Kizungumkuti Dowans

Mkuu,
Hapa JF inajulikana kuwa kuna chama kimoja tu cha upinzani. Hata wewe huwa unadiscourage ushirikiano wa Upinzani katika threads nyengine. Kama umebaini udhaifu huu basi tushabihishe upinzani wafanye kazi kwa pamoja ili wapate kutumia nguvu ya sauti yako kukuza kilio cha wananchi kwa serikali.

Chama kimoja kimoja bado ni weak, inapopambana na chama cha dola au dola yenyewe. Tunajua kuwa serikali ni CCM na CCM ni serikali.
wanafanya watakavyo. sasa huu wito wako ni mzuri lakini tuwasaidie vyama vya upinzani kwa kuwataka wafanye kazi ya kuwawakilisha wananchi bila ya kuweka maslahi ya chama mbele, utaifa mwanzo.

Hongera kwako kwa kauli hii,"Katika hili kofia ya CDM nitaiweka pembeni kwa muda nakujikosoa mwenyewe"
Sasa elewesha na CDM wengine ili waone haja ya kuacha malumbano yasiyo na tija ya kuita vyama vyengine CCM-B, C, D, wameolewa, wanandoa, wanalala kitanda kimoja na kama hayo haya yanarudisha nyuma upinzaniMaslahi ya taifa mwanzo na matatizo ,shida za wananchi kama ulivyoyataja yako mengi na yanahitaji kupatiwa ufumbuzi.
 
Wasalaam,

Leo wanaJF tuvisaidie vyama vyetu vya upinzani kujua wajibu wao wakati wa matatizo kama huu.

Je ni makosa kwa vyama hivyo kuchukulia matatizo yetu kama mtaji wao wa kisiasa kuingia ikulu au kuchukua madaraka?

Naamini wapo baadhi ya viongozi kama sio wote wa vyama vya upinzani wanafurahi matatizo yanayotokana na udhaifu mkubwa wa chama tawala hivyo basi badala ya kusaidia utatuzi wa matatizo hayo wao wanasubiria muda wao ufike! Je wanaamini kwamba wakiingia madarakani ndio watatatua matatizo ya wananchi? Je ni kwa kiasi gani wananchi waendelee kusubiri ukombozi wao?!

Je vyama vya upinzani vina nafasi gani ya kusema na kutetea wananchi katika haya yafuatayo,

1. Malipo ya Dowans

2. Deni la taifa

3. Migomo ya wanafunzi

4. Kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne

5. Ukosefu wa ajira

6. Na mengine mengi!

Nini wafanye? Au wasubiri zamu yao wakiwa madarakani? Nini mawazo yako ewe Mfikiri Mkuu 'Great Thinker'?

Usihangaike sana,Chukua ilani za ccm,chadema,cuf,appt maendeleo na vinginevyo utapata majibu ya moja kwa moja wala usiumie kichwa.Kikwete na CCM yake wameshindwa kabla hawajaanza!!Aluta continua!!
 
Back
Top Bottom