Nina jamaa yangu mmoja alikuwaga na demu toka nyanda za juu kusini. Jamaa alikuwaga chap Sana kwenye kutoa. Demu akikohoa tu, jamaa anarespond.
Zikaja tetesi kuwa demu wake anatoka na jamaa mwingine. Mshkaji akabisha. Wadau wakamchorea mchoro, siku hiyo kwenye movie cinema Mlimani City, jamaa anashuhudia demu wake analiwa mate mle ndani. Uzuri jamaa hakupanick, akawashtua kistaarabu tu, kuwa humu tumekuja kuangalia movie, mambo yenu kafanyieni gest.
Demu alikosa amani baada ya kumuona jamaa ndio yupo viti vya nyuma yao. Sisi hatukumaliza movie, tukasepa. Kesho yake jamaa anaenda serikali ya mtaa anaokaa demu, akawaelezea hali halisi ilivyo, then akaomba akachukue vitu vyake tu. Yule demu akaitwa kwanza ofisini, then ndo wakaondoka wote kwenda anapokaa demu ili jamaa achukue vyake.
Sisi wote tulijua jamaa anaenda kuchukua nguo zake na viatu. Ila Cha ajabu, jamaa alichukua hadi nguo alizomnunulia demu, viatu, chupi n.k. Mpaka mjumbe akawa anaulizia sasa hizi chupi unachukua za Nini? Jamaa anajibu simple tu, kuwa huyu anamtu mwingine, nikitoka atamletea vyote hivi.
Jamaa alimsafisha kiasi kwamba demu jeuri ilikata, akawa anaomba msamaha [emoji1787][emoji1787][emoji1787]