usku ntampeleka hosp kwa gar yangu sio nkupe ww udrveee,ukipata nalo ajal najua huna uwezo wa kulinyoosha wala nunua pampa ya mble hvo tutakorofshana tu n bora unchukie kulko mimi kukuchukia kwa uharbifu wa mali angu.hutak acha kwan wakat natafuta mpaka nmelnunua gar ww ulikuwa wapi?jifunze kuish kwa kile mungu alchokujalia

Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
Gari yako ni kama Mke/Mume wako , kama huwezi kumuazima mtu Mkeo usimuazime mtu gari yako.
Hii nimesikia leo! Naomba ambao hawajaoa wasiige hii.Mke/mme ni zaidi ya gari.
Gari likikusumbua unauza,mke/mme?
 
Uchumi wako ni wa kiwango fulani, ndiyo maana huoni tabu kumwazima fyekeo. Uchumi wako ungekuwa wa kiwango fulani kingine usingeona tabu kumwazima gari. Nakublina nawe kwamba jamaa anakosea kujaribu kwenda kinyume na hali zenu za uchumi.

Hujamuelewa jamaa inavyoonekana, ukisoma vzr Uzi utaona jamaa yupo tayari kumuazima tatizo hawapo too close to the extent ya kuazimana vitu kama magari.. Hujue kuna vitu au huruma unaweza ukafanya baadae tatizo likitokea utashindwa hata ya kuelezea ilikuaje
 
Jamaa yangu aliniazima gari wakati naenda kuoa toka Dar kwenda mkoani, Landcruiser Prado, akaniwekea na mafuta full tank na gari nilikaa nayo wiki nzima ndio nikamrudishia. Tena ilikuwa ndio gari yake ya thamani kuliko nyingine na wakati nimesafiri akawa anashea na mkewe gari kwenda kazini. Inategemea mnahusiana vipi na uwezo wako kiuchumi. Una kagari kamoja, tena ka mkopo then unamuazima "mtu baki" hata Mimi nisingetoa.

Si useme tu ulienda kuoa Iringa
 
Kuna jirani yangu amekuja leo kwangu anaazima gari awapeleke jamaa zake kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Jirani mwenyewe japo namfahamu kwa sura lakini hata jina lake silifahamu kwa sababu si miongoni mwa majirani ambao tuna ukaribu sana.Swali likanijia huyu bwana anafunga safari kuja kuazima gari kama fyekeo hivi akipata nalo ajali atakuja na maelezo gani?
Lazima tujifunze kuishi kwa kile mwenyezi Mungu alichotukadiria
Sasa hiyo personal issue ya jirani yako kutaka kukuazima gari, nayo unaileta humu janvini?

Sasa kama wewe mwenyewe kama ulivyosema huyo jirani yako humjui hata jina lake!

Sasa ulishindwa nini kumpasulia LIVE kuwa pamoja na kuwa nyinyi ni majirani, lakini ujirani huo una mipaka yake, vipo vitu vya kushare, lakini vingine siyo vya kushare, vikiwemo hilo gari lako plus your wife/husband!!
 
Back
Top Bottom