sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,034
Yes, Pesa sio kila kitu, ni mpaka ikosekane kabisa ndio kila kitu ila ukiwa nayo hata kiasi sio kila kitu. Najua kuna msemo siku hizi kila mara "Tafuta Pesa" ila ukichunguza ni athari za watu walioishi katika umaskini tangu wadogo hivyo kisaikolojia wanaamini pesa ni kila kitu, siwezi kuwalaumu.
Ok tukija kwenye lengo la hii post ni wazi kabisa kwamba pesa sio kila kitu.
Rafiki yangu alikuwaga wa kishua sana miaka ya 2006 tu hapo simu haikosi anawekewa vocha za laki na mzee wake, pesa ya matumizi ya kutosha. Simu yake ndio niliitumia sana mzee ananipigia simu kwa namba yake kujua hali yangu, nikichelewa nyumbani anaona wazazi wananigombeza, akija nyumbani tuna mkaribisha chakula, anaona namna tunapiga stori na mzee. basi kuna siku akaniambia hawezi kujifikiria hata mara mbili tubadilishane nafasi za wazazi sababu wazazi wake hawana time nae kabisa zaidi ya kutuma pesa.
Niliwahi kuwa na mbwa wangu nimemkuza tangu mdogo, kuna mtu alikuwa anamtaka aliniletea hadi shilingi laki 5 lakini wapi, nilimwambia hata aje na milioni 5 huyo mbwa siuzi, huyu mbwa kuna kipindi mtoto alitoka nje kuna mbwa sijui aliruka fensi akataka kumshambulia mtoto, alimtoa nduki huyo mbwa koko.