Ayemeric Laporte: wachezaji wengi waliotoka Ligi za Ulaya wamechoshwa na maisha ya Saudi Arabia

uwe hodari

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
3,994
8,370
Mchezaji wa Zamani wa Manchester City amekuja hadharani na kusema maisha ya Saudi Arabia yamekuwa ndoto za alianacha kwa wachezaji waliotoka ulaya

"Tunawasiliana na wachezaji wengi hapa miongoni mwa waliotoka bara la ulaya, wengi wanaonyesha hawafurahii kabisa maisha ya hapa... Lakini ni changamoto tunajarubu kujifunza"

Hapa Saudi Arabia kila kitu wanaichukulia kwa uzito mdogo, mchezo wa uwanjani bado ni dhaifu bado labda wataboresha kwa kuwa bado wachanga

Pia ni kuhusu wao na maisha yao unaweza kukaa kwenye folen masaa matatu na mambo mengine kama hayo nje ya uwanja

Serkali ya kifalme mjini riadhi imetenga mabilion ya dola kuvisaidia vilabu kadhaa nchini humo kusajili majina makubwa ili kuipeleka saud arabia duniani pmj na maadili yake

Mtakumbuka kuwa baadhi ya wachezaji wamesharudi ulaya na wengine wapo kwenye mazungumzo kuondoka uarabuni kutokana na kutoridhishwa na maisha nchini saudi arabia

Credit :as
 
Fedha siyo kila kitu. Waarabu wanapenda mno sifa na ufahari. Hili la kutumia fedha kununua umaarufu wa mpira China limemshinda. Umaarufu wa ligi unaletwa na wingi wa mashabiki na siyo wachezaji maarufu.
Mwanzo nilimshangaa sana Messi kwenda Florida, US na kuacha deal la kwenda Saudi Arabia, lakini inawezekana kuna kitu alishaona kinakuja.
 
Starehe ni sehemu ya maisha ya binaadam na ndivyo Mungu alivyotuumba, ukitaka kwenda kinyume cha hapo lazima utashindwa tu.

Hata waarabu wenyewe wanakimbilia nchi za magharibi kwa wingi kwa sababu tu ya dhana hiyo
 
Fedha siyo kila kitu. Waarabu wanapenda mno sifa na ufahari. Hili la kutumia fedha kununua umaarufu wa mpira China limemshinda. Umaarufu wa ligi unaletwa na wingi wa mashabiki na siyo wachezaji maarufu.
Mchina alianzisha mfumo wa kuwatoza kodi zaidi ya 60% kwenye malipo mishahara yao wakaamua kuhamia kwa waarabu.
 
Back
Top Bottom