Kitisho cha Dr. Slaa si zaidi ya Mrema - Kinana

Kitisho cha Dr. Slaa si zaidi ya Mrema - Kinana

Mkuu acha tuhuma za zamani kuna meno pembe za ndovu zimekamatiwa Zanzibari kwenye makontena yakiwa disguised kama dagaa na vitu vingine!! Meli zilizoyapeleka pale hatujajua ni za nani inahisiwa ni za kigogo fulani, ila CCM kwa kizima mambo sijui kama hilo litawekwa wazi????

Kiongozi hii kashfa ya Kinana na kampuni yake usiiite ya zamani, mimi mpaka leo bado sijasikia meaningful answers in response to this scandal, hili haliwezi likaisha hivi hivi tu kama ambavyo Serikali inataka tulichukulie. Tunataka kujua kama wananchi, who are the people involved kwenye kusafirisha ule mzigo, wamafanywa nini hadi sasa????Kashfa za Ufisadi za zamani kama Deep Green na wenzake, JK na wenzake wanaziita za zamani, hivi ni lini kama Serikali ilitolea meaningful answers juu ya huu ufisadi???Hizi tutaendelea kuziulizia hadi tupate majibu, na masuala haya hata kama wabunge wa sasa wa ccm watayakingia kifua, tukichukua nchi tutayafunua tu and no stone will be left unturned hadi tuisafishe nchi na fedha zetu zirudishwe. Hatuwezi tukaishia tu kukaa kimya wakati hatuna majibu ya maana ya kuwaambia wajukuuu zetu. Maana watatuuliza okay Deep Green/Meremeta/Epa waliwaibia halafu........?????Then tuanza kujiumauma kwenye kutoa majibu Hatuwezi tukawa tunaishia kusema tu tumeibiwa afu tunaishia hapo. We need to know who are behind these dubious deals??

So ndugu yangu pamoja na ukweli kwamba zipo kashfa mpya zinajitokeza kila siku, hizo haziwez kutufanya tuzibe midomo na kuzisahau za zamani ambazo hadi leo hazijataftiwa ufumbuzi. Hili la ZNZ sijalipata bado, ila nifahamuvyo mm znz hawana Tembo wa kujaza container if any. So ni hawa hawa wakwetu huku Bara ndo wanaendelea kumalizwa. Wahusika watakuwa ni wale wale wanaolindwa na askari tunaowalipa mishahara kwa kodi zetu. Its pity!
 
Nape kagonga mwamba kwenye nini?

Kinana kaingia mwenyewe kwenye nini?

Katibu wa CHADEMA kaonyesha kishindo kwenye nini?

1. NAPE kagonga mwamba kwenye propaganda ya Kadi ya CCM ya Dr. Slaa
2. KINANA kaingia mwenyewe kwenye kazi ya kutaka kudhibiti kasi ya Dr. Slaa kisiasa ambayo haiwezi sababu tunamdai meno yetu ya Tembo.
3. Dr. Slaa ameonyesha kishindo kwani alishinda katika uchaguzi mkuu 2010 ila walifanya hujuma ya matokeo na wao wanatambua ndo alitakiwa awe Rais na Mzimu huo ndo unawaandama CCM hadi sasa.
 
Kuelekea 2015 magamba mtasema yote lakini Dr. Slaa mwendo mdundo!
Ni vizuri mkajiandaa kisaikolojia kuwa chama cha upinzani kwakuwa dalili zote zinaonyesha kwamba hamuwezi kunusurika na gharika ya wananchi tunapoelekea katika chaguzi za 2014 na 2015!
Mkuu nakwambia kazi safari hii wanayo, si ulipata habari ya yule kigogo Bulembo alivyo zomewa Musoma pale Mkendo baada ya kukosa majibu ya fedha zetu za Uswiss????Na bado moto huo ni nchi nzima hadi Katavi kwa mtoto wa mkulima!!

 
Tofauti ya Mrema na Slaa mbona iko wazi! Mrema alikuwa na ndoto za Ikulu 1995 ila Slaa 2010 alilazimishwa na chama kugombea na huku akijua kulingana na NEC hangeweza kushinda ila alikubali ili kujenga mtandao wa chama nchi nzima. Hilo CCM wanalijua ila wanajivesha ujinga tuu
 
Mkuu nakwambia kazi safari hii wanayo, si ulipata habari ya yule kigogo Bulembo alivyo zomewa Musoma pale Mkendo baada ya kukosa majibu ya fedha zetu za Uswiss????Na bado moto huo ni nchi nzima hadi Katavi kwa mtoto wa mkulima!!


Mkuu hawa jamaa wana hali mbaya.
 
"Natangaza rasmi kuwa hakuna kama Dr Wilbroad Slaa" Nape na habari zake za kuungaunga
kachemka sasa Kinana rasmi ulingoni kwa mapambano"
 
Kivuli cha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kinazidi kukiyumbisha chama tawala CCM.

Baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuanzisha kampeni za kila aina ya vituko dhidi ya Dr Slaa na kuonekana kugonga mwamba sasa kampeni hizi zimechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kujitosa.

