Kizungumkuti Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizungumkuti Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ngoshwe, Jan 19, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hapa Watanzania ni kama tunamtafuta mchawi nani wakati wote tunajua kuwa haya yote yanayotokea yanafanywa na watanzania wenzetu ambao tunaishi nao hapa hapa nchini na tunaweza kuwawajibisha kwa nia moja au nyingine kutokana na dhamana walizinazo. Kama kweli hawana hisa yoyote kwa Dowans, ya nini kuonekana wakiumiza vichwa vyao kutaka Dowans ilipwe? Ni makampuni mangapi ya kizalendo au ya kigeni ambayo yameshinda kesi dhidi ya Serikali na mpaka leo hayajalipwa? Kuna nini kwa hili la Dowans?

  (i) Inawezekanaje Kampuni ya Kigeni au raia wa nje akasajili kampuni hapa nchi pasipokuwa na mkono wa Mtanzania eti hata wakili tu wa kugonga mihuri nyaraka hayupo kiasi cha kutufanya tusijue Dowans ni ya kina nani?

  (ii) inawezekanaje Msajili wa Makampuni akawa kimya na kumwachia mtu kama Mhe. Ngeleja kutuziba mdomo watanzania kwa kujifanya anajua wamiliki wa Dowans wanati yeye si Bosi wa BRELA??

  (iii) Iweje Mhe. Ngeleja akasimama na kuwaeleza wananchi tuilipe Dowans kutokana na kesi ambayo inaihusu Tanesco wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco yupo??

  (iv) Imekuwaje Mwanasheria Mkuu wa Serikali akawa kimya na kuwaachia mawakili binafsi wa Rex Attorney kulishauri na kuliwakilisha Mahakamani shirika la Umma ilihali ikijulikana tokea mwanzo kuwa kesi husika ni nyeti kwa Serikali?? (tukumbuke kuwa Taarifa ya Dr. Mwakyembe ilibainisha mapungufu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu usimimizi wa Suala la Umeme wa dharura na mkataba na kampuni ya Richmond LC. Hata hivyo, uzembe huo umeendelea kujitokeza mpaka sasa ambapo Mwanasheria Mkuu badala ya kuitetea Serikali analazimisha tuliilipe Dowans mabilioni ya shilingi.)

  (v) Mawakili kama akina FUngamtama wanahisa gani kwenye Dowans mpaka wakadiriki kusimama mbele ya wanatanzania na kuda tuilipe Dowans wakati yapo makampuni kibao ya kizalendo ambayo yameshinda kesi dhidi ya Serikali muda mrefu na hayajalipwa (Ikumbukwe kesi kama ile ya Valambia, Ubomoaji wa Maghorofa ya Masaki nk).

  (vi) Kama kuna uhalali wowote wa kuilipa Dowans, kwa nini uwepo wa kesi hii haukufahamisha kwa watanzania kabla hukumu haijatolewa ili kuwezesha haki kutendeka kwa fedha za walipa kodi kama ilivyokuwa katika kesi ya BIWATER/CITY WATER??.
   
