Kituo cha Afya Fore Plan Clinic chafungwa

Kituo cha Afya Fore Plan Clinic chafungwa

Sasa dawa mbaadala si hiyo mitishamba na matunda? Unahitaji wataalam wa aina gani? Mbona wamejaa tele huko mjini hadi wamaasai. Kusema tu hawajatimiza vigezo haitoshi. Watoe details ili watumiaji wajue na wajihadhari.
 
Wizara ya Afya imekifunga kwa mda usiojulikana kituo cha Fore plan Clinic kilichopo ilala Bungoni. Kituo hiki kinamilikiwa na Dr J.J Mwaka mtaalam wa magonjwa ya kinamama akitibu kwa kutumia tiba mbadala.Wizara imesema kituo hakijatimiza vigezo na masharti yanayotakiwa na serikali ikiwemo kutokuwa na wataalam wenye sifa na elimu stahiki.Dr J.J Mwaka amekuwa akionyesha kazi nzuri za kituo chake kwenye vyombo vya habari ikiwemo kutibu ugumba na upungufu wa nguvu za aina mbalimbali.Watu wengi wamekua wakifurahia sana tiba hii mbadala itolewayo na Dr Mwaka na mpaka kituo kinafungwa wagonjwa wengi walikua wakisubilia huduma.
Dr bila digree. ujinga na wizi. wanachukua dawa za hospitali zikiwe ARV s na kuchanganya na miti shamba. ubatili mtupu
 
Dr bila digree. ujinga na wizi. wanachukua dawa za hospitali zikiwe ARV s na kuchanganya na miti shamba. ubatili mtupu
Kuna maduka ya dawa mbadala dawa za asili,wengi Wenye maduka Hawa,hawana elimu ya tiba mbadala,pia wangetizamwa kwa jicho LA tatu,afya ni muhimu,wanawapa watu dawa bila vipimo na maelekezo ya kubahatisha,wako kibiashara zaidi,sio kuwasaidia wagonjwa.
 
Clouds Tv na radio nao vipi, maana huwa wanamshadidia sana
 
Lakini nimejiuliza kitu kimoja! Hivi karibuni huyu bwana anashindana matangazo na kampuni za simu na coca cola kwenye television za hapa nchini, na kwenye ma blog mbali mbali n.k. Najua biashara ni matangazo na matangazo ni ghali. Ila swali ninalojiuliza ni hili, haya makampuni niliyoyataja yanatuvuna sana hela kwa uwingi wetu, Je Dr. Mwaka anatuvuna kwa kiasi hicho?
 
Kuhusiana na hili la kufungiwa kwa muda, mwenye ufahamu kwa UNDANI SANA juu ya kitengo hiki TFDA atujuze, hata pamoja na kwamba kazi yake ni kuthibiti but what's extra authority about natural remedies?
Ambayo weeengi naona tunaikataa kwamba si dawa salama na ina garama kubwa?

TFDA Haihusiki na Tiba Mbadala, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ndio jukumu lake, na ndio maana unaona wamemfungia wao na si TFDA.
 
ni kweli, sio msabato ni mwislam anaitwa Juma (J). yeye nilimsikia kwenye tv anasema amesoma degree ya kwanza hapa nchini na ya pili alisoma ya mambo ya kienyeji india. nilimsikia kwa masikio yangu kwenye tv anasema hivyo. alisema amesomea udaktari wa kawaida, akamaliza akaenda kusomea huu wa mimea, hivyo anajua vitu vyote na ni dr halisi. ninyi mnaposema alikuwa anauza mitumba, siamini kwasababu anapoelezea utakuta ni mtu ambaye at least amefika form four au form six and above. pamoja na kwamba, anapoelezea mambo mengine utakuta ni ya layman, si ya daktari bingwa.

all in all, amekusanya hela nyingi sana, ni bilionea, hata wakifunga wanajisumbua kwasababu ameshapata hela nyingi, ataweza kuwekeza kwingine. kama kuchuma ameshachuma za kutosha. jamaa ndi mganga wa tiba asili aliyejimarisha kuliko wote na aliyepata hela nyingi kuliko wote. pale appointments unaenda siku mbili kabla, siku nyingine zote hizi watu wameshabook, na dawa zake ni garmaa sana. malaki. miaka yote hii kila siku amekuwa akikusanya mamiilioni. zaidi ya yote, hawa tfda wanaompinga, huyo jamaa ana hela, atawapa hela kesho tu hapa kituo kitafunguliwa na ataendelea kutoa dawa.

