KKKT na mtego kwenye msiba wa Mengi

KKKT na mtego kwenye msiba wa Mengi

Kama inavyofahamika katika kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania ,ndoa inayotambulika ni moja tu hadi kifo kitakapowatenganisha.
Mzee Mengi ambaye alikuwa ni muumini wa kanisa la kilutheri Tanzania na katika uhai wake inasemekana alifunga ndoa nyingine na Jack wakati huo huo Mama Mercy Mengi alikuwa bado yupo hai.
Je Mengi atazikwa na kanisa la kilutheri ,kikristo?
Je kanisa litamtambua Jack kama mke wa marehemu?
Kiukweli huu ni mtego na nightmare kwa kanisa la kilutheri.
Kwani mama Mercy ndio mke wa kwanza wa Mengi?
 
Uzuri wa Mungu kwake kuna 2nd chances za kumwaga. Kama walirudi kundini kawaida tu.

Mwisho wa siku baada ya kufa ni hukumu. Inawezekana marehemu alitubu just before he died and that is good enough. Haya ya kuzika ni mbwembwe tu za wanaadamu
Kama alifanya yote hayo kuungama sawa,ila Jack aliemuoa wakati Mama Mercy Mengi akiwa hai itakuwaje? Tutaona.
 
alikuwa anazini. Kuoa mpaka baraka za Padre kanisani na si vinginevyo (ukiacha haya ya kiserikali). Mengi alikuwa anazini tu! Mzinifu na malaya celebrity
Nasubiri kumsikia Askofu Malasusa akimtaja Jack kama mke,Askofu Shoo akifanya vile vile kule machame. Ndo tutajua watamtumikia Yesu au Mabilionea wa hapa duniani.
 
Ibada inayo mpendeza Mungu ni kuishi vyema, kulisha wahitaji, kutoa sadaka, kusaidia yatima na wajane, kutembelea wagonjwa na wafungwa, haya Marehemu mzee wetu ameyafanya vyema, kuzikwa na padri askofu au mchungaji haimsaidii marehemu kuwekwa pema peponi hata siku moja., mbona wao mapadre wana lawiti watoto na wanazikana ndani ya makisa wengine ina maana wao ndio wanona ufalme wa Mungu?
 
Mkuu KKKT haina TAABU taabu ni baadhi ya VIONGOZI, kukimbia kanisa hukufanya jema maana hata huko kwa WALOKOLE si ndio wako kina KAKOBE ( tunakula mema ya nchi ikulu) kina LUSEKELO ( wanao tukana majirani wakiwa wamelwa kabisa) na wengine wengi.. Simama na BIBLIA ijue kweli nayo itakuweka huru.
Hatuongei DINI hapa wala MTU; mbinguni hatutaingia kwa dini hata kama ni ya kilokole; kule ni utakatifu sawasawa na NENO.
Una uwezo wa kushinda dhambi;ulevi , uzinzi, nyumba ndogo etc.
Watazika kwa heshima ZOTE; je mbele za Mungu ana heshima hiyo? Wewe pia ni mhanga wa DINI ; Okoka leo
 
Uzuri wa Mungu kwake kuna 2nd chances za kumwaga. Kama walirudi kundini kawaida tu.

Mwisho wa siku baada ya kufa ni hukumu. Inawezekana marehemu alitubu just before he died and that is good enough. Haya ya kuzika ni mbwembwe tu za wanaadamu
Ibaada ya mazishi ni stage muhimu sana katika maisha ya mkristo. Kwetu sisi wakristo.
 
Ibada inayo mpendeza Mungu ni kuishi vyema, kulisha wahitaji, kutoa sadaka, kusaidia yatima na wajane, kutembelea wagonjwa na wafungwa, haya Marehemu mzee wetu ameyafanya vyema, kuzikwa na padri askofu au mchungaji haimsaidii marehemu kuwekwa pema peponi hata siku moja., mbona wao mapadre wana lawiti watoto na wanazikana ndani ya makisa wengine ina maana wao ndio wanona ufalme wa Mungu?
Two wrongs do not make it right.
 