 2. SHILINDE

  SHILINDE Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 23, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  kwa nini tunarumbana, si tusubiri appeal ya LHRC.
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii everyone,this information still disturbs the mind.Is it worthy to pay Dowans after all this information,l dont think so.The Company managed to get contract with Tanesco through fraud and misrepresentation.So in that scenario what is the fate of the alleged contract still valid,l dont think so.Kindly enjoy the reading bellow.*This is Dowans HQ in Costa Rica - (Pictures)Hi everyone; I'm back, wounded and limping but still kicking LOL.Numerous trips I have made since I reported to you about the thenpending ITV saga. With some of my "little ones" we were able to travelextensively through Europe, US and Costa Rica as well as making somecontacts in Singapore. What we have discovered is nothing less thanshocking!I visited the so called Headquarters of Dowans S.A in Costa Rica andhad access to relevant organs that deal with businesses there. Some ofthe things we were able to raise with the Costa Rican gvt and the USgvt were addressed in the meeting in London when the major economicpowers addressed the current economic crisis. If you can recall, CostaRica was named as one of the countries that unless they change theirlegal framework concerning offshore accounts they will be blacklisted.We are glad as we left the Costa Rican gvt decided to change some ofthe laws and regulations. We are eternally grateful to those peoplewho made the trip worthy taking and fruitful.We learned a number of things about Dowans:a. If It was registered in Costa Rica then simply as a briefcasecompany. Due to the legal and procedural laxity that existed then inCosta Rica it was very easy for some shady businessmen to appoint a"lawyer" who would act as their middleman and a point of contacts.After our extensive investigations through different lawyersorganisations we were unable to find the lawyer involved with Dowansnor his/her address or whereabout. One authority told us confidentlythat such a person does not exist except in papers.b. We visited the offices of Dowans Costa Rica as indicated in theirBRELA forms. In these forms Dowans (T) has listed two companies as oneof the major shareholders, one is Dowans S.A of AVENIDA DE LA ROSAS 3JCALLE BLANCOS, 1150 sAN JOSE, COSTA RICA and the other company is amajor Singaporean company and world world leader in Port Management..Portek Internation of 20 HARBOUR DRIVE #02-01 PSA VISTA, SINGAPORE 117612 (Portek International Limited).The later (Portek) assured us with no qualifications that it has noshare, none whatsoever in the Dowans (T). And it is not involved inenergy products in Tanzania. The only project they had was the sale ofsome logistics equipments to TICTIS. This can be verified easily bycontacting: Tel: (65) - 6873 1114 or Fax: (65) - 6873 2224The former (Dowans S.A) has been a pain in some places better leftunmentioned. The report of our investigation team under my ableleadership came to this conclusion "there is no such a business inCosta Rica operating under that name".Indeed my visit to the address mentioned in BRELA forms led me to afree trade zone. A check of the business located there revealed nosuch company. After combing public and private records such as theNational Registry of Costa Rica, Telephone, electricity, automobilesand database searches all revealed nothing. Not about Bernal ZamoraAlce (the "lawyer") nor the company itself.Our conclusions then are as follows:a. Dowans entered into Tanzania under false pretenses, providingmisleading information and therefore has engaged in fraud.b. Due that fact in a, Dowans in Tanzania was wrongly registered andits activity as a company had no legal basisc. Due to (a and b) Dowans lacks legal standing in our courts to askcompensation as an illegal entity operating illegally.d. The government should seize all of Dowans assets and take everybodywho was involved in enabling this company to enter into a contractwith Tanesco to a court of law for abusing their offices andauthority.We have finished the incredible work on Meremeta going back to thetime of Wemba Dia Wemba and the second Congo War. We have submittedour work to our commander of ideological battles to decide if he wouldpublish them or due to the explosive nature (no pun intended) of theallegations he would not publish in Cheche.After we bankrupted him he wants to charge a one time 25USD for theSpecial Edition of Cheche on Meremeta (good luck M!).It is the choice for the CCM MPs to continue to support their corruptgovernment or to take it to task and restore the rule of law. We hopea courageous CCM MP will bring the issue of Dowans to the floor of theNational Assembly and call for an independent inquiry to refute theallegations we have raised or confirm them. We believe such an inquirywill have more resources to dig more and do more than we did with ourvery limited budget.Thanks M for giving us another mission.

  We are ready to fly again.We humbly submit.

  View attachment The+Paradox+of+Procurement+Politics.pdf

  Fw: Dowans ni nani? - Wanabidii | Google Groups
   
 4. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jee gazeti hili litapata mgao, ikiwa wamiliki wa downs wakilipwa?
  waandishi wao hawana uchungu na nchi?
  Kwani kila ukisoma gazeti hilo utaona jinsi linavyosafisha downs licha ya wanaharakati na wanaccm wenye uchungu wanapinga
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwani wewe hujui? Ni gazeti la Rostum na amewaambia waandishi kuwa watapewa mgao wa Dowans.
   