Akizungumza na gazeti la Dira Tanzania Kinana amezungumzia kishindo cha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Slaa na kusema hakimnyimi usingizi.

Kinana amesema pamoja na nguvu za kisiasa alizo nazo Dr Slaa kwa sasa lakini anaamini CCM ilikuwa na wakati mgumu zaidi mwaka 1995 kwani nguvu za Augustine Mrema wa wakati huo zilikuwa kubwa kuliko za Dr Wilbroad Slaa wa sasa.

Source:
DIRA TANZANIA.

huyu kinana naye anaanza kuchemka hivi mwaka 1995 ni sawa na 2012 sijui utakua ni ulevi wa madaraka huu
 
Mkuu mke Dr si mlimpa Udiwani mkawa mnajichukulia kwenye mikutano kama kawaida yenu (Mwigulu Mchemba) sasa wewe ulitegemea huyo mzee wetu afanyeje??? Hata Mandela aliachana na mke mzinzi!!

Mkuu,hiyo bakora imemwingia sawasawa!
 
Ni maneno yenye ukweli Mrema hakuwa na kashfa ndani ya jamii iliyomzunguka na kama zilikuwepo hazikujulikana; Slaa dhambi ya uwongo inamsuta; sijawahi kuona kiongozi asiye na maadili kama Slaa; hainingii akilini kuona mtu anayejinadi ni kiongozi wa jamii kutelekeza familia yake kwa ajili ya kimada na leo atumie majukwaa ya kisiasa kujinadi eti ni mtetezi wa wanyonge ikiwa alishindwa kuitetea familia yake hasa watoto dhidi ya tamaa zake za kimwili leo ataweza kuwatetea watanzania?

Chama
Gongo la mboto DSM

Hapo unachangia kama unaangalha Film ya CYBOG ALIYO IANZISHA NEPI NNAUNYA"political-Cybog in Tanzania".KWA KUWA VI CYBOGS huwa ni Vingi,basi kinana naye ni cybog
 
kweli CCM imechoka kulinganisha VENUS WILIAM NA BACELIONA.

MREMA ALIKUWA KAMA MCHEZA TENIS KWA SABABU ALIKUWA PEKE YAKE NA UMAARUFU ALITOKA NAO MAGAMBANI ILA DR SLAA NA TIMU YAKE NI KAMA BACELONA,TIMU INAPANDA NA KUSHUKA INAKABA INAMILIKI KIUNGO NA INASHAMBULIA MBAYA.

UKISIKIA MTU ANASIFIA TIMU YA MTU MMOJA UJUE IKIJA YA 11 ILIYOKAMILIKA NA BENCHI LAKE LIKO VIZURI ANATAKA KUWEKA MPIRA KWAPANI.

ANAPODAI HANYIMWI USINGIZI NA DR ANANYIMWA NA TEMBO?
 
Kwanza serikali ilianguka Waziri mkuu akamwaga manyanga Lowassa,Baraza la mawaziri limevunjwa mara tatu,waziri wa Fedha wamebadirishwa mara tatu, karibu kila wizara kwa mfano; Waziri wa elimu mara tatu,Nishati na Madini mara nne,Afya mara Tatu,miundo mbinu mara tatu, sheria mara tatu,Bunge masipika wawili,Ardhi mara tatu,Mambo ya ndani mara tatu
Fedha za Wafadhili kila mwaka zinakatwa ,Bado unasema sio tishio yoote hayo na mengine katika miaka saba tu ,Kwa maoni yangu Dr Slaa ni nguvu ya Zege anatisha
 
NAPE ni mwana CDM moyoni mwake ndiyo maana anampigia kampeni dr.slaa kwa njia ya kuanzisha malumbano huku akijua watu wakianza kumjadili DR.tayari image yake inapanda.CCM kazi wanayo kila aliye kijana anayeshabikia CCM usiku wako cdm including NAPE take it or leave
 
jina la dr. Slaa linajadiliwa sana kwa sababu zifuatazo:-
1. Ni kiongozi makini na mwenye busara, hekima na utashi mkubwa
2. Ni mtu muadilifu katika maisha yake
3. Ni mtu mwenye msimamo anayeweza kusimamia jambo analoamini kuwa ni jema kwa utashi mkubwa
4. Ni kiongozi mwenye nidhamu ya hali ya juu sana ktk taifa sasa hivi
5. Ni mtu mwenye moyo wa kuthubutu kufanya lolote wakati wowote ambalo anadhani litakuwa na manufaa kwa wanaomzunguka
6. Ni kiongozi pekee ktk siasa za mageuzi aliyeweza kuwataja kwa majina bila uoga watu alioamini kuwa wala rushwa wakubwa katika nchi hii
na sababu nyinginezo nyingi ambazo zimemfanya awe akiandamwa ktk nyanja zote za maisha yake. Ongeza unazozifahamu
yaani silaa anatwajwa kwelikweli mithili ya akina ponda! Yaani hata ponda pamoja na kutajwa sana mimi si dhani kama kamfikia silaa.
 
Back
Top Bottom