KKKT Msikubali CCM iwageuze BAKWATA

KKKT Msikubali CCM iwageuze BAKWATA

Mkuu TAI DUME, shukrani kwa mchango wako mzuri wenye mtazamo wa kihistoria na kimaandiko. Kwenye hoja yako ya msingi upo sahihi kwa asilimia kubwa: Yesu hakuwa mwanamapinduzi wa kisiasa aliyetaka kupindua Dola ya Roma kwa mtindo wa msituni au kijeshi. Alilenga mapinduzi ya kiroho. Hata hivyo, unachukulia mambo juujuu sana na unashindwa kuelewa maana halisi ya uanaharakati (activism) wa kimkakati. Ili kuweka kumbukumbu sawa na kuongeza nyama kwenye mjadala huu wa JF, kuna maeneo madogo ya kihistoria na kimaandiko yanayohitaji marekebisho kidogo (fine-tuning):
Kwanza, ulipomchanganya Yesu na Yohana Mbatizaji. Pale uliposema Yesu aliwaasa askari wasichukue kodi zaidi ya kiwango (rushwa), hapo umempa Yesu mistari ya Yohana Mbatizaji. Kimaandiko katika Luka 3:14, ni Yohana ndiye aliyewaambia askari waliomwendea: "Msidhulumu mtu, wala msishtaki kwa uongo; tena mtolewe na mishahara yenu."
Pili, kuhusu mtego wa kodi (Je, alitambua mamlaka ya Roma kwa 100%?). Siyo kwa asilimia mia moja mkuu. Ule mtego wa kulipa kodi kwa Kaisari haukuwa swali la kawaida tu la darasani kama unavyofikiria wewe hapo. Huo ulikuwa ni mtego mzito wa kijasusi na kisheria uliolenga kumgombanisha Yesu na Serikali ya Kirumi ili iwe rahisi kumfungulia mashtaka ya uhaini na kumnyonga. Waliomtega walijua fika: Kama Yesu angesema "Msilipe kodi," wangemkaba koo na kumpeleka kwa Gavana Pilato kama muasi wa serikali. Na kama angesema "Lipeni kodi," wananchi wa kawaida (raia wanyonge waliokuwa wananyonywa na kodi hizo za kikoloni) wangemwona Yesu ni msaliti na kibaraka, na harakati zake za kuwatetea zingekufa siku hiyo hiyo.
Akili kubwa ya uanaharakati wa kiwango cha juu (genius activism) wa Yesu ulionekana pale alipoutategua ule mtego wao kwa kuwauliza wao wenyewe sarafu ina sura na anwani ya nani. Walipomwambia ni vya Kaisari, akawapiga na ile punchline ya karne katika Mathayo 22:21: "Basi, mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu." Kaisari alijiona yeye ni Mungu na kila kitu ni chake. Yesu kwa kutenganisha vitu vya Kaisari na vya Mungu, aliweka mipaka ya utii. Alimaanisha kuwa utii mkuu (dhamiri, ibada, na utu wa mtu) ni mali ya Mungu pekee, siyo ya serikali dhalimu ya Roma. Hapo aliwanyamazisha watesi wake, akalinda harakati zake mitaani, na akaonyesha kuwa serikali haina haki ya kuwadhulumu au kuwanyonga raia wake.
Tatu, kosa la kusulubiwa lilikuwa la kisiasa (Uhaini). Ni kweli viongozi wa Kiyahudi walimchukia kwa masuala ya kidini. Lakini walipompeleka kwa Pilato, walijua Pilato (Kama Gavana wa Kirumi) hawezi kumhukumu mtu kifo kwa makosa ya kidini ya Kiyahudi. Ndiyo maana walibadili mashtaka mbele ya Pilato yakawa ya kisiasa, wakidai Yesu anajifanya "Mfalme" na anazuia watu kulipa kodi (Luka 23:2). Roma ilimsulubisha Yesu kwa kosa la Uhaini (Sedition/Treason) dhidi ya Kaisari, na ndiyo maana msalabani wakaandika shtaka lake la kisiasa: "Mfalme wa Wayahudi."
Hitimisho:
Uko sahihi kabisa kwamba Yesu hakuwa mwanasiasa wa mrengo wa kushoto aliyetaka kuiondoa Roma kimwili ili Israel iwe huru. Lakini mafundisho na harakati zake zilikuwa hatari sana kwa watawala kwa sababu yalifundisha kwamba mamlaka ya Mungu yapo juu ya mamlaka yote ya kidunia. Kuwa mwanaharakati sio kuwa mjinga wa kukurupuka na fujo za kujipeleka gerezani kabla ya wakati. Yesu alikuwa mwanaharakati mwenye akili nyingi sana (strategic activist) aliyepambana na mifumo dhalimu kwa akili kubwa na akawashinda wote waliotaka kumziba mdomo!
Nawasilisha, Mkuu!

Habari mkuu.

