Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Kova unataka kutuambia Al shabab wapo nchini tayari,na je kama hivyo nvdivyo polisi wamechukua hatua gani?hivi anawajua Alshabab au anawaangalia kwenye TV na kuwasoma kwenye gazeti?akawaulize Uganda watampa jibu,na kama iko hivyo hatua gani zimechukuliwa kuzuia mikusanyiko?je ligi ya vodacom itasimama?je mechi ya simba na yanga nayo itaahirishwa?hapo wamechemka,je kwenye night club amabazo zinakuwa na watu wengi wamefanya nini kuzuia mashambulio yasitokee?makanisani na misikitini hali ya usalama ikoje?
Hapana hapo naona wanaibeba serikali kwa kuwa wao ni vibaraka wa sisiemu-magamba basi wametafuta mbinu ya kuzuia,kwani naamini ccm lingewashuka.
Jamani wa JF tutafanyaje kuonyesha hisia zetu juu ya DOWANS
kwahiyo anajua wapo, na hao alshabab watahakikisha kwamba wanaharibu maandamano kwa manufaa ya dowans, in short alshabab wanasapoti dowans, na jeshi la polisi linajua, na hivyo basi jeshi la polisi haliwezi kulinda wananchi wake dhidi ya alshabab kwasababu alshabab ni wakali zaidi ya jeshi letu na in other words polisi wamehalalisha uwepo wa alshabab kwetu ingawa juzi tuliambaiwa tusiwe na wasiwasi.

akili yangu fupi kama mie mwenyewe inaniambia alshabab wapo, hawana madhara kwa sasa ila tukiandamana tu tutakoma.... aisee!!

sasa sijui walipitia mipaka ipi?
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....
Hizi sio zile taarifa za kiintelijesia kama zile za maandamano ya arusha??
 
Kamanda Kova amezuia maamndamano yaliyoandaliwa na wanaharakati kwa kile alichodai kuwa ni kuepuka uwezekano wa kushambuliwa na Al Shabab eti ni kusanyiko na kwamba ikitokea maafa jeshi la polisi litalaumiwa (source ITV)

Namuunga Mkono

Lakini sijamsikia kamanda akikataza makusanyiko mengine kama yale yanayofanyika makanisani, misikitini ama mikutano yoyte mikubwa. Kwa mimi nilitegemea makusanyo mengine yote yapigwe marufuku kwa sababu hizo hizo alizozitoa kamanda ili kuepusha kile alichodai ni mashambulizi ya Al Shabab.

Kwa mtazamo wangu mimi naona hizi ni mbinu za mafisadi yanayohusika na Richmond/Dowans yaliyotengeza mpango ambao unaonekana kushirikisha viongozi wa ngazi za juu akiwemo Kamanda.

Je tutafika salama?

Hata ile graduation ya UDSM isingefanyika.
 
Hapo penye bold pameharibu kabisa maana halisi ya ujumbe wa bandiko lako hili.
Kwa kifupi umejichanganya.Umemuunga mkono,halafu ukampinga,then ukajipinga na wewe mwenyewe.
Ndo ukweli huo.
 
hizo ndo akili za askari wetu na inelijensia zao! masaburi kwisha kazi.
 
hizo ndo akili za askari wetu na intelijensia zao! masaburi kwisha kazi.
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....
In the good old days, the good guy wore the white hat and the bad cowboy wore the black hat.
 
Ama kweli fumbo mfumbie mjinga mwerevu atalifungua! Al shaabab watakuja kwenye maandamano alafu waache mechi ya simba na yanga!? Hebu tusifanyane watoto jamani! Wewe Kova na wenzako jiongezeni upeo wenu wakufikiri!
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

Sasa wameamua kutumia Al Shabab ili kuwazuia Watanzania kuandamana!!!!!....wasanii hawa wanaudhi sana.... watasema lolote lile ili kuzuia haki za Watanzania katika kuonyesha kutoridhika kwao na Serikali taahira.
 