Kama inavyofahamika katika kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania ,ndoa inayotambulika ni moja tu hadi kifo kitakapowatenganisha. Mzee Mengi ambaye alikuwa ni muumini wa kanisa la kilutheri Tanzania na katika uhai wake inasemekana alifunga ndoa nyingine na Jack wakati huo huo Mama Mercy Mengi alikuwa bado yupo hai. Je Mengi atazikwa na kanisa la kilutheri ,kikristo?
Je kanisa litamtambua Jack kama mke wa marehemu?
Kiukweli huu ni mtego na nightmare kwa kanisa la kilutheri.
Wenzako tayari wamepanga safu.
 
Two wrongs do not make it right.
Hata Ruge walimsusa kuzika lakini kanisani humo humo kumefanyika ibada ya shukrani ya marehemu Ruge, some times wakiristu tuache kuhukumu marehemu.
 
Ibada inayo mpendeza Mungu ni kuishi vyema, kulisha wahitaji, kutoa sadaka, kusaidia yatima na wajane, kutembelea wagonjwa na wafungwa, haya Marehemu mzee wetu ameyafanya vyema, kuzikwa na padri askofu au mchungaji haimsaidii marehemu kuwekwa pema peponi hata siku moja., mbona wao mapadre wana lawiti watoto na wanazikana ndani ya makisa wengine ina maana wao ndio wanona ufalme wa Mungu?
Udhaifu wa mapadre hauhalalishi maovu ya wengine! Wao watahukumiwa kwa makosa yao ya kulawiti , naye atahukumiwa kwa uzinifu pamoja na kutoa sadaka kwa wingi. Hakuna sheria ya kanisa inayosema ukitoa sadaka, kuwasaidia masikini etc basi you are exempted from adhabu kwa makosa yako! Victoire
 
Sokoine sijui alizikwaje,wanaojua watatusaidia,Hao wote ulowataja hapo juu walioa wake wengi sawa,Ila baada Ya Yesu kuja yote hayo yakavunjwa. Mke mmoja mme mmoja mpaka kifo kitakapowatenganisha.

Yalivunjwa vipi wakati yesu hakuoa kabisa? Basi msioe
 
Victoire, kuna taratibu. Alitubu? Aliungama? Sijui taratibu za KKKT lkn RC siyo rahisi kihivyo!
KKKT wao mtu HURUDI KUNDINI, yaani ukizaa nje ya ndoa unakwenda kusimama mbele ya kanisa unasalishwa sala ya toba unarudi kundini, maisha yana songa. Ila tangu nimekua sijaona MWANAUME alierudishwa kundini nilimuuliza mama angu ambae ni mzee wa kanisa, ina maa hawa wanawake wana zaa peke yao? Maana mwanaume aishi poa tu kama hajafanya chochote akakosa jibu.. Makanisa yanamambo mengi ya ajabu.
 
Huwa KKKT viongozi wa Kanisa wanatia AIBU kwa kuwakumbatia marehemu wenye pesa au cheo au hadhi fulani katika jamii. Nawakumbusha tu KKKT , MUNGU wetu ni mtakatifu na hana upendeleo; mbele zake sisi wote ni sawa na haangalii hata sura ya mtu.Pasipo utakatifu hakuna atakayemwona Mungu. Nilihama huko baada ya kuokoka miaka 20 sasa. NENO la Mungu walishatia MAJI siku nyingi. Watatafuta mistari ya kuhalallisha chochote ili mradi chombo cha sadaka kitafurika.
Muogopeni MUNGU WETU HADHIHAKIWI, mtavuna nmlichopanda siku ya mwisho.
PASIPO UTAKATIFU HAKUNA MTU ATAMWONA MUNGU.
Mbona mnaanza ramli mapema? Mwenye kuhukumu ni Mungu pekee na hakuna kosa lisilosameheka mbele zake. Hakuna siku wala muda wa kusamehe, hakuna kuwahi wala kuchelewa. Kumbuka mfano wa yule mnyang'anyi pale msalabani,muhimu ni toba basi
 
Back
Top Bottom