Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Mbona hakuna taarifa za kiintelijensia kuwa wataiba kura au kuwa wananchi watavamiwa usiku wa manane na maninja kisha kubolewa nyumba zao? kwahio hata ibada zisifanyike mana kuna mikusanyiko!!!! Masaburi style
 
Kutokana na taarifa ya polisi, maandamano ya kupinga malipo ya Dowans hayawezi kufanyika kutokana na hofu ya Al Shabab.

Source ITV saa 2 usiku.
Hii ni kali ya miaka 50 ya uhuru... Al Shabaab na dowans wapi na wapi? Hawa manjagu wamepiga ramli ndio mganga akawapa huu usanii
 
Intelijensia ya Jeshi letu hii. Acha nicheke miye!
Lakini kwanini intelijensia yetu inaonyesha kufanikiwa kwenye mambo ya MAANDAMANO tu, na si kwenye issu kama KILIMO KWANZA na uchumi?
 
Intelijensia ya Jeshi letu hii. Acha nicheke miye!
Lakini kwanini intelijensia yetu inaonyesha kufanikiwa kwenye mambo ya MAANDAMANO tu, na si kwenye issu kama KILIMO KWANZA na uchumi?
Nadhani kuna haja ya kuahirisha maazimisho ya miaka 50 ya uhuru, mechi ya simba na yanga na mikusanyiko mingine mingi itayojumuisha viongozi wa taifa na kimataifa kwa kuhofia Al Shabab!
 
Tufike mahali tuheshimu ushauri unaotolewa na vyombo vya usalama siyo kubeza kila tunachoambiwa. Yanayowapata wakenya hamyaoni?????
 
Hili ni zito, tuone Wana-Harakati wameweka uzito gani juu ya jambo lenyewe..!
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

Polisi wana source nyingi za kujua hatari inayoweza kujitokeza. Tusipuuze kwa ajili ushabiki tu.
 
Mnaumiza vichwa bure jamaa anataka kutulipia deni ndio maana hataki maandamano,anaona mbali.Aaaaah i was dreaming.......
 
Hili tishio la dowans hajawahi kuliona hata kidogo?

Tuwache ushabiki jamani. Mwenzenu ANANILEA NKYA kisha pokea chake sasa anataka kutuingiza vitani. Hivi huyu mama kasomea sheria kweli?. Basi vurugu zikianza na awe Mbele kabisa ili aoneshe uzalendo wake. Hili Deni lazima lilipwe tu tulishafanya makosa tena yaliosababishwa na siasa zetu za kupakana matope. Hivi kweli tumefika huko ambako sasa tunajifanya hatutaki kuheshimu sheria za kimataifa?
 
Nadhani kuna haja ya kuahirisha maazimisho ya miaka 50 ya uhuru, mechi ya simba na yanga na mikusanyiko mingine mingi itayojumuisha viongozi wa taifa na kimataifa kwa kuhofia Al Shabab!

kweli umenichekesha sana..
 
kwa mara ya kwanza ninakubaliana na Polisi ktk hili sababu kwa kipindi hiki ambacho hali ni tete hawa jamaa Al shabab wanaweza kutupiga ktk maandamano na kusababisha mass casualty,tukikumbuka uganda jinsi walivyoshambuliwa wakati wakiangalia world cup.Kifupi kwa kipindi hiki tujiepushe na mikusanyiko siyo ya lazima.

thats rediculas usalama wa nchi watakua wapi?
 
Tatizo hawa maitelijensia wetu wanafikiria kwa masaburi! Vitu vya muhimu kwa Taifa kwao havina umuhimu...

Tusibeze vyombo vyetu vya ulinzi. Amani ya nchi yetu inatokana na kuwajibika ipasavyo kwa hivi. Tukisema vinafikiri kwa matusi ni sawa na kumtukana mzazi wako wakati nguvu uliyo nayo inatokana na kuhangaika kwake ili upate kula. Laana hizo. Hakuna mtanzania ambaye anapenda DOWANS ilipwe lakini pia kama nchi iliyoridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa hatuna budi kukubaliana na uamuzi wa ICC
 
Nawaomba Tanesco walipe deni la DOWANS mapema kuepuka hili deni kukua zaidi.
 
This iz Tz bhana ukicomplicate saanA utalala na viatu! Kila chenye mwanzo kina mwisho! Akili kumk.......
 
Hivi kumbe Dowans ni Al shabab hii ni siri nzito ndiyo maana huko nyuma imekuwa vigumu kutaja wamiliki wa Dowans!! Sasa tuna sababu za uhakika za kuandamana. Kumbe watawala wetu wanafanya kazi na Al shabab kuhujumu wananchi?
 
Ukitaka kufanya maandamano unatakiwa kutoa taarifa polisi tu. taarifa ishatolea amani ya watwa na sidhani kama kova ana haki kuzuia maandamano yu makini. lakini akumbuke kuwa ana doa kubwa pale ambapo jeshi la poilisi aka magamba wameshindwa kuzuia uhalifu ndio maana wanasindiukiza sukari ivushwe nje ya mipaka yetuulishi na -maneno ya pinda waziri mkuu. polisi nchi hii imewachoka maana hawajishha ughulishi na usalama wa raia na mali zao. leo wezi/vibaka wakiiba vitu na ukaenda kituo cha polisi utaambiwa hawawezi kuja eneo la tukiob kwa sb hakunab gari aunkama lipo halina mafuta wanataka uchangie na wakihisi huwezi na huna pesa utaabiwa kamkamate mwizi wako uje nae. polisi tumewacvhoka lakini kumbuka nanyi ni sehemu ya jamii. dowans isipolipwa kiasi hicho ni kewa manufaa yetu na nyie mkiwemo
 
Kuna uhusiano gani wa kulipwa doainzi na Al Shabaab?!! Ifike muda watawawala wetu wawe wanafikiri kwa kutumia bongo zao badala ya kuendelea kutumia nyayo zao kufikiri!!!!! Shwine kabisa


nadhani kuna watu kwenye dowans wana mahusiano na dowans
 
Back
Top Bottom