 6. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hilo gazeti liko mtaani kwa ajenda ya kulinda maslahi ya fisadi papa RA ambate atachukua mzigo wote wa Dowans na kugawana na jamaa zake akina JK, Salva Rweye, EL, Karamagi. Cha kushangaza gazeti haliuzi nakala za kutosha kulipia garama za uendeshaji ikiwemo mishahara ya wafanyakazi lakini kila wiki liko mtaani kufagilia mafisadi. Wafanyakazi wa Rai kupata mshahara tarehe 40 ni kawaida tu
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,271
  Trophy Points: 280

  Kwa sababu mmiliki wa Dowans ni Dr Wilbroad Slaa, na doctor Slaa ana hisa kubwa kwenye magazeti ya Habari corporation( Rai).
   
 8. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,299
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Rai lipo pale kutetea maslahi ya Mafisadi. Hakuna tena taaluma pale, ukichukulia pia na hawa waandishi wetu form four ya point 30 na kozi ya uandishi wa habari ya miezi 6
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Unaishi nchi gani wewe unayetaka kujua sababu ya rai kuipigia debe dowans!! Hujui kuwa fisadi papa RA ndiye mmiliki wa dowans!!
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,117
  Trophy Points: 280
  Mpwa wangu, mbona hujauliza swali bali umeuliza jibu? hebu uliza swali ili upate jibu ila kwa hapo pigia mstari tu
   
 11. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
   
 12. n

  niweze JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunaona yote kila mahali ni shida. Nchi haina pesa ila CCM na magari mapya na nyumba za kifahari. Dowans wanaelekea kulipwa na jeuri Rostam anatuambia ajali chochote wananchi tunalala mika bure. Jk na CCM wanataka kuunda Tume ya Katiba baada ya kuiba uchaguzi.

  Machungu yapo na vilio ni vingi mahospitalini na nyumba nyingi Tanzania. Hakuna pesa wazazi kulisha familia zao na watoto wanabaki majumbani bila elimu. Waliofanikiwa kupata nafasi vyuoni hawapewi pesa za kutosha za masomo na wakimaliza hawana kazi. Sijui kingine kipi nimesahau....

  Ukitembelea bank kuu watoto wa viongozi ccm, wanamejaa tele wakilipwa pesa nyingi kwa kazi wasizo stahili. Ukiangalia maisha na utajili wa viongozi wa ccm utaanguka vilio kwamba walipata vipi hizo mali na pesa? Waliwezaje kujenga nyumba za thamani kubwa hivyo? Mikataba migodini, viwanda vilivyo taifishwa vya serikali na kuuzwa kwa faida na faida za uzalishaji imekwenda wapi? Mikopo inatolewa na serikali kuwezesha viwanda viendeshwe baada tu ya kununuliwa wapi ulisikia hii? Ukiuliza na kufuatilia kama mfanya kazi wa serikali, maisha wana kutishia na unanyimwa malipo...

  Tanzania ni Taifa Bovu Lote au Wananchi Hawataki Mapinduzi au Wakati Haujafika Tusubiri CCM Wamweke Pinda Kutupiga Misumari Mingine ya Miaka Kumi?
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hehehe, unajua gari kazi yake ni kuendeshwa hata korongoni linapita bila kulalama cha msingi dereva yupo salama.
  Kwenye tope kanyaga twende
   
 14. B

  Baba Tina Senior Member

  #14
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) umeibuka an kuitaka serikali isiilipe kampuni ya DOWANS. Vuguvugu hilo liliibuka kwa mara ya kwanza juzi na baraza la umoja wa vijana mkoa wa Mara ambao uliitaka CCM kuitamka kampuni ya dowans kua ni kampuni hewa na hivyo haistahili kulipwa chochote..

  Jana pia tumeshuhudia kamati ya utekelezaji ya UVCCM taifa ikipita kwenya mkondo uleule na kuitaka serikali isiilipe kampuni ya dowans na pia iwataje wamiliki wa kampuni hiyo. Nimetafakari kwa kina na kujiuliza UVCCM wametoa wapi ujasiri huu wa kugusa maslahi ya wakubwa. Nionaavyo mimi UVCCM wanatumiwa kufanya sanaa ili kuuaminisha umma kwamba CCM wanachukia dowans kulipwa mabilioni hayo ya pesa. Wameamua kujitokeza baada ya kuona kauli za kupinga malipo ya Dowans zimeongezeka na nyingine zikitoka kwa watu mashuhuri hivyo na wao wakajipenyeza humohumo.

