Kuazima gari ni ustaarabu?

Kuazima gari ni ustaarabu?

Cha mtu mavi mambo ya kuazima azima si ustaarabu iwe chochote.

Ulichotakiwa kufanya kama hukujisikia ni kumtosa sio unampa kisha unalalamika na kuwa na wasi pengine anaweza pata ajali na kuwaza mengi kichwani
 
hivi jirani yako akija kukuazima kitu mpaka uje kuuliza jf?!! haujatuambia ulimjibu nini (huenda ulimwongopea), ulitakiwa umpe za macho kuwa "hapana ndugu yangu, hatufahamiani sana hivyo sitakupatia, ni kwa ajili ya usalama wako na wangu pia", lakini kama ni jirani mnafahamiana baba fulani baba fulani sioni ubaya kumpa, otherwise siyo jambo la kujadili saana mpaka jf!!
 
Kuna jirani yangu amekuja leo kwangu anaazima gari awapeleke jamaa zake kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Jirani mwenyewe japo namfahamu kwa sura lakini hata jina lake silifahamu kwa sababu si miongoni mwa majirani ambao tuna ukaribu sana.Swali likanijia huyu bwana anafunga safari kuja kuazima gari kama fyekeo hivi akipata nalo ajali atakuja na maelezo gani?
Lazima tujifunze kuishi kwa kile mwenyezi Mungu alichotukadiria

mkuu kuna watu hawana soni wala woga kwenye mali za wengine hata kidogo!

Kwa mali kama hiyo ama yoyote ile, ni lazima kwanza uwe mwangalifu, unaweza kukuta mtu kahamia tu ajifunze mazoea na wewe, baada ya muda tu, anakwapua kila kilicho chako cha thamani.. mjini wapi? shule baba!
 
Kwani gari ina nini usiazime mwenzio? Kama kitu cha maana sana mbona ukifa huzikwi nayo?
Cha msingi
1.mufahamiane,
2.Ajue kuendesha,
3.ujue shughuli anayoenda kufanyia.
Tuache ulimbukeni ukiwa na gari ndo kujiona umemaliza.

Katika watu wenye hoja za kitoto basi Makamee unaongoza.
 
Last edited by a moderator:
Katika watu wenye hoja za kitoto basi Makamee unaongoza.

Kuna mmoja juzi kaazima gari ya rafiki yake kufika kwenye mataa red ikawaka kajifanya ana haraka kuvuka tu kagongwa ubavuni. Mbona alizimia watu wakadhani amekufa kumbe presha juu alipozinduka machozi yanamtiririka anaambiwa shukuru Mungu umepona unalia nini akajibu gari ya watu hii sijui nalipa na nini
 
Last edited by a moderator:
Uchumi wako ni wa kiwango fulani, ndiyo maana huoni tabu kumwazima fyekeo. Uchumi wako ungekuwa wa kiwango fulani kingine usingeona tabu kumwazima gari. Nakublina nawe kwamba jamaa anakosea kujaribu kwenda kinyume na hali zenu za uchumi.

Basi kaazime gari kwa Dewji, au Mengi!
 
sasa mimi nina jamaa yangu ana gari yake na akisafiri huipaki kwangu kwa sababu kwake hana parking ili kuokoa gharama za ulazaji magari na ufunguo uniachia pia.

lakini mpaka anarudi gari yake huikuta iko vilevile ninachokifanya uwa namsaidia kuiwasha injini asubuhi iungurume na kuizima. that's it.
thats brilliant mzee.......cha mtu mavi.
kwa kuongezea, hata kama ingelikuwa na wewe huna gari, hilo la kwake unaliacha hapo hapo na unapanda zako daladala.
 
Sasa hiyo personal issue ya jirani yako kutaka kukuazima gari, nayo unaileta humu janvini?

Sasa kama wewe mwenyewe kama ulivyosema huyo jirani yako humjui hata jina lake!

Sasa ulishindwa nini kumpasulia LIVE kuwa pamoja na kuwa nyinyi ni majirani, lakini ujirani huo una mipaka yake, vipo vitu vya kushare, lakini vingine siyo vya kushare, vikiwemo hilo gari lako plus your wife/husband!!
amefanya la maana sana kushare, faida kubwa imepatikana kutokana na komenti za wachangiaji.
kuna wengine walitamani tu kujua mambo ya kuazimana magari na nini cha kufanya.
 
huyo
Heshimu gari baba .gari siyo kiungo mtu anazaliwa nacho.
huyo mtu wa karibu nilishawahi kumuazima gari masaa matano badae kapata nalo ajari tena akiwa amelewa...garama matengenezo ilikuwa 1.2m , wala nusu ya gharama hakuweza kuto.
ukiazimisha gari, u do it for your own risk.ushikaji ndo unatuponza waafrica.
 
Back
Top Bottom