Happi awaomba TEC wawaombee Chadema wakubali maridhiano.

Happi awaomba TEC wawaombee Chadema wakubali maridhiano.

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,448
Reaction score
46,216
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukutana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki kupitia Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Ikulu.

Akizungumza leo Agosti 12, 2026 na Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wa Kilosa Mjini, Mkoani Morogoro, Hapi amewataka Maaskofu hao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili waondokane na pepo ya ukaidi na kuitikia wito wa kwenda kwenye meza ya maridhiano.

Hapi amesema Rais amekuwa akitoa nafasi kwa Vyama vya Siasa kukutana na kujadiliana kuhusu masuala ya Taifa, lakini CHADEMA hawajaitikia wito huo.

Amesema TEC imeonyesha mfano kwa kuitikia mwaliko wa Rais na kukutana naye, hivyo amewaomba Maaskofu kutumia nafasi yao kuwaombea Viongozi wa CHADEMA ili nao wafunguke na kuona umuhimu wa mazungumzo.

“Maaskofu TEC, waombeeni CHADEMA, Mungu awasaidie pepo ya ukaidi iwatoke, waende kwenye meza ya maridhiano,” amesema Hapi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom