KIWIRA na MCHUCHUMA: A Campaign To Reclaim...

Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamini Mkapa
*Serikali yasema ni mtu safi, mcha Mungu
*Hamiliki akaunti nje ya nchi wala ndege
*Hata Kiwira anashindwa kulipa mishahara
*Yasema shukrani ya punda daima ni mateke

link hii: Tuhuma za ufisadi, Mkapa asafishwa
 
Nimesoma article kwenye hiyo link mkuu. Watanzania tulikuwa tuna tegemea nini? Ndiyo maana ishu ya Kiwira imechukua muda maana walikuwa wana tafuta jinsi ya kumuokoa na aibu huyo mzee. Kama kweli Mkapa alitaka kufufua Kiwira kwa sababu ya hali mbaya kama Pinda alivyo sema kwa nini hawakutafuta mwekezaji wa maana? Kwa nini raisi ajiingize kwenye mambo ya kibiashara kama haya ambayo mwisho wake ni kuumbuka? kama kweli alikuwa na nia nzuri basi angetafuta mwekezaji wa maana ambae angeendeleza mgodi huwo. Nakuambia serikali washamtafutia back door Mkapa atoke zake.

Na hiyo ya kuwa mfumo wetu sijui unazuia mtu fisadi kuwa raisi is a BIG lie. Hawawezi kutuambia mfumo wetu is ufisadi proof wakati mambo yanayo tokea sasa suggest otherwise.
 
Nziku.. sidhani kama kuna mjadala.. uamuzi umeshachukuliwa. Kiwira inarudishwa serikalini. HIvyo ndivyo nilivyoipata sijui technicalities zake.

Ni kweli naona magazeti yote yameandika na pinda amenukuliwa akisema mkapa hana account nje ya nchi, hana ndege kwa hiyo kiwira ni kosa moja na wananchi tusisahau uungwana wa mkapa.

Sijui Mzee Mwanakijiji unalionaje hili la ku-reclaim kiwira, lina tija??
 
Deni lililopo atalipa nani kati ya serikali na Mkapa?.

Mgodi unarudi serikalini ama serikali inaununua upya mgodi huo toka kwa Mkapa?

Pinda aulizwe deni litalipwa na nani? na kwa njia gani?
 
Kuna tatizo kubwa sana linaendelea katika system zetu;

I feel sorry fo BMW , I believe he had good motives but wrong approach and timing!

In short hakuna mwekezaji yeyote anayeweza kuwekeza ule mgodi, believe me natokea hapo hapo, inamnataka mtu mwenye nguvu sana serikalini ili aweze kupambana na TANESCO. Mkapa was the best one, but kwa cheo chake na ethics havikumruhusu ndio maana nikasema wrong timing.

Sijajua je, baada ya kuondoka madarakani angeruhusiwa kuuchukua??????
 
Ni kweli naona magazeti yote yameandika na pinda amenukuliwa akisema mkapa hana account nje ya nchi, hana ndege kwa hiyo kiwira ni kosa moja na wananchi tusisahau uungwana wa mkapa.

Sijui Mzee Mwanakijiji unalionaje hili la ku-reclaim kiwira, lina tija??

Mkapa hakuwa na nia nzuri hata kidogo katika hili suala la kiwira.
- Kama Raisi wa nchi hakupaswa kufanya biashara akiwa ikulu.
- Sheria za ubinafishwaji hazikufuatwa, bali tamaa iliwekwa mbele.
- Alitumia pesa ya wananchi kujichukulia mgodi huo

Kwa kifupi sioni sababu ya kuwa na Mkapa uraiani kwani ilibidi awe kifungoni muda mrefu uliopita.
Matatizo mengi tuliyonayo Tanzania kwa sasa chimbuko lake ni Mkapa ama wakati wa utawala wake.
 
Deni lililopo atalipa nani kati ya serikali na Mkapa?.

Mgodi unarudi serikalini ama serikali inaununua upya mgodi huo toka kwa Mkapa?
nakuunga mkono, sio kurudisha tu , je madeni yake yanakuwaje, na pia hilo kosa lazima iwe na adhabu yake ili mtu mwingine asijaribu kufanya kosa kama hili, na hilas la kiwira ni moja tu, lipo la kuwaingiza kwanguvu net group,mkewe kuchukua mali za ttcl na posta, misamaha ya kodi ya madini, rada, ndege ya laisi akishirikiana au akimtumia waziri wa fwedha wa wakati huo etc etc. Pinda asitake kumaliza hii issue kisiasa ni kulea ugonjwa., wakati matatizo haya yahitaji dawa ya kudumu.
 
nakubaliana nawewe 100%, hapa Pinda kapindisha hoja, na kuleta siasa, anapo sema atahakikisha shea zote zina rudi serikalini kivipi? mbona hili haliweki wazi, kwamba tangu leo huo mgodi ni mali ya serikali kwa vile sheria hiii na hii haikufuatwa?

