AZUSA STREET
JF-Expert Member
- Oct 31, 2013
- 2,007
- 1,898
ni kweli, sio msabato ni mwislam anaitwa Juma (J). yeye nilimsikia kwenye tv anasema amesoma degree ya kwanza hapa nchini na ya pili alisoma ya mambo ya kienyeji india. nilimsikia kwa masikio yangu kwenye tv anasema hivyo. alisema amesomea udaktari wa kawaida, akamaliza akaenda kusomea huu wa mimea, hivyo anajua vitu vyote na ni dr halisi. ninyi mnaposema alikuwa anauza mitumba, siamini kwasababu anapoelezea utakuta ni mtu ambaye at least amefika form four au form six and above. pamoja na kwamba, anapoelezea mambo mengine utakuta ni ya layman, si ya daktari bingwa.Dr mwaka sio msabato ni mwislam alikuwa anauza mitumba ilala baada ya hapo akaingia kwenye ushonaji wa nguo za kike sasa nikaja kushangaa anajiita dr kuna ndugu yangu aliwai kufika clinic kwake akashangaa sana kumwona fundi wake ktk kudadisi pale kijana wake akasema amesomea uarabuni lkn sio kweli
all in all, amekusanya hela nyingi sana, ni bilionea, hata wakifunga wanajisumbua kwasababu ameshapata hela nyingi, ataweza kuwekeza kwingine. kama kuchuma ameshachuma za kutosha. jamaa ndi mganga wa tiba asili aliyejimarisha kuliko wote na aliyepata hela nyingi kuliko wote. pale appointments unaenda siku mbili kabla, siku nyingine zote hizi watu wameshabook, na dawa zake ni garmaa sana. malaki. miaka yote hii kila siku amekuwa akikusanya mamiilioni. zaidi ya yote, hawa tfda wanaompinga, huyo jamaa ana hela, atawapa hela kesho tu hapa kituo kitafunguliwa na ataendelea kutoa dawa.
rai yangu ni kwamba, kama kweli hawa watu wawe ni wasababu au waislam, kama wanatoa dawa wakati hawajasomea udaktari, wakamatwe wafungwe kabisa. mke wangu alishawahi kupata tatizo fulani, kaenda sana kwa hao wasababu, kuna msabato mmoja alikuwa kule tabata alikufa tayari, wife alienda sana na kwa hao wote wanaolisha watu malimao na machungwa mia, matokeo yake nilitoa sana hela hakuna kupona, waifu alikuja kuponea kwenye maombi ya kanisani hadi leo mzima. hao majamaa ni waongo ajabu, na wanatisha watu kwa maelezo ya magonjwa wanawapa matumaini ya uongo na kuwapiga hela na kwasababu watu wako kwenye shida mfano ya kupata watoto etc, anaweza kutoa hela yeyote na kwasababu wao wanajua kupata watoto na matatizo ya wanawake ndio mtu anaweza kutoa chochote, basi wanashikilia hapohapo na kuchuma hela za watu.