  Inaniwia vigumu kuamini kua UVCCM wana nia ya dhati kupinga malipo ya dowans. Nahisi ni njama za CCM kukisafisha na kukitenga chama hicho dhidi ya ufisadi wa DOWANS. Wanataka tuamini kwamba CCM inachukia ufisadi wa dowans na kwamba wanachukia nchi hii kutafunwa na watu wachache. Nadhani UVCCM wametumia strategy nzuri ya kujaribu kukirudisha chama chao kwenye chati baada kupoteza dirakatik uchaguzi mkuu uliopita.

  Nawasilisha.

   
 15. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unaulizia busha Bagamoyo?!! Gazeti haliuzi, unategemea hela ya mishahara itapatikana wapi kama sio consolidated sources za mmiliki?!!
   
 16. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  Rostam Aziz yuko kazini
   
 17. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli mambo ni magumu kwa mwananchi wa kawaida. Kwa maisha kama haya, sidhani kama inawezekana kuwa na tabaka la kati lenye nguvu kama inavodaiwa!Hapa tutaishia kuwa na matabaka mawili tu, la juu sana la hao wenye nacho na wanaoendelea kufaidi daima dumu.
  Mkuu katika vitu ulivyotaja umesahau kutaja 'gesi'. maana nayo imepanda kwa bei ya kutisha!Katika hali kama hii unategemea miti itanusurika kwa shoka la mchoma mkaa?

  Nakumbuka slogan ya chama kimoja cha siasa hapo siku za nyuma ilikuwa, ''saa ya ukombozi ni sasa!'' Jamani watanzania, saa ya kujikomboa ni sasa!
   
 18. M

  Mwasongwec Member

  #18
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 15, 2007
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  21st January 2011
  Nipashe
  Kilichowasilishwa ni viambatanisho tu
  Mahakama yasema bado inaisubiri

  Siku tatu baada ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ignas Kitusi, kueleza kwamba, hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) iliyoamua kesi ya kampuni ya Dowans Tanzania Limited dhidi ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), imewasilishwa Mahakama Kuu, sasa imebainika kilichowasilishwa mahakamani hapo si hukumu, bali viambatanisho vya mwenendo wa kesi hiyo.

  Hukumu hiyo iliyotolewa na ICC iliyoko nchini Ufaransa, Novemba 16, mwaka jana chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker, inaiamuru Tanesco kuilipa Dowans Sh. bilioni 94, zikiwa ni fidia ya kuvunjiwa mkataba wake (Dowans).

  Habari kutoka Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam zilizothibitishwa na baadhi ya maofisa waandamizi wa mahakama hiyo, zinaeleza kuwa viambatanisho hivyo vilibainika baada ya Ofisi ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambayo inashughulikia suala hilo, kufungua kifurushi kilichohifadhi nyaraka hizo.

  "Hadi sasa hukumu ya ICC bado haijawasilishwa mahakamani. Kitusi alipoeleza vile, kifurushi kilikuwa hakijafunguliwa. Alitoa jibu la jumla. Kilichowasilishwa na ICC ni Annexture (viambatanisho vya mwenendo wa kesi) ile," alisema Afisa mmoja mwandamizi wa Mahakama Kuu kwa sharti la jina lake kutochapishwa kwa maelezo kuwa sio msemaji.

  Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, hukumu hiyo inaitaka Tanesco kuilipa Dowans Tanzania Limited dola za Marekani 65,812,630 (Sh. bilioni 94) zikiwa ni fidia ya kuvunjiwa mkataba wake.

  Ngeleja alisema malipo ya fidia hiyo hayatafanywa endapo hukumu hiyo haitasajiliwa katika Mahakama ya Tanzania.