Kwanza hilo jina la "Ifoza" linanikumbusha sekondary ya ifakara tulikuwa tumeipa nickname ya jina Hilo

Pili, Asante kwa uchanganuzi wako wa kina. Nikubaliane na wewe ni kweli Kuna mahali nimemlisha Yesu maneno ya Yohana. Hata hivyo nikiri tu umedadavua kwa kina sana.

Thanks mkuu
 
Asante sana Mkuu TAI DUME kwa majibu yako ya kiungwana na kistaarabu. Hakika mijadala ya namna hii ndiyo inayofanya jukwaa letu la JF kuwa la kipekee na lenye kujenga upeo mkubwa wa kifikra. Hakuna anayejua kila kitu, na sote tupo hapa kupeana maarifa na kujifunza kila siku.
Kuhusu hilo jina la Ifoza, umepatia kabisa kuwa linabeba kumbukumbu za kule Ifakara na umenifurahisha kuona unaijua hiyo nickname.
Sasa kwa kuwa umegusia habari za sekondari ya kule Ifakara na kuonyesha unajua kisa chake, na mimi naomba nikuulize swali moja dogo tu mkuu ili tuchagize kidogo kumbukumbu za pande hizo: hivi hiyo shule unayoiongelea wewe ni Michipi ama? Funguka kidogo mkuu tuone kama kweli unapakumbuka vizuri!
Pia, asante kwa kukubali marekebisho yale ya kimaandiko, ni ishara ya ukomavu mkubwa sana wa kifikra.
Nawasilisha, mkuu!
 
Kijana wa Ifoza umeitaja Michipi umenikumbusha Ifakara. Pamoja na joto lake lakini kumekaa kimji sana.

Sasa kule Lumemo ndiyo chuo kikuu cha matapeli Tanzania. TCRA wanasema kati ya matapeli kumi wa mitandaoni, tisa wanatoka Ifakara.

Kwa maana nyingine Ifakara ndiyo makao Mkuu ya utapeli wa mitandaoni na inawezekana wana IFOZA wenzako pia ni sehemu ya mastering wa hiyo shughuli.
 
Mkuu Allen Kilewella, shukrani sana kwa mchango wako na kuleta kumbukumbu hizi tamu za Ifakara! Hakika umegusa popote pale. Pamoja na joto lake, kile kijiwe kimekaa kimji sana tangu zamani.
Hata hivyo mkuu, kwenye hili la Lumemo na ripoti ya TCRA, naomba nikuwekee "fine-tuning" kidogo kulinda heshima ya Wana-Ifoza na wazawa wa Ifakara kwa ujumla.
Hapana kiongozi, Ifakara haijawahi kuwa mji wa matapeli wa asili. Kiuhalisia, Ifakara ni kama Dar es Salaam tu; "wakuja" (watu wanaokuja kutoka mikoa mingine) ndio wamepaharibu baada ya kumiminika pale kutafuta fursa za kibiashara, kilimo cha mpunga, na misitu. Hawa matapeli wa mitandao unaowasikia Lumemo wengi wao ni wageni waliohamia pale kwa sababu ya mzunguko mkubwa wa fedha, siyo Wana-Ifoza wazawa!
Umenikumbusha mbali sana ulipotaja enzi za ukuaji wa mji wetu. Ni kweli kulikuwa na wahuni na miaka hiyo mji ulikuwa unaitwa kabisa "Manzese Ndogo". Nakumbuka vizuri kabisa, ukishuka usiku wa manane kwenye mabasi yale ya Myowela, TRC, au Dar Oyee, madereva wenyewe walikuwa wanatoa tahadhari na kukushauri: "Kama huna mwenyeji hapa, lala humu humu kwenye basi mpaka kuku wakicheza asubuhi!"
Hiyo ndiyo ilikuwa Ifakara yetu bwana; mji wenye harakati nyingi, changamoto zake, lakini pia ukarimu mkubwa kabla haujavamiwa na wimbi hili la kiteknolojia la akina Lumemo.
Nawasilisha mkuu, na karibu tena Ifoza!
 
Hii hoja ya "WAKUJA" kuwa ndiyo wanaoendesha kiwanda cha matapeli pale Lumemo na kwa sehemu Lipangalala inaweza kuwa na mashiko... Lakini mbona wenyeji hawapambani na hali hiyo?

Miaka kama mitano iliyopita kilizuka kikundi cha waporaji wakijiita "changa ule" lakini wenyeji walipambana nacho wakakisambaratisha. Hili la utapeli vipi?
 
Unataka wavuvi na wakulima wapambane na cyber kiongozi?
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ni chombo kinachosimamia maslahi ya waislamu Tanzania lakini lisilokubalika na baadhi ya kizazi kipya cha waislamu.

Vijana wengi wa kiislamu hulishutumu Baraza hilo kutumiwa kisiasa kufanikisha maslahi ya CCM.

Miaka ya hivi Karibuni BAKWATA walibadili mfumo wao wa kupata masheikh wa mikoa kutoka masheikh wa kuchaguliwa na waislamu wa mkoa husika hadi masheikh wa kuteuliwa toka makao Mkuu ya BAKWATA.

