Klabu kubwa Ulaya Zimepata Hasara Wachezaji Wao Kuumia Euro /WC Q 2024/ 2026

Somi

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
3,605
4,360
Kutokana na ratiba ngumu na wachezaji kukosa muda wa kutosha kumpumzika imepelekea Baadhi ya wachezaji kuwa na kipindi kigumu ikiwemo majeraha wakati timu ya taifa Ina wahitaji na vilabu navyo vinawahitaji.

Barcelona itamkosa Gavi kwa msimu wote uliosalia kwa majeraha , na wanajiandaa kupeleka malalamiko kwa chama cha Mpira cha Spain Kwasababu tayari Spain ilishafuzu Euro 24 lakini bado wakamchezesha Gavi Kwenye mechi isiyo na umuhimu .

Real Madrid itamkosa Vicious Junior kwa miezi 2 aliyeumia Kwenye mechi ya Brazil na Eduardo camavinga aliyeumia Kwenye mechi ya france .

Real socieded itamkosa mikael oyarzabal aliyeumia mechi ya spain .

Manchester United itamkosa kwa mechi kadhaa Andre Onana aliyeumia Kwenye mechi ya Cameroon .

Manchester city itamkosa Halaand aliyeumia Kwenye mechi ya Norway lakini hatakawia kurudi uwanjani .

Napoli imeshamkosa Kwenye mechi kadhaa Victor osimhen aliyeumia Kwenye mechi ya Nigeria .

Fifa imetenga dola 150 millioni Kama bima kwa vilabu vyote duniani Kwa msimu wa kufuzu na kushiriki kombe la dunia yaani kipindi cha 2023 Mpaka 2026

Klabu italipwa dola 22450 kwa kila siku ambayo mchezaji aliyeumia atashindwa kutumika Kwenye klabu yake au dola 8.2 millioni kwa mwaka mzima Kiwango cha juu kutoka Fifa .
 
Back
Top Bottom