Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Kwani hao Al Shabab si ni sawa na mafisadi ya nchi hii sema ni katika character tofauti tu ni kuwa wale jamaa wanatoa roho za watu hawa mafisadi wa bongo wanaiba mali za watanzania. What is the difference. Hebu aache watu watimize haki yao ya kikatiba. Alah!
 
Imefiki muda viongozi na wananchi wajue haki za kila upande. Viongozi wanajiona wanahaki ya kuamua chochote. Wananchi watafikia mahali watachoka, matokeo hayatakuwa mazuri. Hatuwezi kuwa wajinga siku zote. Maandamano ya kupinga Dowans na al-shabaab wapi kwa wapi?
 
Akapambane na wezi na wahalifu maana ndo anaowaweza si kuzuia maandamano ambayo ni ya kutetea maslahi ya wananchi wa Tz.....
 
hayo maandamano yaleteni arusha huku tungeandamana pamoja na iyo intelijensia yao, wasifanye watu watoto ila ipo siku kitachimbika kama vipi andamaneni hivyo hivyo liwalo na liwe
 
Ingekuwa ni uwezo wangu,maandamano bado yangekuwepo.
Na watanzania wakiendelea kuufyata na kubaki kulia lia kama wengi wetu humu,kama ambavyo wamekuwa wakifanya,basi ukombozi wao/wetu ni bado sana.
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

Kwa hiyo bwana mkubwa wa usalama wa bandari salama yetu anataka kutuambia kwamba kuanzia sasa TZ yetu hakutakuwa tena na mikusanyiko mikubwa kama ya akina waheshimiwa Nape na wengine wa CCM? Au walipwaji wameshatoa shinikizo la kuzuia maandamano!!?? Tulizoea kusikia kauli kama 'Only in America' sasa itakuwa 'Only in Tanzania'. Na itangazwe basi hali ya hatari, tumevamiwa na Al Shabab!!! Tunaogopa kivuli?
 
Haya ndio matunda ya watawala kutumia vyombo vya dola kulinda uozo wao.
 
Kova unataka kutuambia Al shabab wapo nchini tayari,na je kama hivyo nvdivyo polisi wamechukua hatua gani?

Hivi anawajua Alshabab au anawaangalia kwenye TV na kuwasoma kwenye gazeti?akawaulize Uganda watampa jibu,na kama iko hivyo hatua gani zimechukuliwa kuzuia mikusanyiko?je ligi ya vodacom itasimama?je mechi ya simba na yanga nayo itaahirishwa?

Hapo wamechemka, je kwenye night club amabazo zinakuwa na watu wengi wamefanya nini kuzuia mashambulio yasitokee?makanisani na misikitini hali ya usalama ikoje?

Hapana hapo naona wanaibeba serikali kwa kuwa wao ni vibaraka wa sisiemu-magamba basi wametafuta mbinu ya kuzuia,kwani naamini ccm lingewashuka.

Jamani wa JF tutafanyaje kuonyesha hisia zetu juu ya DOWANS
Naashangaa sana uamuzi wa kova kama ni hivyo basi wapige marufuku mikusanyiko yote maana kama ni milipuko ya alshabab inaweza kufanyika hata sokoni kariakoo au ubungo na hata vyuoni kwenye lecture theaters sasa kova anataka kusema huko kote wameweka tahadhari??????
 
alpha5 said:
hayo maandamano yaleteni arusha huku tungeandamana pamoja na iyo intelijensia yao, wasifanye watu watoto ila ipo siku kitachimbika kama vipi andamaneni hivyo hivyo liwalo na liwe
Maandamano haya yanatakiwa yawe ya nchi nzima kwasababu madhara ya malipo ni kwa Taifa zima.

Mtakubali vipi kupangiwa na polisi ambao kwa kupitia kauli ya kamanda mkuu wao, Said Mwema walishakiri kuwa hawawezi kuwashughulikia mafisadi kwasababu wana nguvu sana? Nina uwezo wa kuileta ile habari hapa.Imo humu ndani.

Hivi wananchi waliitafsiri vipi?

Ama wananchi na viongozi wapenda mabadiliko waliingiwa na uvivu wa kufanya hivyo?


Kifupi hapa, ili muweze kuwashinda nguvu mafisadi,basi nilazima kwanza muweze kuwashinda nguvu Polisi.

Kauli ya Kamanda Mwema ilimaansiha kuwa polisi watawalinda mafisadi na ufisadi kwa nguvu zao zote.

Tatizo hajui kuwa nguvu ya wananchi ie nguvu ya umma ni above all that
 
Naashangaa sana uamuzi wa kova kama ni hivyo basi wapige marufuku mikusanyiko yote maana kama ni milipuko ya alshabab inaweza kufanyika hata sokoni kariakoo au ubungo na hata vyuoni kwenye lecture theaters sasa kova anataka kusema huko kote wameweka tahadhari??????
Kuendelea kujadili issue ya Al shabab ni sawa na kucheza mziki wanaoupiga wao mafisadi.Tukifanya hivyo wataendelea kutudharau.

Pointi ya Al shababh ni ya kuignore all the way.Sababu hii haina mantiki kabisa na kuendelea kuijadili ni sawa na kufanya wanavyotaka.Yani getting the eye off the ball.
 
Kutokana na taarifa ya polisi, maandamano ya kupinga malipo ya Dowans hayawezi kufanyika kutokana na hofu ya Al Shabab.

Source ITV saa 2 usiku.
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

Nadhani haya maandamano tungechukua CDM tuwafundishe adabu hawa wajinga....yani haoni tishio la uchumi kuanguka ila anaona tishio la al-shabab.....
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

Hapo ndipo Jeshi la polisi linapofanya kazi kwa utashi wa CCM.

Jana tu akiongea ofisini kwake na waandishi wa habari IGP alisema nchi iko shwari na kwamba wao wamejipanga kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kuhakikisha nchi iko salama sasa tishio la Al Shabab linatoka wapi?

Hapo ndipo jeshi la polisi linapofanya kazi za siasa inakera sana! Kwasababu maisha sasa ni magumu kwa wananchi wote wakiwamo polisi, watu wanataka kuundamana kwa amani halafu linaibuka jitu (Kova) linapinga kwasababu za kisiasa kwakweli inakera!!
 
Wakati mwingine hata kama mtu unatumiwa ni vizuri ukachanganya na zako.
Yani kova bila aibu anasitisha maandamano kwa kisingizio cha tishio la alshaba!!

Kama angekuwa anachanganya na zake angekumbuka kwamba shule hazijafungwa, michezo haijaacha kufanyika na jumamosi kutakuwa na mechi uwanja wa taifa ambapo takriban watu 60,000 watakuwa wamekusanyika pamoja!
 
kwa mara ya kwanza ninakubaliana na Polisi ktk hili sababu kwa kipindi hiki ambacho hali ni tete hawa jamaa Al shabab wanaweza kutupiga ktk maandamano na kusababisha mass casualty, tukikumbuka uganda jinsi walivyoshambuliwa wakati wakiangalia world cup.

Kifupi kwa kipindi hiki tujiepushe na mikusanyiko siyo ya lazima.
 
Sasa hapo yeye ndio anakichokoza kile anachoogopa kisitokee... For a minute najiuliza kama hawa jamaa wenye dhamana ya kuongoza wana akili kweli??
 
Back
Top Bottom