rai yangu ni kwamba, kama kweli hawa watu wawe ni wasababu au waislam, kama wanatoa dawa wakati hawajasomea udaktari, wakamatwe wafungwe kabisa. mke wangu alishawahi kupata tatizo fulani, kaenda sana kwa hao wasababu, kuna msabato mmoja alikuwa kule tabata alikufa tayari, wife alienda sana na kwa hao wote wanaolisha watu malimao na machungwa mia, matokeo yake nilitoa sana hela hakuna kupona, waifu alikuja kuponea kwenye maombi ya kanisani hadi leo mzima. hao majamaa ni waongo ajabu, na wanatisha watu kwa maelezo ya magonjwa wanawapa matumaini ya uongo na kuwapiga hela na kwasababu watu wako kwenye shida mfano ya kupata watoto etc, anaweza kutoa hela yeyote na kwasababu wao wanajua kupata watoto na matatizo ya wanawake ndio mtu anaweza kutoa chochote, basi wanashikilia hapohapo na kuchuma hela za watu.

IMG-20150708-WA0018.jpg
 
Sikutarajia kituo kama hiki kufungiwa sababu dk Mwaka amekuwa akijatangaza sana kwenye radio na tv na niliamini kituo kina vigezo vyote vya kitaalamu vinavyotakiwa

Tatizo la nchi hii ni wahusika wa sekta mbalimbali kuzembea kuchukua hatua stahiki pale kunapojitokeza tatizo. Kama ni uchunguzi utachukua miaka mpaka watoe maamuzi watu wengi wanakuwa wameshaathirika. Tujitokeze kwa wingi tuyaondoe magamba!!!!
 
Afadhali waziri wa afya kidogo umefanya kazi binafsi mimi na familia yangu t7nakupongeza hongera sana waziri wa afya,huyo jamaa ni tapeli wa kufa mtu hafai hata kidogo kisifungiwe tu kifutwe kabisa!

Pole sana mkuu. Tushirikishe na sisi ni lipi baya lilikupata kwa dr. Year?
 
Wizara ya Afya imekifunga kwa mda usiojulikana kituo cha Fore plan Clinic kilichopo ilala Bungoni. Kituo hiki kinamilikiwa na Dr J.J Mwaka mtaalam wa magonjwa ya kinamama akitibu kwa kutumia tiba mbadala.

Wizara imesema kituo hakijatimiza vigezo na masharti yanayotakiwa na serikali ikiwemo kutokuwa na wataalam wenye sifa na elimu stahiki.

Dr J.J Mwaka amekuwa akionyesha kazi nzuri za kituo chake kwenye vyombo vya habari ikiwemo kutibu ugumba na upungufu wa nguvu za aina mbalimbali.
Watu wengi wamekua wakifurahia sana tiba hii mbadala itolewayo na Dr Mwaka na mpaka kituo kinafungwa wagonjwa wengi walikua wakisubilia huduma.

Sina shaka we mleta uzi ndio Mwaka mwenyewe maana ni dr bingwa wa kujipiga prömo. Jamaa amekariri kila vipindi vyake utasikia homonal imbalance na UTI. Hata ukiumwa kichwa atakwambia homon imbalansi.
 
Huyu mwaka si ndo yule anaandaa vipindi anajiuliza maswali na kujijibu mwenyewe!
 
Dr Mwaka anauza mihadarati na hilo wanalifahamu fika polisi na viongozi wakuu. Hiyo ya tiba mbadala ni kusafisha hela chafu tu. Huwezi uza miti shamba halafu ukamiliki mali na maisha yenye ukwasi mrefu kiasi hicho.
 
Sina shaka we mleta uzi ndio Mwaka mwenyewe maana ni dr bingwa wa kujipiga prömo. Jamaa amekariri kila vipindi vyake utasikia homonal imbalance na UTI. Hata ukiumwa kichwa atakwambia homon imbalansi.

Ha hahaha,
 
Back
Top Bottom