KKKT na mtego kwenye msiba wa Mengi

KKKT na mtego kwenye msiba wa Mengi

Ndugu wanataka wamalize haraka haraka waanze kupambana na jack
Lakini nashangaa historia ya marehemu wanasema kaacha watoto 4 na mjane mmoja wakati watoto wa marehemu nasikia hawamtambui jack
Kutokana na Ratiba waliyotoa familia,hapa Dar es Salaam hatapelekwa kanisani pale Azania Front.
 
Zipo.
RC by a permit from the Pope but it is really a very long process
RC kuna annulment(ndoa kubatilishwa) zamani ilikuwa inafanywa na Pope tu siku hizi migogoro ya ndoa inaanza kusikilizwa ngazi ya Parokia mpaka jimbo na ndoa inabatilishwa na Askofu wa jimbo, hayo mambo ya kibali kutoka Roma kwa Papa ni ya kizamani... Ila mpaka ndoa ibatilishwe kuwe na sababu za kutosha na ushahidi unaojitosheleza kwamba hiyo ndoa haikupaswa kufungwa tangu mwanzo
 
Ndugu wanataka wamalize haraka haraka waanze kupambana na jack
Lakini nashangaa historia ya marehemu wanasema kaacha watoto 4 na mjane mmoja wakati watoto wa marehemu nasikia hawamtambui jack
Ni kweli kaacha watoto wa 4 na mjane mmoja. Watoto 2 alizaa na marehemu mke wa kwanza na watoto wa 2 alizaa na mjane wa sasa. Jumla watoto wa 4 na mjane mmoja.
 
Nasubiri kumsikia Askofu Malasusa akimtaja Jack kama mke,Askofu Shoo akifanya vile vile kule machame. Ndo tutajua watamtumikia Yesu au Mabilionea wa hapa duniani.
Tena huyu shoo anayejidai Ana misimamo
Tunamsubiri machame,muhudumu ongeza glass [emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23]
 
Ndugu wanataka wamalize haraka haraka waanze kupambana na jack
Lakini nashangaa historia ya marehemu wanasema kaacha watoto 4 na mjane mmoja wakati watoto wa marehemu nasikia hawamtambui jack
Jack analo huyu
Ajipangee,Mali ya mangi hailiwi hovyoo aiseeh babanguuu
 
Kama inavyofahamika katika kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania ,ndoa inayotambulika ni moja tu hadi kifo kitakapowatenganisha.

Mzee Mengi ambaye alikuwa ni muumini wa kanisa la kilutheri Tanzania na katika uhai wake inasemekana alifunga ndoa nyingine na Jack wakati huo huo Mama Mercy Mengi alikuwa bado yupo hai.

Je Mengi atazikwa na kanisa la kilutheri ,kikristo? Je kanisa litamtambua Jack kama mke wa marehemu? Kiukweli huu ni mtego na nightmare kwa kanisa la kilutheri.
Either kwa kutokuelewa au umeamua kupotosha kwa makusudi kabisa.
Naomba nikufahamishe kwa ufupi tu;
1. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri halina utaratibu wake binafsi kuhusu mambo ya ndoa. Linafuata taratibu za mamlaka husika lakini na namna neno la Mungu linavyosema katika Biblia Takatifu.
2. Vinginevyo uwe umesoma Biblia kwa kumeza, na ambapo Biblia hiyo haitumiwi na KKKT peke yake, pia makanisa mengine huitumia, Kipo kigezo ambacho kinakuruhusu kuvunja ndoa na kinakubalika kibiblia na kuruhusu ndoa mpya.
3. Sina hakika kama unajua sababu ya Dr. Mengi kufunga ndoa mpya baada ya kuachana na Mkewe wa kwanza. Lakini kama yaweza kuwa ni kwa sababu zilizotajwa na Biblia, then Dr. Mengi atazikwa kama Mfuasi wa Kristo.

Lakini pia niruhusu kukosolewa kama ndoa yake mpya haitambuliki Kibiblia.
 
Huwa KKKT viongozi wa Kanisa wanatia AIBU kwa kuwakumbatia marehemu wenye pesa au cheo au hadhi fulani katika jamii. Nawakumbusha tu KKKT , MUNGU wetu ni mtakatifu na hana upendeleo; mbele zake sisi wote ni sawa na haangalii hata sura ya mtu.Pasipo utakatifu hakuna atakayemwona Mungu. Nilihama huko baada ya kuokoka miaka 20 sasa. NENO la Mungu walishatia MAJI siku nyingi. Watatafuta mistari ya kuhalallisha chochote ili mradi chombo cha sadaka kitafurika.
Muogopeni MUNGU WETU HADHIHAKIWI, mtavuna nmlichopanda siku ya mwisho.
PASIPO UTAKATIFU HAKUNA MTU ATAMWONA MUNGU.
Hakika mkuu umenena
 
Roho iko ndani ya Mwili huwezi kuvitenganisha, Hapa ni NENO la MUngu katika Biblia linasemaje? Hakuna kwenda kulia au kushoto. mwenye Mbingu ni mmoja tuu. =MUNGU
Roho ikiwa ndani ya mwili hakuna mauti,na kama hakuna mauti hukumu yatoka wapi?
 
The old Rules are now intergrated by Globalization and Internationalization,Religion and Culture are within the Line.
 
Sokoine sijui alizikwaje,wanaojua watatusaidia,Hao wote ulowataja hapo juu walioa wake wengi sawa,Ila baada Ya Yesu kuja yote hayo yakavunjwa. Mke mmoja mme mmoja mpaka kifo kitakapowatenganisha.
Yesu hakuja kutengua torati, hakuna kifungu clear kwenye Bible kinachokataza wake wengi , hata Yesu alipoulizwa swali hilo hakujibu kwa kukataza, bali alisema Mungu aliruhusu kwa tamaa za binadamu, ila yeye alimuumba Adamu na Hawa.

Hata Mzee wa upako aliwahi hoji hii kwamba ni wapi Bible imekataza wake wengi
 
Yesu hakuja kutengua torati, hakuna kifungu clear kwenye Bible kinachokataza wake wengi , hata Yesu alipoulizwa swali hilo hakujibu kwa kukataza, bali alisema Mungu aliruhusu kwa tamaa za binadamu, ila yeye alimuumba Adamu na Hawa.

Hata Mzee wa upako aliwahi hoji hii kwamba ni wapi Bible imekataza wake wengi
Kasome agano jipya.
 
Back
Top Bottom