Simba vs Al Ahly ni mechi ya kawaida sana ila tukio si la kawaida

Smart codetz

Senior Member
Jan 25, 2023
180
703
Hizi taarifa za kuwa Al Ahly wamegomea wachezaji wao muhimu kujiunga na timu zao za taifa zinanipa ukakasi kidogo, nimemwona ALIOU DIENG Kiungo wao tegemezi ameenda kwenye timu ya taifa nchini Mali na ameripoti kambini, Misri wenyewe wameita wachezaji watano kutoka Al Ahly na hata Golikipa wao ambaye ni Nahodha wao yumo kikosini na wanaendelea na mazoezi huko Falme za Kiarabu tena ni nje ya Afrika kabisa.

Dear Brothers and Sisters inapofika kalenda ya michuano ya kimataifa, Mchezaji ni mali ya Shirikisho! Klabu hutumiwa barua za uthibitisho wa wachezaji kuitwa, klabu haiwezi kuzuia Mchezaji kuondoka hata iwe na nguvu kiasi gani isipokuwa sababu maalum haswa Majeraha ama majanga yasiyozuilika au Mchezaji akatae kujiunga na timu.

Nje na hapo klabu inaweza kuliomba shirikisho kuwaachia wachezaji endapo watakubaliana, nje na hapo ni rungu zito kutoka kwa FIFA, hivyo akibaki Mchezaji sio kwamba kazuiliwa bali wamekubaliana, ndio maana hata Manchester United kipindi cha Fergie alikataa sana Afrika kisa AFCON kuwa January.

Mohamed Salah, Sadio Mane walikuwa muhimu sana Liverpool ila wakati wa AFCON nini kinatokea? Wachezaji duniani kote wengine wanasafiri nusu ya dunia kwende kutumikia mataifa yao! Kalenda ya Kimataifa ina heshima yake! Labda kuwe na makubaliano.

Kwa mfano Simba inaweza kuwaomba TFF idhini ya Wachezaji, wakikubali TFF na wakibariki wanawachukua ila huwezi kuwazuia wasiende National Team! Hii ni mechi ya kawaida kama mechi nyingine za mpira wa miguu, ukubwa ni tukio tu ila mechi ni ile ile tu, Wachezaji wa timu zote wameshajiandaa just a normal football game.

20231011_151054.jpg
 
Kiufupi Simba kucheza na waarabu c jambo lakushangaza Tena n ktu Cha kawaidaa atakae jianda vyema ndio atashindaa..

Hakuna under dog hapo n wababe wanakutana...
 
Hizi taarifa za kuwa Al Ahly wamegomea wachezaji wao muhimu kujiunga na timu zao za taifa zinanipa ukakasi kidogo, nimemwona ALIOU DIENG Kiungo wao tegemezi ameenda kwenye timu ya taifa nchini Mali na ameripoti kambini, Misri wenyewe wameita wachezaji watano kutoka Al Ahly na hata Golikipa wao ambaye ni Nahodha wao yumo kikosini na wanaendelea na mazoezi huko Falme za Kiarabu tena ni nje ya Afrika kabisa.

Dear Brothers and Sisters inapofika kalenda ya michuano ya kimataifa, Mchezaji ni mali ya Shirikisho! Klabu hutumiwa barua za uthibitisho wa wachezaji kuitwa, klabu haiwezi kuzuia Mchezaji kuondoka hata iwe na nguvu kiasi gani isipokuwa sababu maalum haswa Majeraha ama majanga yasiyozuilika au Mchezaji akatae kujiunga na timu.

Nje na hapo klabu inaweza kuliomba shirikisho kuwaachia wachezaji endapo watakubaliana, nje na hapo ni rungu zito kutoka kwa FIFA, hivyo akibaki Mchezaji sio kwamba kazuiliwa bali wamekubaliana, ndio maana hata Manchester United kipindi cha Fergie alikataa sana Afrika kisa AFCON kuwa January.

Mohamed Salah, Sadio Mane walikuwa muhimu sana Liverpool ila wakati wa AFCON nini kinatokea? Wachezaji duniani kote wengine wanasafiri nusu ya dunia kwende kutumikia mataifa yao! Kalenda ya Kimataifa ina heshima yake! Labda kuwe na makubaliano.

Kwa mfano Simba inaweza kuwaomba TFF idhini ya Wachezaji, wakikubali TFF na wakibariki wanawachukua ila huwezi kuwazuia wasiende National Team! Hii ni mechi ya kawaida kama mechi nyingine za mpira wa miguu, ukubwa ni tukio tu ila mechi ni ile ile tu, Wachezaji wa timu zote wameshajiandaa just a normal football game.

View attachment 2778786
Shida sio mechi ya kawaida ila fitness level ya wachezaji kwasababu watakuwa na fatigue na hilo ndio la msingi la kuangalia halafu mechi zenyewe ni friends mechi.
 
Kwba unataka kuniambia jamaa wamezusha timu pinzani imewapiga marufuku wachezaji wake kwa sababu wana mechi kwa Mkapa?
 
Back
Top Bottom