Mfumo huo mpya ambao umelipa mamlaka Baraza la maulamaa kuteua masheikh wa mikoa, umeleta hofu na sintofahamu.

Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT) na lenyewe liko kwenye harakati za kubadili Katiba ya kanisa hilo kumpa mamlaka Mkuu wa kanisa mamlaka ya kuhamisha na kuteua Maaskofu.

Nasikitika kuwaambia KKKT mpango wa kubadili Katiba yao na kumpa mamlaka Mkuu wa kanisa kuteua na kuhamisha Maaskofu, umekaa kisiasa zaidi na utawagharimu.

Siku Katiba hiyo ikipitishwa, ndiyo KKKT itaanza kutumiwa kisiasa na CCM. Hivi Maaskofu wenye fikra huru kama Bagonza watasalimika kweli?
Carrot wansyo onyeshwa mbele yao ni kuwa safari hii ni wao sio TEC tena kwenye urais, na watu kama Shoo na Malasusa rahisi kufika bei.
 
Unataka wavuvi na wakulima wapambane na cyber kiongozi?
Nimekuwa pale ni kweli wakuja wapo lakini na wenyeji wapo pia wa kutosha.

Kuna kijana mwaka huu anamaliza sekondari nadhani pale Kwa Shungu, naambiwa kanunnua Pikipiki kwa utapeli wa mitandaoni wenyewe wanaita "Halohalo".

Sasa kwenye viwanja vya kutumia kama kule ze Place na kwingineko hao wavuvi na wakulima si wanawajua kwa majina hao matapeli, wanafanya nini kuwazuia wasichafue taswira ya mji wao?
 
Asante sana Mkuu TAI DUME kwa majibu yako ya kiungwana na kistaarabu. Hakika mijadala ya namna hii ndiyo inayofanya jukwaa letu la JF kuwa la kipekee na lenye kujenga upeo mkubwa wa kifikra. Hakuna anayejua kila kitu, na sote tupo hapa kupeana maarifa na kujifunza kila siku.
Kuhusu hilo jina la Ifoza, umepatia kabisa kuwa linabeba kumbukumbu za kule Ifakara na umenifurahisha kuona unaijua hiyo nickname.
Sasa kwa kuwa umegusia habari za sekondari ya kule Ifakara na kuonyesha unajua kisa chake, na mimi naomba nikuulize swali moja dogo tu mkuu ili tuchagize kidogo kumbukumbu za pande hizo: hivi hiyo shule unayoiongelea wewe ni Michipi ama? Funguka kidogo mkuu tuone kama kweli unapakumbuka vizuri!
Pia, asante kwa kukubali marekebisho yale ya kimaandiko, ni ishara ya ukomavu mkubwa sana wa kifikra.
Nawasilisha, mkuu!
Sorry mkuu nimechelewa kukujibu hili. Ifoza ninayoizungumzia ni hiyo hiyo machipi iliyoko karibu na kining'ina hahaha.

Mimi nilipita pale nikiwa intake ya kwanza form five -ndio waanzilishi.
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ni chombo kinachosimamia maslahi ya waislamu Tanzania lakini lisilokubalika na baadhi ya kizazi kipya cha waislamu.

Vijana wengi wa kiislamu hulishutumu Baraza hilo kutumiwa kisiasa kufanikisha maslahi ya CCM.

Miaka ya hivi Karibuni BAKWATA walibadili mfumo wao wa kupata masheikh wa mikoa kutoka masheikh wa kuchaguliwa na waislamu wa mkoa husika hadi masheikh wa kuteuliwa toka makao Mkuu ya BAKWATA.

Mfumo huo mpya ambao umelipa mamlaka Baraza la maulamaa kuteua masheikh wa mikoa, umeleta hofu na sintofahamu.

Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT) na lenyewe liko kwenye harakati za kubadili Katiba ya kanisa hilo kumpa mamlaka Mkuu wa kanisa mamlaka ya kuhamisha na kuteua Maaskofu.

Nasikitika kuwaambia KKKT mpango wa kubadili Katiba yao na kumpa mamlaka Mkuu wa kanisa kuteua na kuhamisha Maaskofu, umekaa kisiasa zaidi na utawagharimu.

Siku Katiba hiyo ikipitishwa, ndiyo KKKT itaanza kutumiwa kisiasa na CCM. Hivi Maaskofu wenye fikra huru kama Bagonza watasalimika kweli?
alex Gehaz Malasusa kisha mkaribisha Shetani kwenye mahali pa takatifu.
 
January 2021 nipo zangu Ibadani (KKKT )ghafla Askofu akasema CHADEMA walishindwa na CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 kwa kuwa CHADEMA mwaka 2019 wakati wa COVID 19 walikaa upande wa shetani.

Nikajiuliza kama yule Askofu (siyo Malalsusa) hakuona dhuluma iliyofanywa na CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2020?
 
Aisle... inasikitisha
 
Back
Top Bottom