Wakati watu wameshakula mshiko wa maonyesho na maadhimisho? Usilete utani na matumbo ya watu mzee

Nadhani kuna haja ya kuahirisha maazimisho ya miaka 50 ya uhuru, mechi ya simba na yanga na mikusanyiko mingine mingi itayojumuisha viongozi wa taifa na kimataifa kwa kuhofia Al Shabab!
 
Maandamano ya watu kudai haki zao na kujaribu kuzuia kile kidogo kilichobaki kisiibiwe na mafisadi unaita mikusanyiko isiyo na lazima? Na hiyo mikusanyiko inayoendelea kila kukicha ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru ambao hatuujui ndiyo mikusanyiko ya lazima? Kila kukicha pesa zinaendelea kuliwa na watu wanaacha kazi za ujenzi wa Taifa kusherehekea miaka 50 ya uhuru, kila wizara ina wiki yake, na pengine kila shirika la umma lina siku yake. Mpaka hiyo tarehe 9 Desemba itakapofika mikusanyiko mingapi itakuwa imeshafanyika? Na hizo mechi za ligi kuu, na mabonanza, na washindani wa Vodacom Miss wanaokusanyika kila kukicha, hayo yote ni ya lazima? Ama kwako wewe kwa kuwa wananchi wanasimama kupinga azma ya serikali ya ccm kuilipa kampuni ambayo hata jk amedai kuwa hamjui mwenyewe ni nani, pamoja na kwamba itawazidishia ugumu wa maisha watanzania unaona si jambo la lazima? Amka utazame, mbiu imeshalia, Afrika ya jana siyo ya leo. Kuna waliofikiri Hosni Mubarak hataondoka, kuna waliofikiri Ghadaffi hataondoka. Ole wao wanaolala wakifikiri wataendelea kuwanyanyasa watanzania kwa kutokubali kusikia sauti ya wanyonge!
mPUUZE HUYO, DALALI WA UFISADI
 
Kwan sis tuna tatizo gan na Al-shabab,viongoz wetu tunaomba muache kuwachokoza hao jamaa. Hatuna ugomv nao sis.
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

Lakini je Dowans haitalipwa? Hiyo kesi itaishalini? Je tusipoandamana, hao Al-shabab kama wapo hapa tayari kwa mashambulio wataacha azma yao kwa sababu mandamano yamesitishwa? Au na bunge litaahirishwa ili lisishambuliwe na Al-shabab? Au Al-Shaba wana uhusiano na Dowans/TANESCO?
 
Siku zote Nguvu ya utawala wa kimabavu unatokana na kunyenyekea kwa watawaliwa ,hata hivo kama watawaliwa kwa makusudi wanaamua kuondosha ushirikiano na utawala huo, basi utaporomoka tu. Shuhudia utawala wa Hosni Mubarak,Zine el albidine Ali na Gaddafi. Mwisho wa nukuu Gene Sharp: Godfather of non violent revolution.
 
Hivi inamaana raia wakiamua kuandamana, askari wa kova watachukua hatua ya kuwavamia na kuwazuia kwa kutumia nguvu? Na itaweza kutokea matumizi ya mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na labda hata risasi za moto? Na hapa watakua wamewaokoa raia kutokushambuliwa na al-shabaab na kushambuliwa na wao, huyu kova atakuja kulazimika kutujibu haya yote anayosema leo ni intelijensia na kutumia nafasi hiyo ya kazi yake kutimiza matakwa ya wachache kukandamiza wanyonge.
 
Mnajaribu kupinga kisichopingika, Dowans lazma ilipwe.
 
Mnajaribu kupinga kisichopingika, Dowans lazma ilipwe.

Sawa wao washasema lazima walipe maana ni dili lao, sisi tunasema waliohusika tangu mwanzo yote haya yalipoanzia ambapo ni richmond wawajibike na hili, na wafilisiwe katika kulilipa hilo deni na wengine wazembe huko serekalini wakimbizwe mahakamani nao wawajibishwe, sio kukubali tuu eti kisheria tumeshindwa wakati tunaona wazi huu ni wizi kweupeee, upo hapo?
 
Back
Top Bottom