Huu ni mkenge mwingine, watatumia mabilioni yetu kuwahonga wezi wa mgodi wetu kwa kisingizio cha kununua na kurudisha shea zote serikalini! Tumeliwa wakuu.
 
Mkapa hakuwa na nia nzuri hata kidogo katika hili suala la kiwira.
- Kama Raisi wa nchi hakupaswa kufanya biashara akiwa ikulu.
- Sheria za ubinafishwaji hazikufuatwa, bali tamaa iliwekwa mbele.
- Alitumia pesa ya wananchi kujichukulia mgodi huo

Kwa kifupi sioni sababu ya kuwa na Mkapa uraiani kwani ilibidi awe kifungoni muda mrefu uliopita.
Matatizo mengi tuliyonayo Tanzania kwa sasa chimbuko lake ni Mkapa ama wakati wa utawala wake.
Nilibahatika kuipata document aliyoandikwa na mwandishi mmoja alioongozana na kamati ya bunge ilikwenda kiwira kupata undani wa mmiliki wa kiwira.ducument hiyo aliifax usiku uleule hakukuwa na jina la benjamin bali la mtoto wake.Ninachoshangaa iweje tunang'ang'ania kuwa ni Benjamin.kwakweli nninadhani hatumtendei haki.
 
Huyu jamaa ni mwizi na fisadi tuu.Hana utaifa hata kidogo.
 
Serikali wameona mbali maana sijui BWM angekimbia vipi hii kashfa ya kujitwalia ule mgodi. Wayamalize na mengine yote badala ya kujaribu kufukia chini ya kapeti ili tuachane na ufisadi sasa na kufikiria maendeleo.
 
Hizi ni Kampeni kabla ya muda wake, Walikuwa siku zote na ndio siku hizi wanakuja kufanya hivyo, Yako wapi Meremeta, Kagoda na uchafu mwingine?? Mbona tunaona haya tu?? Mbona wanasema kuwa ni ya Mkapa?? Mbona wanakataa ukweli kuwa alifanya biashara akiwa Ikulu, Lazima watazame kwanza alianza kumiliki Lini?? Mbona wanachuku bila ya maelezo ya Kutosha kama alifanya sahihi
 
Kwa kifupi sioni sababu ya kuwa na Mkapa uraiani kwani ilibidi awe kifungoni muda mrefu uliopita.
Matatizo mengi tuliyonayo Tanzania kwa sasa chimbuko lake ni Mkapa ama wakati wa utawala wake.

Ni busara kufikiria zaidi ya hapo! Kwa mtazamo wangu nafikiri watanzania wote tunatakiwa kubadili tabia, mitazamo, na kadhalika. Mpaka dakika hii hakuna rais wa Tanzania aliyepita bila kulalamikiwa kwa chochote. Hata baba wa Taifa Mwl Nyerere alionekana kama ni chanzo cha matatizo mengi ya Tanzania, tukumbuke huyu mzee tulimpamba zaidi baada ya kufa. Natabiri, Mkapa anaweza kutajwa kuwa ni rais bora zaidi Tanzania mara baada ya Mungu kumpumzisha kwa amani.

Sifagilii kitendo cha kujipatia Kiwira kwa style aliyotumia. kama binadamu nilitegemea Mkapa asingeweza kuwa mtakatifu kwa miaka yote 10 ya uraisi wake. Tunaongelea mengi mabaya aliyoyafanya au tunayohisi ameyafanya, Lakini kama watu tunaofanya arguments based on facts mbona hatugusii na mazuri pia ili tupime performance ya utawala wake
 
Unajua Mwanakijiji ukiamua kushinda uoga kuthubutu kurudi nyumbani na ukaendeleza hizi kampeni zako katika mikakati rasmi utalisaidia sana Taifa.....

Huu utamaduni wa kubwekea nje ya uzio wa nyumba ni mojawapo ya upotevu wa RESOURCES adimu tulizonazo katika kusukuma gurudumu la DEMOKRASIA nchini.

omarilyas
Mkuu,
Wazo lako ni sawasawa, ila mda mwafaka bado haujafika mwache aendelee kubadilisha fikra za watanzania kwanza.Fikra zikishakomazwa basi sisi tunaofuatilia upepo hapa nyumbani tutamtaarifu kuwa tayari watu wameshaamka.Matokeo ya Busanda ilikuwa barometer yetu,dalili zimeshaanza kuonekana.Namuomba mwanakijiji aelekeze nguvu zaidi kubadilisha fikra za DPP,TISS,Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi.Hili eneo bado halijaguswa kwenye ukombozi wa kifikra.Ushuhuda kwa mliofuatilia chaguzi zetu ndogo mtakubaliana na mimi kuwa tatizo sio wapiga kura.Tatizo ni taasisi zinazosimamia uchaguzi ndiyo kikwazo kikubwa. cha kupata uongozi unaowajibika.
 