  Wakati hayo yakijiri, habari zilizothibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Francis Kiwanga, zinaeleza kuwa wanaharakati wa mashirika 17 nchini, jana waliwasilisha barua Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba waruhusiwe kupeleka maombi ya kutaka hukumu hiyo ya ICC isisajiliwe katika mahakama yoyote itakapopelekwa.

  Akizungumza na NIPASHE jana mara baada ya barua yao kuwasilishwa Mahakama Kuu, Kiwanga alisema nakala ya barua hiyo wameipeleka kwa wasajili wote wa Mahakama kwa vile wana maslahi na hukumu hiyo kwa niaba ya Watanzania.

  Alisema wamelazimika kufanya hivyo baada ya kusikia kuwa hukumu hiyo imewasilishwa Mahakama Kuu wakati walikwisha kufungua kesi kupinga suala hilo katika Mahakama ya Biashara, ambayo hadi sasa haijasajiliwa.

  Kiwanga alisema kesi yao imeshindwa kusajiliwa katika Mahakama ya Biashara kwa vile hukumu hiyo ya ICC haijawasilishwa katika mahakama hiyo kwa ajili ya kusajiliwa.

  Wanaharakati hao kupitia mashirika 17 yasiyokuwa ya kiserikali, walifungua kesi hiyo katika mahakama hiyo kuitaka ikatae kusajili hukumu hiyo ya ICC ili kuzuia malipo hayo kufanyika kwa Dowans.

  Hata hivyo, kesi ya wanaharakati hao awali ilielezwa kuwa imesajiliwa na kupewa namba 4 ya mwaka 2011 na kupangiwa Jaji Robert Makaramba.

  Prof. Saffar naye aipinga Dowans

  Wakati huo huo, mwanasheria aliyebobea, Profesa Abdallah Saffar, amesema hakuna haja ya kulipa fedha hizo kwa sababu kampuni hiyo ilirithi mkataba mwenye utata.

  Profesa Saffar alisema hata sheria za kimataifa zinasisitiza haja ya kuheshimu mikataba ya kimataifa, lakini iliyo halali.

  "Sheria za kimataifa hazisemi tuheshimu mikataba feki kama huu wa Dowans unaojulikana wazi kwamba kulikuwa na mizengwe na mazingira ya rushwa," alisema.

  Alikumbusha kwamba mwaka 1961 baada ya Tanganyika kupata uhuru, Mwalimu Julius Nyerere alitangaza kutoutambua mkataba wa Mto Nile uliokuwa ukizikataza nchi za Afrika Mashariki kutumia maji ya ziwa Victoria na Tanzania haikupata madhara yoyote.

  "Mimi nakubaliana kabisa na Samuel Sitta (Waziri wa Ushirikiani wa Afrika mashariki) kwa sababu hakuna sababu yoyote ya kuilipa kampuni ya Dowans, kufanya hivyo ni kutapanya rasilimali za taifa," alisema Profesa Saffar.

  Alisema Ibara ya 9 (c) ya Katiba ya nchi, inaeleza pamoja na mambo mengine, kuwa shughuli za serikali zitatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine.

  Amepinga azma ya serikali kuilipa kampuni ya Dowans siku chache baada ya Waziri Sitta kueleza waziwazi kwamba ulipaji wa Dowans ni sawa na kuhujumu uchumi kwa kuwa ni mpango wa watu watatu wenye malengo ya urais mwaka 2015.
   
 19. V

  Vipaji Senior Member

  #19
  Jan 21, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana Prof. Safari. Wazungu wakati wote wanafurahia kuona nchi za Afrika zinazidi kuwa maskini. Ili watengeneze ajila kwa ajili yao. Imefika wakati wote tuungane hii HATUILIPI Dowans iwe sauti yetu watanzania.
   
 20. K

  Kibori Member

  #20
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Please understand that, as part of sharing knowledge it is also prudent to discuss issues of great importance, which have also captured the attention of the general public, here at the forum.I urge all lawyers to stand and support this topical issue. May I provoke you therefore. Karibuni
   
Loading...