SaidSabke:
Nilibahatika kuipata document aliyoandikwa na mwandishi mmoja alioongozana na kamati ya bunge ilikwenda kiwira kupata undani wa mmiliki wa kiwira.ducument hiyo aliifax usiku uleule hakukuwa na jina la benjamin bali la mtoto wake.Ninachoshangaa iweje tunang'ang'ania kuwa ni Benjamin.kwakweli nninadhani hatumtendei haki.

Huyo mwanae ange-dream kuupata mgodi huo kwa chee kama ding wake hakuwa Ikulu? Katika masuala haya, scandali inabaki pale pale kwa BWM, alitumioa vibaya madaraka yake.
 
Ni busara kufikiria zaidi ya hapo! Kwa mtazamo wangu nafikiri watanzania wote tunatakiwa kubadili tabia, mitazamo, na kadhalika. Mpaka dakika hii hakuna rais wa Tanzania aliyepita bila kulalamikiwa kwa chochote. Hata baba wa Taifa Mwl Nyerere alionekana kama ni chanzo cha matatizo mengi ya Tanzania, tukumbuke huyu mzee tulimpamba zaidi baada ya kufa. Natabiri, Mkapa anaweza kutajwa kuwa ni rais bora zaidi Tanzania mara baada ya Mungu kumpumzisha kwa amani.

Sifagilii kitendo cha kujipatia Kiwira kwa style aliyotumia. kama binadamu nilitegemea Mkapa asingeweza kuwa mtakatifu kwa miaka yote 10 ya uraisi wake. Tunaongelea mengi mabaya aliyoyafanya au tunayohisi ameyafanya, Lakini kama watu tunaofanya arguments based on facts mbona hatugusii na mazuri pia ili tupime performance ya utawala wake
Ndugu,
iwapo yapo mazuri aliyoyafanya Mkapa wakati wa urais wake basi unapaswa kutambua kuwa huo ulikuwa wajibu wake. Ukumbuke pia kuwa aliomba urais kutenda mazuri, siyo kuiba kiasi chochote cha mali ya umma!
 
Ni busara kufikiria zaidi ya hapo! Kwa mtazamo wangu nafikiri watanzania wote tunatakiwa kubadili tabia, mitazamo, na kadhalika. Mpaka dakika hii hakuna rais wa Tanzania aliyepita bila kulalamikiwa kwa chochote. Hata baba wa Taifa Mwl Nyerere alionekana kama ni chanzo cha matatizo mengi ya Tanzania, tukumbuke huyu mzee tulimpamba zaidi baada ya kufa. Natabiri, Mkapa anaweza kutajwa kuwa ni rais bora zaidi Tanzania mara baada ya Mungu kumpumzisha kwa amani.

Sifagilii kitendo cha kujipatia Kiwira kwa style aliyotumia. kama binadamu nilitegemea Mkapa asingeweza kuwa mtakatifu kwa miaka yote 10 ya uraisi wake. Tunaongelea mengi mabaya aliyoyafanya au tunayohisi ameyafanya, Lakini kama watu tunaofanya arguments based on facts mbona hatugusii na mazuri pia ili tupime performance ya utawala wake
Mkuu hapa hata sielewi unachojaribu kusema pengine ndizo tofauti za imani na tafsirii kati ya Waislaam na Wakristu..
Nasema hivi kwa sababu:-
Waislaam wanaamini kuwa Motoni (Jahanam) kuna MOTO na Peponi kuna PEPO..(Motoni=moto; Peponi=pepo)
Na upande wa pili Wakristu wanasema Motoni kuna MOTO, huko Peponi haijulikani! kwa sababu PEPO kwa tafsiri yao ni SHETANI..Hivyo, haiwezekani Peponi kuwa na Pepo...

Sasa pengine lugha zetu zina mtazamo tofauti ktk tafsiri, labda tueleze vizuri unachojaribu kusema hayo mazuri ya Mkapa. maanake navyofahamu mimi hata jambazi linalofungwa maisha huwa limefanya mazuri ambayo yanaweza kuhesabika!..Kinachomweka hatiani sii mazuri yake bali kitendo kimoja kiovu alichokifanya...
 
Back
Top Bottom